Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

sasa watalipwa mishahara bila kufanya kazi.?
Yaani corona imeleta kazi kweli kweli.


"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Wanastahili kulipwa ndiyo maana siyo wao walioileta Corona! Na pia siyo wao waliotoa tamko la kusitisha masomo kwa shule na vyuo vyote nchini. Sasa wasipolipwa hiyo mishahara, watakula nini?

Na wewe kama ni mfanyabiashara, unadhani utamuuzia nani hizo bidhaa zako? Iwapo wanunuzi wakuu (ambao ni hao wafanyakazi) hawalipwi mishahara kisa Corona!! Maana makundi yote kwenye jamii hutegemeana.
 
Haya mliyataka wenyewe. Elimu kayumba primary ni bure.

Unasomesha mtoto international, unampeleka China kusomea udaktari kisha anakuja kusubiri ajira za serikali za laki 8 mshahara kwa mwezi.
kuna mdogo wngu kapiga master china kuja bongo kapangiwa kazi mshahara 1.5m hayo makato sasa mbona na kazi yenyewe alikimbia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah wanafikiri watoto wao wanavyopanda school bus za njano kila siku tunafurahi?Afu inakuaje watoto wao wadogooo wa std 4 wanajua kiingereza kuliko watoto wetu wa form 3?

Wazazi wa Kayumba tunaumia mnooooooooooooooo.
Halafu watoto wao ni wanene na wengine wanavyo vitambi.
Na wamegoma kuwaita vibonge wanawaita big.
 
Hebu tunaangalie pande zote mbili ni kweli kwamba swala Elimu limesimama na hilo alina athali sana kwa wanafunzi kwasababu mfumo wa nchi lazima ubadilike ili kuwawekea mazingira mazuri wanafunzi.
Haya upande wa pili ambao wanaofanya biashara zote za elimu ni kweli wanapitia wakati mgumu mno hapa ni wamilimi wa biashara mfano shule , vyuo nk. Na wafanyakazi wa sekta binafsi za kielimu mfano walimu, wahadhili na wafanyakazi wengine.
Hapa nilipo kuna watu kadhaa wamepewa barua za kusimamisha mikataba bila kujali hali halisi ya muhusika
Kiukweli kwa upande wa pili sisi wazazi hali ni mbaya biashara hazitoki hamna wateja hivyo hata kodi za pango hamna sasa ada ya shule? ?

-Wito wangu serikali itoe kodi zote za sekta zilizoathiliwa sana na Corona mfano sekta ya elimu , utalii hapa naongelea sekta binafs
- Punguzo la asimia 50 % la ada Kwa kipindi cha likizo ili walau pande zote mbili zifaidike
-punguzo la mishahara kwa asilimia kidogo Kwa walimu kwa kufanya e-learning ili kuweza kuiendesha shule na walimu kufaidika
- ushirikiano baina ya shule na mzazi
 
Sasa, wewe unalipaje ada kipindi Kama hiki? Hili ni janga huwezi jua litaisha lini, naomba niseme hivi? Huwezi Chukua hela ya Muhula wa pili Wakati shule muhula wooote wa pili watoto watakuwa nyumbani, na bado hujui hali hiii itaisha lini!

Halafu msichanganye habari ya walimu kulipwa na swala la wanafunzi wanafunzi hawajawaajiri walimu no, Mwanafunzi ana mkataba Kati ya mwenye shule na yeye, na Mwalimu anamkataba Kati ya mwenye shule na yeye, hivyo kumbuka kuwa wenye shule wanafanya biashara na biashara ni pata potea kuna kufilisika, kutajirika na kwenda hasara na kumbuka hili ni janga linakula kwa kila pande, huwezi hangaika na Mwanafunzi ili kumlipa Mwalimu wako Wakati Mwanafunzi hajasoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada unayo hoja nzuri kabisa. Kimsingi haukatai kulipa ada kwa mwanao kama angekuwepo shuleni na anapata huduma ya masomo chakula usafiri nk...,Wanaosema ulipe hiyo ada saiv ni kwa ajili ya huduma gani? ..kwa sababu watotto saiv wako nyumbani wanaingia mwezi wa pili na kwa upepo unavyoendelea hawatarudi hata baada ya miezi miwili mitatu ijayo. So ikiendelea hali hii mpka mwaka kesho wazazi waendelee kulipa ada tu wakati watoto wapo nyumbani eti kwa hoja dhaifu kuwa shule inalipa mishahara walimu nk?
BIG NO.

Hapa labda ifanyike yafuatayo:
1.Wazazi na walimu wakubaliane kulipa percentage fulani ndogo ya sehemu ya ada(SIYO YA TERM NZIMA) kwa saiv kwa ajili ya kugharimia hizo online learnings, na iwe kwa makubaliano kwa pande zote mbili na siyo kwa kutishana kuwa asipolipa mzazi ada basi mtoto hatapewa promotions za kwenda next levels na vitisho vingine of the same. Kwanza hata wenyewe wenye shule hawana uhakika 100% kama mwaka huu utaenda salama kuruhusu wanafunzi waingie next levels as normal.

2.Wamiliki wa shule waishawishi serikali iwakingie kifua kwa mabenki isimamishe urejeshwaji wa mikopo angalau kwa miezi kadhaa ili akiba waliyo nayo iweze kugharimia some of fixed costs.

3.Serikali isimamishe kodi kwa wafanyakazi na wamiliki wa sekta binafsi kuwapunguzia ukali wa maisha
 
Mleta uzi ni mpumbavu sana

Shule za kata si zipo na ada ni elfu ishirini yaani bei ya bia 10 tu

Peleka mtoto huko shule ya kata

Unafahamu Capitalist economy wewe?

Tanzania uchumi hauodhiwi na serikali ndio maana kuna sekta binafsi upo?

Unajifanya tajiri kumbe maskini wa kutupwa, Peleka mtoto shule ya kata
mleta uzi ana hoja, issue sio kutoa Pesa, Issue ni kutoa pesa bila matumizi.
 
Haya mliyataka wenyewe. Elimu kayumba primary ni bure.

Unasomesha mtoto international, unampeleka China kusomea udaktari kisha anakuja kusubiri ajira za serikali za laki 8 mshahara kwa mwezi.

Shule za kayumba zinatosha kuchukua wanafunzi wote Tanzania?

Na mtoa mada hajalalamika ukubwa wa fees bali ni kulazimishwa kulipa fees yote wakati shule imefungwa.

Shule za bure zibaki kwa ambao hawana uwezo na wanaopenda kuwasomesha watoto wake huko. Hatuwezi kufanana kila mtu ana choice yake, na kulalamika ni sawa kama Jambo halipo sawa.

It's all about choice!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta uzi ni mpumbavu sana

Shule za kata si zipo na ada ni elfu ishirini yaani bei ya bia 10 tu

Peleka mtoto huko shule ya kata

Unafahamu Capitalist economy wewe?

Tanzania uchumi hauodhiwi na serikali ndio maana kuna sekta binafsi upo?

Unajifanya tajiri kumbe maskini wa kutupwa, Peleka mtoto shule ya kata
Some people bana loh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una kataa kulipa ada hao waalimu wana familia pia, wazazi, watoto nk wale nini? Tufikirie mara mbili juu kwenye kila jambo
Muwe mnaelewa. hajakataa kulipa ada..alichokataa kulipa ni ada yote full wakati mtoto haendi shule zaidi ya kutumiwa assignments. Ada ingepungua kulingana na situation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlete huku
Ye%20help%20my%20chest%20wan%20fall_joy_%20name%20of%20one%20skull%20for%20my%20area%20here%20...jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh Waziri wa Elimu na Serikali tunaomba muingilie kati hili linaloendelea katika hii shule ya Academic International School ya hapo Dsm kwani wanawalazimisha Wazazi kulipa Ada ya term nzima wakati huu ambao tupo kwenye janga la Corona, shule zote zimefungwa na haijulikani ni lini hali itarudi kuwa ya kawaida pale shule zitakapofunguliwa rasmi.

Ipo hivi, mara baada ya Serikali kuzifunga shule zote kutokana na janga la corona, shule hii kama zilivyo nyingine nyingi, imekuwa ikiwatumia wanafunzi wake assignments/maswali mbalimbali kupitia walimu wa masomo kama sehemu ya kuwa keep watoto busy hasa kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Hili ni jambo jema na Wazazi hawakatai kwamba kwenye hili kuna gharama za hapa na pale ambazo Shule na walimu wamekuwa wakiingia ili kulifanikisha hili la kuwasaidia watoto kipindi hiki wakiwa nyumbani. Lakini hili la kuwaambia Wazazi walipe ADA/TUITION FEES ya muhula mzima HALIKUBALIKI kwani watoto wapo nyumbani na hawapati zile class sessions za masomo yote kama wanapokuwa shuleni full time. Hakuna chochote kipya cha kwenye masomo ambacho wanakipata hivi sasa zaidi ya Walimu kuwatumia assignments/maswali ili kuwa keep busy kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Shule walau ingesema Wazazi wanapaswa kulipa kiasi fulani cha Ada/percent fulani ya Ada ili kusaidia hili ambalo linafanywa na walimu hivi sasa la kuwasaidia wanafunzi wakiwa nyumbani lakini sio kulipa Ada kamili.

Tunaomba sana Serikali kupitia Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako kulimulika hili.Vyombo vya kiuchunguzi vya serikali viliangalie hili linalofanywa na hii Academic Internationl School la kudai Ada kwa Wazazi wenye watoto kwani hii sio HAKI kabisa.

View attachment 1420400
View attachment 1420395View attachment 1420396
Mimi nimelipa ada ya miaka miwili mbele.

Wewe ya mwaka mmoja tu unalialia hapa wakati shule za Magufuli zipo
 
nimemuelewa mtoa mada na nimesoma coment mpka ya 30 ivii nilichokigundua kwa haraka haraka sana watanzania wengi hawana akili kichwani yani mazuzuzu na ndio maana hata nchi yetu haiendelei...
.
Yan kuna watu wanantetea kabisa kuwa ada iendelee kulipwa, mtoto anakaa nyumbani, aitomatically bajeti ya hom inaongezeka bado ulipe shulen ada ya bure tu maana haofanyi kazi yoyote mtt yupo nyumbn sijuh mpka lini. wengine wanasema shule inajiendesha sijuh wafanyakazi mishara labda tu chakiliza apo apo sisi wazazi biashara zetu hazija athiriw na corona??
.
fikiria adi nchi za ughaibuni zimepunguza masharti kwa nchi za africa means hili tatizo ni kote yan.
so haingii akili kabsa kulipa hela ambazo sawa na za bure basa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Serikali inatoa elimu bure, kwenda hizo shule binafsi ni kiherehere chenu, kwani serikali ndio imeleta corona ? Si mnachapa kazi? Mnataka serikali ifanye nini?"
Hayo si mawazo yangu lakini
 
Back
Top Bottom