Study tour 2015

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Wanabodi salama?

Nimepanga kufanya study tours za kutosha 2015 ili niweze kuimarisha shughuli zangu za ujasiriamali. Nilishawahi kufanya huko nyuma,niliyoyaona yalinipa hamasa ya kufanya vizuri zaidi. Kama Chasha poultry farm atanipa kibali nitafika Arusha. Plan ni kuona mashamba yafuatayo, ng`ombe,sungura Morogoro,cocoa,kuku/bata,samaki,nyuki,parachichi.

Baadhi nafahamu yalipo,kama unajua shamba kubwa ktk hayo nijulishe ili nilifikie kwa lengo la kujifunza na kupanua uelewa.

Kama kuna kiwanda kidogo cha usindikaji,kisiwe cha alizeti,pia nitapenda kukiona.
 

You have a fantastic idea. Nadhani ungeanza na ku google, then ukaenda kwenye wizara wakupe hizo taarifa. Pia, usisahau kufanya booking mkuu.
 
You have a fantastic idea. Nadhani ungeanza na ku google, then ukaenda kwenye wizara wakupe hizo taarifa. Pia, usisahau kufanya booking mkuu.

Wizara gani mkuu? Hizi za Kikwete? Utakuwa unapoteza muda bure.

Kwa upande wa kuku nitamwomba Chasha/Jilanjo,samaki nitapata wakulima wakubwa kupitia SUA na akina Lady RA, au sarnisa Africa, Cocoa nitawatembelea MOCOA pale Mbingu Ifakara kwa mara ya pili, migomba nitaenda Kilosa kwa Mzungu mmoja hivi,nyuki nitaenda shambani kwa PM pale Dodoma. Sungura nimeshapata kibali pale Morogoro kwa Padri fulani.

Parachichi nitapiga kwata mpaka Kiwira kwa jamaa anayesindika na Njombe kwa jamaa yangu, nitaomba nitembelee mashamba yake kabisa, nitapiga kwata hadi Makete, kuna jamaa ana shamba la kawaida la apples, mwaka jana alipiga bingo sana kwenye maonyesho ya nane nane Mby. Kwa upande wa ng`ombe, ng`ombe ndio bado.
 

Kwa ng'ombe si kuna yule jamaa wa Asas iringa?? Mashamba ya Kitulo je??

Kwani huwezi kwenda nje ya nchi ukajifunza?? Kama uholanzi?? Nadhani kule kuna darasa murua zaidi.
 
Kwa ng'ombe si kuna yule jamaa wa Asas iringa?? Mashamba ya Kitulo je??

Kwani huwezi kwenda nje ya nchi ukajifunza?? Kama uholanzi?? Nadhani kule kuna darasa murua zaidi.

Kitulo napajua, nilifanyia project pale wakati nasoma hawana jipya, kwa Asas pia si pabaya,yupo mzee mmoja namlia timing anipeleke hadi kwenye plant yao ya mtindi.


Nimechelewa mdau wangu aliyekuwa Ug karudi Tz, plan ilikuwa niende Ug nikajifunze kwa prof mmoja,ana shamba la nguvu ktk mazingira ya Kiafrica.
 

Mkuu Malila safi sana kwa plan hiyo nzuri, niko kwenye mipango ya kilimo cha kisasa baada ya kupata land hivi karibuni. Naenda China hivi karibuni kwa madhumuni kama hayo ya kwako na kununua baadhi ya vifaa vya kuanzia. Baada ya study tour yako kama kuna vitendea kazi utavihitaji nipe order nikuletee.

All the best.
 

Kwa sasa natafuta potable water test kit kwa ajili ya maji ya samaki. Kit hiyo natarajia iwe DO tester, salinity,ph tester na thermometer.
 
Reactions: MC
Kwa sasa natafuta potable water test kit kwa ajili ya maji ya samaki. Kit hiyo natarajia iwe DO tester, salinity,ph tester na thermometer.

Ok, nitaweza kukuletea, nime-kuPM for more specifications
 

Mkuu malila hongera sana..Mara zote nisomapo comment zako na thread zako huwa unanipa moyo sana...mungu akubarik...
 
Safi sana,hongera sana na kila la heri, natamani ningejifunza na mimi ila majukumu yanabana sana...
 

Malila Mungu akubariki na aendelee kubariki kazi za mikono yako.........wazo lako ni nzuri saana naomba na mimi nikuunge mkono kwenye mambo mawili......Mosi ni ufugaji wa ngombe na kilimo cha Apple........nianze na Ufugaji wa ngombe......kwa Tanzania wapo wafugaji wenye mashamba mazuri na mbegu nzuri saana za ngombe LAKINI hawajitangazi...na taarifa zao ni ngumu saana kuzipata kwenye vitabu au mitandaoni.......hawana website wala kwenye mitandao ya kijamii hawapo...........mimi nimefanya utafiti wa ngombe wa maziwa na nyama...tangu mwaka 2012...nilijaribu kuangalia maeneo mawili...ufugaji kwa lengo la kuuza maziwa..na ufugaji kwa minajili ya nyama...nilichogundua..na kuambiwa....watanzania hatuna utamaduni wa kunjwa maziwa....familia zetu maziwa sio kipaumbele...Kenya kwenye kila mlo maziwa yanakuwepo mezani...so... soko la maziwa lipo kubwa saana Kenya na wanaviwanda vikubwa saana vya maziwa na viwanda bingi vidogodogo vinavyomilikiwa na cooperative society.....tambua brookside walinunua kiwanda kikubwa cha serekali cha maziwa kilichokuwa Arusha baada ya kufanya market analysis walikigeuza sehemu ya kukusanyia maziwa..baadae wakafnga kabisa na kuondoka......MBEGU BORA ZA NGOMBE KWA TANZANIA.......ukimtembekea SHASHA pitia na National Artificial Insemination Centre...kipo USA river wana mashahawa ya mpwapwa breed na ngombe wengine ushauri watakupa mzuri tu....ASAS unaweza watembelea ila ukiwaandikia mail wala simu hawpokei wala hawajisumbui kujibu...ni wakala wa VIKING GENETICS YA DENMARK WANAUZA MASHAHAWA YAO.......Ukiweza pia kuna mkulima moja wa kingereza yupo iringa anaitwa Philips sina contact ila ukiulizia tu anajukikana saana.......ILA NAKUSHAURI tunisha budget yako utembelee Kenya na hapa NA RECOMEND SHAMBA MOJA TU.......ukiwatemebelea TASSELS DIARY FARM (WATAFUTE FACE BOOK AND WANAWEBSITE YAAO) wana kila kitu kuhusu ngombe na elimu wanayotoa lazima ushibe kabisa wala hutatamani tena kutembelea wafugaji wengine........http://www.tassellsdairyfarm.net/...........hawa ni mtu na mke wamebobea kwenye ufugaji wa ngombe wa maziwa, mbuzi,kondoo na ngombe wa nyama...ni wataalam kweli......kuhusu ngombe wa NYAMA kuna ngombe wanaitwa FLECKVIEH...kampuni inaitwa,..... Fleckvieh Genetics East Africa..... ukipata hawa ngombe madume 20 ndani ya miezi sita ....wanaweza pata uzito mpaka wa kilo 300......watafute facebook na hata you tube utawapata..http://www.fleckviehgeneticsea.com/................kilimo cha APPLE nilikuwa nahisi apple zinalimwa tu sehemu kama lushoto na Iringa KUMBE kuna APPLE unaweza ziotesha hata hapa dar es salaam na zikakuwa vizuri kabisa....kuna wamarekani walishafanya reseach na kuja na matokeo mazuri kabisa wanaitwa KUFFET CREEK ......http://www.kuffelcreekapplenursery.com/.......Wanazo mbegu za kutosha unaweza otesha sehemu yoyote na ukavuna vizuri tu..Kuffel Creek Apple Nursery of Uganda, Ltd.
PO Box 74857 (Ntinda-Buye, Kiwatule Road) Kampala, Uganda Tel/Fax +256 312 266 244
jb@kuffelcreekapplenursery.com cell +256 752 651 834
www.kuffelcreekapplenursery.com
____________________________
Pricing: 10-99 $8 each, 100-999 $7 each, 1000-4,999 $6 each,
$5,000+ $5 each tree; email first for shipping quote. Payment and Import Permit are
required prior to shipping; order is not confirmed until the Import Permit is received..........................................kwa leo naomba ni ishie hapa kama kuna mtu atakuwa na swali kuhusu niliyoyaandika ..........akiuliza naweza toa ufafanuzi..........mniwie radhi kwa maelezo marefu
 

Ameni,

Nimefungua hizi website,nimepata nguvu ya ajabu sana. Nimeanza kukusanya ndama japo wa kienyeji,lakini picha yangu ni kubwa. Ziara ya A town ni pamoja na kufika Tanapa Hq, pia kuna shule moja binafsi kali sana nitaipitia,nitamfikia Chasha kuchukua uzoefu na kuona uwezekano wa yy kuniunganisha na wabobezi wa Kenya.

Yupo Dr mmoja wa mifugo hapo A town, alichukua sungura Moro tukiwa wote na anajua mbuzi wa pacha tatu walipo. Nitaingia A kwa kazi nzito kidogo. Nimesoma mahali, kuwa kuna shamba linaitwa Tanzania poultry farm mitaa ya Ngurdoto A town. Kuhusu apples, nitamfikia Kambarage Sanga,alichukua tuzo ya matunda mwaka jana, huyo namfikia pasaka mwaka huu. Kwetu vyote hivi vinawezekana kabisa,tayari eneo la kuanzia nishapata.
 
Hongera sana mkuu...samahani naomba kujua mahali anapopatikana huyo padri hapo moro,nina mpango wa kujifunza ufugaji wa sungura mkuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…