Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

Wakati huu ndo wakati wa kujua huruma za waajiri hasa hasa kwenye shule za private.. Tutegemee walimu wa private kuwa affected zaidi na hii Hali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF wengi uchumi chini tu hzo ma Vogue husoma mtandaoni,ndo Mana badala ajibu hoja eti mrudishe mtoto shule za kata, I think wizara ije na Muongozo utumike nchi nzima ka watoto wamejikalia nyumbani kwanini utoe Ada nzima Bora ingekuwa kutoa kiasi flani, si ajabu hyo shule wanataka Hadi fees za school bus, Mara food huko sikuchekesha

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli pia nadhani hata walimu wa hizo shule hawapaswi kulipwa full salary kwa kuwa hawafanyi kazi kwa sasa. Sidhani hata kama wanaenda shuleni kila siku maana kwa walimu shule ikifungwa nao hawaendi shule kwa kuwa hamna wa kuwafundisha.

Huu ugonjwa una changamoto na zimeshaanza kuonekana katika baadhi ya sekta kama hiyo ya elimu ambapo vijana wamerudishwa nyumbani
 
Mkuu acha kulia lia hapa. Tatizo mnafanya mambo yaliyo juu ya uwezo wenu. We unaiomba wizara iingilie kati wakati huu mtaala wa uingereza!!! Ungemuomba waziri wa elimu wa uingereza ndio aingilie kati.... ... Pumbavu kabisa. Ndio ujifunze kula kwa urefu wa kamba sio kumuiga tembo anavyokunya..... Hizi shule ni kwa wanaojiweza..QUOTE="MENGELENI KWETU, post: 34999255, member: 178454"]
Mh Waziri wa Elimu na Serikali tunaomba muingilie kati hili linaloendelea katika hii shule ya Academic International School ya hapo Dsm kwani wanawalazimisha Wazazi kulipa Ada ya term nzima wakati huu ambao tupo kwenye janga la Corona, shule zote zimefungwa na haijulikani ni lini hali itarudi kuwa ya kawaida pale shule zitakapofunguliwa rasmi.

Ipo hivi, mara baada ya Serikali kuzifunga shule zote kutokana na janga la corona, shule hii kama zilivyo nyingine nyingi, imekuwa ikiwatumia wanafunzi wake assignments/maswali mbalimbali kupitia walimu wa masomo kama sehemu ya kuwa keep watoto busy hasa kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Hili ni jambo jema na Wazazi hawakatai kwamba kwenye hili kuna gharama za hapa na pale ambazo Shule na walimu wamekuwa wakiingia ili kulifanikisha hili la kuwasaidia watoto kipindi hiki wakiwa nyumbani. Lakini hili la kuwaambia Wazazi walipe ADA/TUITION FEES ya muhula mzima HALIKUBALIKI kwani watoto wapo nyumbani na hawapati zile class sessions za masomo yote kama wanapokuwa shuleni full time. Hakuna chochote kipya cha kwenye masomo ambacho wanakipata hivi sasa zaidi ya Walimu kuwatumia assignments/maswali ili kuwa keep busy kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Shule walau ingesema Wazazi wanapaswa kulipa kiasi fulani cha Ada/percent fulani ya Ada ili kusaidia hili ambalo linafanywa na walimu hivi sasa la kuwasaidia wanafunzi wakiwa nyumbani lakini sio kulipa Ada kamili.

Tunaomba sana Serikali kupitia Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako kulimulika hili.Vyombo vya kiuchunguzi vya serikali viliangalie hili linalofanywa na hii Academic Internationl School la kudai Ada kwa Wazazi wenye watoto kwani hii sio HAKI kabisa.

View attachment 1420400
View attachment 1420395View attachment 1420396
[/QUOTE]
 
Walipwe wamefanya kazi gani?
Nakuunga mkono.
Pesa za mafuta ya mabasi ya shule kila siku zinabaki kwao mana nauli Inalipwa kwa muhula mzima.
Pesa za Uji asubuhi,chakula cha mchana na jioni za kila siku kwa wanafunzi wote zinabaki kwao.

Pesa za umeme,maji na stationary zinabaki kwao mana watoto wapo nyumbani.

Hapa hawa wafanyabiashara wa Elimu wanachofanya ni kutaka kufanya pata potea wengine wanahisi huenda kuna wanafunzi wanaweza kuwa wahanga wa Corona ili wakilipa ibaki kwao tena.

Wanafunzi wapo nyumbani wanakula kwa wazazi na kufundishwa na wazazi mchana na usiku halafu wanaodai ada ni wengine.

Tena hao wamiliki ndio walipaswa warudishe ada za wale waliomaliza Ada ya muhula wakati hawajasoma hata nusu muhula .
Warudishe ada za watu mana watoto wao hawasomi wala kusafiri wala kula chakula cha shule.

Wakiendelea kusumbua basi tutadai ada zetu mana watoto wetu hawasomi.

Watulie tu shule zikifunguliwa wawakumbushe wazazi kumalizia ada za watoto wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CORONA HAIJAADHIRI WALIMU PEKEE NI IDARA ZOTE HUSUSAN SEKTA BINAFSI ZIMEADHIRIKA SANA, WENGI WAMEFUNGA BIASHARA HUSUSAN WANAOTEGEMEA USAFIRISHAJI (UTALII), UKISEMA LIPA ADA KWA SABABU SHULE ZIWEZ KUWALIPA WALIMU JE HUYO MZAZ AMBAE AMEFUKUZWA KAZI AU KUPEWA LIKIZO BILA MALIPO AU KULIPWA 30% YA SALARY KWA SABABU YA JANGA HILI, YEYE ANAHAKI YA KULIPA WALIMU TUU SIO KUJIANGALIA NA ADHARI UPANDE WAKE?. . KWA SABABU SERIKAL IMEFUMBA MACHO KWA WAJIRI WA SEKTA BINAFSI NA HUKU WAKITAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI, HAKUNA NJIA KUSITISHA AJIRA AU KUTOA LIKIZO BILA MALIPO KWA SABABU SHERIA ZA AJIRA HALIJAKUSIA NINI KIFANYWE HUSUSAN KTK JANGA KAMA HILI.
WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WATAMABUE JANGA HILI LIMEWATHIRI HATA WAZAZ PIA. SO HOME WORK HIZO SIO KIGEZO CHA MZAZ KULIPA FULL FEE, NI MAKUBALIANO KATI YA MZAZI NA SHULE, MUAJIRI NA WALIMU kWA SABABU HAKUNA SHERIA INAMLINDA MUAJIRI KTK JANGA KAMA HILI. HATA SHULE ZA NASARI WANAKUJA NA AGENDA HIZO HIZO KUDAI FULL FEES kwa sababu wazaz wanapewa homework on weekly bse.
WANAO KENUA MENO NI WALIMU NA WAFANYA KAZI WA SERIKAL WAO WANAENDELEA KULA MSHAHARA, TUENDELEE KUIBANA MBAVU SERIKAL LABDA INAWEZA SIKIA KILIO CHA WAAJIRI NA WAAJILIWA SEKTA BINAFSI... OTHEWISE TUENDELEE KUOMBA NA KUTUMIA MITISHAMBA .. MWAJIRI KUKOSA INCOME NDANI YA MIAZI MIWILI TAYAR UNASHINDWA KUWALIPA WAFANYA KAZI WAKO PIA INATAFSIR TOFAUT NYUMBA YA PAZIA.
 
Huko shule binafsi, na hasa utalii kilio kitakuwa Cha mda mrefu aiseee na hii corona jinsi tunavyo handle coz I saw news aljazeera kuhusu kupima mapapai na mbuzi pia, wakashtumu takwimu, so ili industry hasa ya Utalii isife na watu kupoteza ajira serikali isaidie ku boost hyo sector muhimu kwa uchumi wetu.

Back
Top Bottom