Hili pia litabuma!
Seif alitwambia kafika hadi UN,
Lisu yeye tukaambiwa kwa vile kahojiwa hard talk basi haki itakuwa mbaya sana.
Msichokijua ni kwamba, huko wanakotegemea watapata msaada wao wenyewe wapo hapa hapa nchini na wanaona kila kitu. Na wao wapo kwa faida siyo kwa ajili ya kina Lema.
Kiufupi hiki wanachofanya kina Lema watakuja kujiona wajinga sana baadae.
Yaani nashindwa hata nianzie wapi kuandika. Kitu ninacho weza sema ni kwamba serikali inatakiwa iangalie kwa makini sana vitendo vinavyo fanywa na wakenya dhidi yetu.
Mpaka sasa sijaelewa, wakenya wana nia gani na sisi au tuseme serikali ya Magufuli, maana naona mda wote wako mstari wa mbele sana kuwa-support wapinzani kwa kila uongo wanao upeleka kwao.
Tunajua mitandao yote ya kimataifa ambayo inarusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili ina brunches zao Nairobi Kenya, tukianza na; BBC, VOA, DW na Al Jazeera.
Wakenya kuwa na mitandao hii ya kimataifa nchini mwao wanaona ni opportunity kubwa sana kwao kuvitumia vyombo hivi kutuharibia sisi sifa ambayo tumejijengea kimataifa. Kibaya zaidi ni kumharibia Rais Magufuli nia yake ya kutuletea sisi watanzania maendeleo ya kweli.
Wakenya ambao wako kwenye level ya Establishment, kusema kweli, hivi sasa wanahaha kuona Rais Magufuli anavyo elekea kutuvusha sisi.
Vijana wengi nadhani hawatalijua hilo, kuwa toka Tanzania iingie kwenye mfumo wa kisoshalisti, wazungu walianza kuijenga Kenya ili iwe challenge kwetu katika vita ya ki-Ideology kama walivyo fanya kati ya nchi za Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mashariki wakati wa cold war.
Ningependa ifahamike kuwa kipindi kirefu, kwenye macho ya wabaya wetu, nchi yetu baada ya Mwalim Nyerere kuondoka, ilionekana kama ni nchi ambayo imelala na ambayo inazama taratibu, kwani tulionekana ka kwamba tumekwisha poteza nguvu na mwelekeo wa kuwa taifa lenye watu wenye msimamo wa kujitambua wenyewe, kitu ambacho kilikuwa ni furaha yao.
Lakini toka madaraka yachukuliwe na Rais Magufuli na kuona jinsi tunavyo piga hatua kuelekea kwenye maendeleo ya kweli, hofu kubwa imewajaa, maana wanaona kuwa sasa tumerudi tena kwenye jukwaa la mapambano. Kitu hiki wabaya wetu hawakifurahii na ndiyo maana mda wote wanajaribu kwa kila hali kutuharibia dreams zetu.
Wakenya na mabeberu wao wanao watuma wanajua kuwa sisi ni very strong kwa kila kitu na hawatuwezi. Hivyo hawatataka kuona kuwa sisi tuko zaidi yao. Wamejiaminisha wenyewe kwa kumda mrefu sana kudhani kuwa sisi ni primitive na tutabaki kuwa primitive. Shock kubwa imewajaa sasa kuona kuwa sisi tunaibuka tena.
Mambo mengi mabaya juu ya Rais wetu na nchi yetu ambayo tunayasikia kwenye ulimwengu wa wazungu msra nyingi huwa yanatolewa na kusambazwa na ndugu zetu wakenya, japo kuwa naweza sema, wakenya wa maisha ya kawaida wao hawako huko.
Walioko huko ni wakenya wanao shikilia nadaraka.
Haya yote ya akina Tundu Lissu na wengineo hayatokei bure, bali wakenya ndiyo supporter wao wakubwa. Huko nyuma nchi nyingi za Europe ziko ikiwemo Amerika pia na lengo lao ni kuzuia maendeleo ya waafrika. Hawataki kuona nchi yoyote ya Afrika inajitegemea yenyewe.
Naiomba serikali ya Magufuli kuwaangalia kwa makini sana wakenya ambao wako kwenye elite positions matendo yao. Hawana nia nzuri na sisi. Wao kwa vile wana excess kwenye hiyo mitandao ya kimataifa kwao, hivyo wamejipanga barabara kuitumia mitandao hiyo kutuangamiza sisi.
Hawa wapinzani wasinge kuwa na mbwembwe hizo nyingi kama wakenye wasinge wapa support kubwa hivyo. Conspiracies nyingi dhidi yetu zinapangwa Kenya na hii taasisi ya haki za binadam iliyopo Kenya. Hii taasisi ina kazi moja ya kutuchafua sisi. Matatizo yote ukiukwaji wa haki za binadam unaofanyika Kenya wao hawauoni kabisa, isipokuwa ule unao fanywa na serikali ya Magufuli tu.
Naviomba vyombo vya serikali yetu kuwa makini na kushirikiana na serikali ya Kenya kukusanya vithibitisho vya uhalifu vinavyo fanywa na hii taasisi ya haki za binadam Kenya dhidi yetu ili kama chochote kitatokea huko mbele tuweze toa kama ushahidi wa matendo yao maovu.
Rais Magufuli chonde chonse Rais wetu usikae kimya na ukiwaangalia wakenya wanatuua taratibu ki psycolijia. Fanya kitu Mzee kujilinda mwenyewe na nchi yako. Watanzania wanakutegemea na wanaimaninkubwa sana na wewe. Usituangushe.
Mimi kusema kweli sielewi kwa nini sisi watanzania tunawapendea wakenya, wakati wao miaka yote wamekuwa wakitufanyia mambo mabaya sisi. Nafikiri sasa wakati umefika wa kuwafanyia wao vitendo kama wao wanavyo tufanyia sisi.
Vitendo wanavyo fanya wakenya huo sio ujirani mwema hata kidogo!