SUA wataka maelezo: Kwanini wapelekewe Mwizi kuwaongoza?

SUA wataka maelezo: Kwanini wapelekewe Mwizi kuwaongoza?

Suala la kuangalia hapo ni kuhusu mchakato wa hizo ajira zao ulikuwaje? Kama zilikuwa za upendeleo ndio tujadili lakini suala la kusema tu watoka sehemu moja halina mashiko, na isitoshe nadhani wana sifa za kutosha kwa hayo madaraka walio nayo. Pengine penye utata ni hapo kwenye uteuzi wa Chairman of the Council, kama hana uadilifu ni hoja ya kujadili lakini je upo udhibitisho?

Watanzania tusianze kujadili makabila yetu tujadili uwezo wa mtu, mbona taasisi nyingi tu zinaongozwa na watu toka sehemu moja na wanafanya kazi vizuri tu?
 
SUA ni chuo cha watanzania kwahiyo watanzania wote wanayo haki ya kufanya kazi hapo ikiwa ni pamoja kuteuliwa kushika madaraka ya juu katika chuo hicho. Haiwezekani na haikubaliki kuona watu wa kutoka sehemu moja tu ya nchi wakijimilikisha kuiongoza taasisi ya umma kama vile hakuna wataalamu wa fani hiyo wa kutoka maeneo mengine ya nchi.

Tusipokuwa wakali na kukemea tabia hizi za kupendeleana halafu mtu anakuja kutoa sababu nyepesi nyepesi tu kwamba hakuna ubaya, kama kungekuwa hakuna ubaya kwanini watu wanalalamika? lazima watanzania tubadilike ili sote kwa pamoja tushirikishwe katika ustawi wa nchi yetu.

Ni kweli kaka, inabidi Watanzania tubadilike kwa kuanza na wabunge wa viti maalumu kutoka kwenye chama chetu pendwa. Ambapo asilimia kubwa wametoka kaskazini au wana undugu na watu wa makao makuu ya chama.
 
MchunguZI ulitaka wajae Wachagga na Wasukuma?

mchagga kwenye nchi hii anakumbukwa kwenye kazi ngumu zisizo na malipo bora tu, hapo mchagga akiwepo hamna ukabila! lakini kosa mchaga akiwa kwenye kazi nzuri mfano TRA tayari hoja ya ukabila inaanza kutoka kwa vilaza wa nchi hii.
 
Thread hii ni ishara ya watanzania kuanza kuzungumzia ukabila!Naona kama huenda muda umefika wa Taifa langu kuvunjika.Kwani mijadala kama hii,kwa sie tuliomchanganyiko wa makabila tofauti,inatutisha sana kwani siku haya yakikomaa,tutasimamia upande upi?Ingawa yamekuwepo na mimi ni muathirika wa tabia hizi za ukabila sehemu nilipokuwa nafanyia kazi,hata hivyo sikutaka kuamini kuwa yamefikia huko.Tuoneeni huruma ninyi mliopewa dhamana ya kuongoza nchi hii, ili Taifa langu lisisambaratike!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mkataeni.... Kama mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu ndio 'Chancellor' hafai.
 
Aliyemteua ujue ndo mwizi zaidi.....
 
Viongozi wa SUA waliotangulia: Prof Msolla (Iringa), Prof Luoga (Ruvuma). Uongozi wa Mwaka 2015 Makamu Mkuu wa Chuo - Mama Mdogo - Katavi. Kanda za Kusini Oyee!!!!
Taarifa Mheshimiwa Mama Mdogo: Prof Lwoga hatoki Ruvuma bali Mkerewe
 
Nd. Philemoni Luhanjo ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Hilo lilikuwa ni tangazo la makamu mkuu wa chuo hicho.

Ni aibu kwa siasa za nchi hii na uongozi wetu kwa mtu kama huyu kuteuliwa nafasi bora kama hiyo bila kujali matukio ya utawala wake na upungufu wa uelewa au elimu yake.

Wafanyakazi wameomba waelezwe ni kwa nini wao SUA wapelekewe mtu mwenye sifa mbaya ya upungufu wa uadilifu. Mtu ambaye ametuhumiwa hata na Bunge kwa kuwasafisha mafisadi/wezi. Makamu mkuu huyo hakuwa na jibu.

Hali nyingine mbaya zaidi ni pale watumishi hao walipoomba kufahamishwa ni kwa nini uongozi mzima umekuwa ni wa kutoka kanda moja ya Kusini.

Makamu mkuu wa chuo -Sumbawanga
Naibu makamu mkuu wa chuo utawala –Iringa
Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma – Iringa
Mwenyekiti wa baraza (Luhanjo) –Iringa
Mwanasheria wa chuo –Iringa (mke wa makamu mkuu wa chuo taaluma).

Kuna walakini mwingine kwamba mtu huyu ni business partner wa makamu mkuu wa chuo utawala na fedha ambao kwa pamoja wanamiliki Hotel iitwayo ARC hapa Morogoro.

Kwa mtindo huu wa uteuzi wa kisiasa, taasisi za serikali zinakufa.

Kuna siku niliwahi kusema kuwa Tanzania tunaandamwa na udini na ukabila vimeanza kujipenyeza basi nilishushuliwa sana.Kila kitu kibaya sisi kazi yetu ni kukificha tu badala ya kukikemea.Kama Rais Kagame anavosema eti Rwanda hakuna mtusi wala mhutu siku hizi baada ya mauaji ya 1994 kwa hiyo anataka mnyarwanda yeyote ajiite Rwandese wakati ni uongo mtupu
 
Suala la kwamba anatoka Iringa sio issue. Kanda hiyo ndo imejaa wakulima na watunza misitu, hivyo si ajabu wanaotoka Iringa wakashika nafasi zaidi. Sema kwanini hakuna mtu hata mmoja anaetoka Kilimanjaro, Ruvuma au Mbeya? Ina maana wote huko hawana sifa? Japo mi sitoki maeneo hayo, nachelea kusema kwamba huo ni uoenevu.
 
Siasa hadi kwenye Academic!!! Luhanjo tena jamani! Hivi Tanzania watu wenye busara za kuongoza hakuna au nini tena. Huyu Mzee amefanya mambo ya ajabu katika kipindi chote alichokuwa Waziri kiongozi. Alikuwa in Godfather wa mafisadi kibao .... mostly visibly mimama ya wizara ya Afya na yule Bandido wa wizara ya Nishati... etc etc.... uvundo kila kona!
 
Nd. Philemoni Luhanjo ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Hilo lilikuwa ni tangazo la makamu mkuu wa chuo hicho.

Ni aibu kwa siasa za nchi hii na uongozi wetu kwa mtu kama huyu kuteuliwa nafasi bora kama hiyo bila kujali matukio ya utawala wake na upungufu wa uelewa au elimu yake.

Wafanyakazi wameomba waelezwe ni kwa nini wao SUA wapelekewe mtu mwenye sifa mbaya ya upungufu wa uadilifu. Mtu ambaye ametuhumiwa hata na Bunge kwa kuwasafisha mafisadi/wezi. Makamu mkuu huyo hakuwa na jibu.

Hali nyingine mbaya zaidi ni pale watumishi hao walipoomba kufahamishwa ni kwa nini uongozi mzima umekuwa ni wa kutoka kanda moja ya Kusini.

Makamu mkuu wa chuo -Sumbawanga
Naibu makamu mkuu wa chuo utawala –Iringa
Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma – Iringa
Mwenyekiti wa baraza (Luhanjo) –Iringa
Mwanasheria wa chuo –Iringa (mke wa makamu mkuu wa chuo taaluma).

Kuna walakini mwingine kwamba mtu huyu ni business partner wa makamu mkuu wa chuo utawala na fedha ambao kwa pamoja wanamiliki Hotel iitwayo ARC hapa Morogoro.

Kwa mtindo huu wa uteuzi wa kisiasa, taasisi za serikali zinakufa.
SUA ni chuo cha kilimo, na kilimo kimeshamiri zaidi kanda ya nyanda za juu kusini..Labda ndiyo sababu! [Tafadhali msinirukie, just thinking aloud]
 
Ingekua vp wote hao wangekua wakwere? Acheni ukabila mi mchaga lakin hata sisi wanatuongelea sana kwenye baadhi ya sekta someni na nyie mje mpate nafasi nzuri we degree umechukua juzi tu leo unataka uwe boss!? Kama kazi hamna siasa inalipa mbona
 
Suala la kuangalia hapo ni kuhusu mchakato wa hizo ajira zao ulikuwaje? Kama zilikuwa za upendeleo ndio tujadili lakini suala la kusema tu watoka sehemu moja halina mashiko, na isitoshe nadhani wana sifa za kutosha kwa hayo madaraka walio nayo. Pengine penye utata ni hapo kwenye uteuzi wa Chairman of the Council, kama hana uadilifu ni hoja ya kujadili lakini je upo udhibitisho?

Watanzania tusianze kujadili makabila yetu tujadili uwezo wa mtu, mbona taasisi nyingi tu zinaongozwa na watu toka sehemu moja na wanafanya kazi vizuri tu?

UNaweza ukakataa kujadili kabila la mtu na kujifanya kwamba hujali. Wanasiasa wamejifanya kujigamba eti hatuna udini, kumbe wanapokuwa pembeni, wanawapa moyo wenzao kwamba ongezeni nguvu. Haisaidii kujiita kipofu wakati unaona.

Hapo kuna walakini mkubwa sana.

Enzi hizi huwezi kufumbia macho jambo kama hili. Ukifanya hivyo unatoa mwanya wa kuongeza malalamiko. Hebu iangalie safu iliyopambwa kwenye mada. Bahati mbaya nyingine ni kwamba, m/kiti wa baraza aliyepita alikuwa balozi Kuhanga (songea). Msaidizi wake mama kamba (Mtwala).

Nini unachoona hapo? Au huoni chochote?
 
Suala la kwamba anatoka Iringa sio issue. Kanda hiyo ndo imejaa wakulima na watunza misitu, hivyo si ajabu wanaotoka Iringa wakashika nafasi zaidi. Sema kwanini hakuna mtu hata mmoja anaetoka Kilimanjaro, Ruvuma au Mbeya? Ina maana wote huko hawana sifa? Japo mi sitoki maeneo hayo, nachelea kusema kwamba huo ni uoenevu.

Nonsense completely (Quote; Idd Amin)
Yaani ukilima sana unakuwa afisa Kilimo na unakuwa kiongozi wa chuo cha Kilimo!!!!!
Huyu rafiki yangu Mchaga mbona ni afisa Uvuvi? Au basi Maafisa Madini wote wawe wasukuma wa Shinyanga eti kwa sababu wanachimba sana madini!??

NONSENSICAL argument!
 
MchunguZI ulitaka wajae Wachagga na Wasukuma?

Mchagga na nani?
Mi sijali kwa sababu hata kama Rais wa nchi atakuwa Kabila langu siamini kama nitapata faida binafsi.
Naamini hata wewe huna faida yoyote na wenzako wa Iringa kushika madaraka ila unadhani mumefanikiwa kumbe raha ni yao.

Kibaya hapa ni hiyo tunayoiona kama syndicate. Kama cartel ya kurushiana faida. Huyo Luhanjo ni lipi amelibakiza serikalini kiasi alirudie. Angalia huo ushirikiano wao wa kibiashara unavyohamishiwa Chuoni.

Chuo hiki nakihitaji kwa manufaa ya wajao siyo kwa ajili ya hawa wastaafu wanaolelewa eti wafe vizuri. Sisi tnataka kuishi vizuri.
 
Suala la kwamba anatoka Iringa sio issue. Kanda hiyo ndo imejaa wakulima na watunza misitu, hivyo si ajabu wanaotoka Iringa wakashika nafasi zaidi. Sema kwanini hakuna mtu hata mmoja anaetoka Kilimanjaro, Ruvuma au Mbeya? Ina maana wote huko hawana sifa? Japo mi sitoki maeneo hayo, nachelea kusema kwamba huo ni uoenevu.

hahahahahaha,,i pity you,,na waliojaa tiss na ikulu ni kwa sababu wanajua kutunza miti,,think critically,,
 
Back
Top Bottom