Suala la baadhi ya viongozi wa kisiasa kutafuta hifadhi za ukimbizi ubalozini, mashirika ya wakimbizi ni "Cover Story"

Suala la baadhi ya viongozi wa kisiasa kutafuta hifadhi za ukimbizi ubalozini, mashirika ya wakimbizi ni "Cover Story"

Hili pia litabuma!

Seif alitwambia kafika hadi UN,
Lisu yeye tukaambiwa kwa vile kahojiwa hard talk basi haki itakuwa mbaya sana.

Msichokijua ni kwamba, huko wanakotegemea watapata msaada wao wenyewe wapo hapa hapa nchini na wanaona kila kitu. Na wao wapo kwa faida siyo kwa ajili ya kina Lema.

Kiufupi hiki wanachofanya kina Lema watakuja kujiona wajinga sana baadae.
Hivi Tundu Lissu alipopigwa risasi alikuwa hajawahi kutoa tahadhari kwamba maisha yake yapo hatarini?Hebu Acha kejeli kwenye mambo muhimu yanayohusu uhai wa watu au sababu wewe ni mnufaika wa huu utawala ndio maana unakoroma hapa?
 
Hili pia litabuma!

Seif alitwambia kafika hadi UN,
Lisu yeye tukaambiwa kwa vile kahojiwa hard talk basi haki itakuwa mbaya sana.

Msichokijua ni kwamba, huko wanakotegemea watapata msaada wao wenyewe wapo hapa hapa nchini na wanaona kila kitu. Na wao wapo kwa faida siyo kwa ajili ya kina Lema.

Kiufupi hiki wanachofanya kina Lema watakuja kujiona wajinga sana baadae.

Ila walionajisi uchaguzi watajiona wana akili sana? Kila kinachoendelea tunakiona kwa macho, na watu kukaa kimya sio kwamba wanaridhika na mambo, bali hofu ya maisha yao ndio inawafanya wakae kimya. Eti chaguzi zote za marudio toka awamu hii iingie madarakani ccm inashinda, huku kukifanyika ukatili, unyama, uhayawani na ukiukwaji mkubwa wa sheria. Uchaguzi wote wa SM umenajisiwa waziwazi. Uchaguzi huu wapinzani tu ndio wamekosea kujaza fomu, ila ccm wanapatia kila kitu!

Kwenye kampeni wapinzani tu ndio wamekiuka sheria, lakini CCM hakuna hata mmoja, kwenye uchaguzi matokeo hayaendani na idadi ya wapiga kura. Hata hayo mashirika unayosema yako kwa faida hawawezi kuona walakini? Hata mtu awe mjinga vipi lazima ataona huo walakini maana uko wazi mno.
 
Sasa ni muda mzuri kwa baadhi kuwa na akili timamu na kuwa wakweli.
Ndugu zanguni, hawa wanajifanya wanakinmbia Nchi ni waongo tu.
Lengo lao ni kutaka kuuaminisha Ulimwengu kwamba Tanzania si Nchi salama tena kwa kuishi.
Ebu jiulizeni, miaka 5 iliyopita wamekuwa wakitukana Viongozi wa Serikali lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.
Wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020, wamekuwa wakitukana matusi ya kila aina, lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.
Leo Uchaguzi umekwisha, mshindi kapatikana, kwa akili ndogo tu, utamtishaje mtu aliyeshindwa? Utamtisha wa nini?
Haya ni MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO.

Wameshindwa kwenye huo uchaguzi? Au unadhani hatujaona kilichofanyika kwenye uchaguzi huu? Dunia hii ya technology bado mnaamini mnayofanya yanaweza kufichika hivyo? Au kwakuwa watu wako kimya kuhofia maisha yao, ndio mnadhani hatujui nini kimefanyika?
 
Mbinu za kitoto, kuna huyu kasafiri kwa raha starehe salama salimini...Kafika Kenya anaomba atambulike Mkimbizi....Ndo mshatoswa ndg zetu wa saccos...muanze upya kuujenga upinzani kwa Ruzuku kiduchu
Unashangaa kwenda Kenya, watu kutoka Tz wapo USA,England, Nodic country Kama wakimbizi, ni wengi mno.
 
Watu tuko mtaani kimya kama vile hakuna kilichotokea ila tuna maumivu moyoni na tuna hofu na maisha yetu.
Kabla ya uchaguzi asubuhi moja nilikuta picha ya mgombea Wa ccm imewekwa kwenye offisi yangu,uchaguzi umeisha ila naogopa kulitoa .
 
Hao ni wakimbizi wa kiuchumi tu wanatafuta fursa
Wengine wanakimbia mkono wa Dola,baada ya njama zao kugundulika
Mtu kama lema au jacobo lazima watoke,Kwa sababu watu wao waliokuwa wanawatumia kupanga njama za kuvuruga Amani wamedakwa,na wameongea kila kitu
 
Ila walionajisi uchaguzi watajiona wana akili sana? Kila kinachoendelea tunakiona kwa macho, na watu kukaa kimya sio kwamba wanaridhika na mambo, bali hofu ya maisha yao ndio inawafanya wakae kimya. Eti chaguzi zote za marudio toka awamu hii iingie madarakani ccm inashinda, huku kukifanyika ukatili, unyama, uhayawani na ukiukwaji mkubwa wa sheria. Uchaguzi wote wa SM umenajisiwa waziwazi. Uchaguzi huu wapinzani tu ndio wamekosea kujaza fomu, ila ccm wanapatia kila kitu!

Kwenye kampeni wapinzani tu ndio wamekiuka sheria, lakini ccm hakuna hata mmoja, kwenye uchaguzi matokeo hayaendani na idadi ya wapiga kura. Hata hayo mashirika unayosema yako kwa faida hawawezi kuona walakini? Hata mtu awe mjinga vipi lazima ataona huo walakini maana uko wazi mno.
Tulikuonya kwamba ili kuepuka lalamiko kama hizi acheni kushiriki hizo chaguzi zao.
 
Ben Sanane angewahi huko, au Lissu 2017 wangewahi huko yasingewakuta.

Tangu lini serikali hii ikatambua kuwepo wa haki?

Hivi waliokuwa wakisema mitandao itarejeshwa tulipokuwa "some days back at 0001" bado wako humu humu JF na akili zao uchwara?
 
Sasa ni muda mzuri kwa baadhi kuwa na akili timamu na kuwa wakweli.
Ndugu zanguni, hawa wanajifanya wanakinmbia Nchi ni waongo tu.
Lengo lao ni kutaka kuuaminisha Ulimwengu kwamba Tanzania si Nchi salama tena kwa kuishi.
Ebu jiulizeni, miaka 5 iliyopita wamekuwa wakitukana Viongozi wa Serikali lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.
Wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020, wamekuwa wakitukana matusi ya kila aina, lakini hakuna aliyewatisha mpaka wakakimbia Nchi.
Leo Uchaguzi umekwisha, mshindi kapatikana, kwa akili ndogo tu, utamtishaje mtu aliyeshindwa? Utamtisha wa nini?
Haya ni MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO, MAIGIZO.
Acha propaganda za kihanith wewe inzi wa kijani!!!!!!!!!

Unasema ati ni MAIGIZO?Hivi Lissu amekaa miaka Mingapi ughaibuni baada ya jaribio la kumwua?

Leo hata baada ya Uchaguzi fake uliojaa vihoja via kuiba kura bado Viongozi wa vyama pinzani wanatafutwa na kutishiwa Wauawe!!!!

Lissu amekimbilia ubalozi wa Ujerumani! Godbless amekimbilia Narobi na kulikuwa na juhudi za kumrudusha Tanzania kwa lazima imebidi Jumuia za Kimataifa kuingilia Kati ndipo Lema akaachiwa!

Bado kina Mbowe, Zitto,Seifu, Mdee,Mbilinyi ,Wenje n.k. maisha yao yako mashakani.....
 
The facked land, no hope, no light, no justice and no promise. Ooooo a land of the died.
 
Hivi Tundu Lissu alipopigwa risasi alikuwa hajawahi kutoa tahadhari kwamba maisha yake yapo hatarini?Hebu Acha kejeli kwenye mambo muhimu yanayohusu uhai wa watu au sababu wewe ni mnufaika wa huu utawala ndio maana unakoroma hapa?
Lema atishiwe ana nini?
 
Alipambana huko Tundu lisu bali sisi huku tunasonga mbele, akataka wazuie misaada lakini wapi, tukapewa,
Akaona aje ajipime labda atafanikiwa bado amekwama na kukimbia tena ubarozi.

Roho ya shetani haitashinda kwa taifa hili.

Mtakimbia sana lakini uzee utawarudisha na muda utakuwa umeisha.

Tundu aliandaa maanadamano mkashangilia siku ilipo fika nyie wa kwanza kuwasha TV muone wapi wameanza.

Washabiki wote mnafungua TV kuangalia sasa nani angeingia barabarani wakati mko kwenye Tv?

Mimi nashauri waende tu ipo siku watawekewa magoti kwenye mashingo yao ndo watajua umbea ni tatizo kwa taifa lako.

Na kwa sababu yao wakidhani magu akitoka ili waje kuleta umbea tuna fanya kama china kwa maombi ya wengi picha liendelee.
 
Wakuu,
Limeibuka wimbi la baadhi ya viongozi wa kisiasa kukimbilia kwenye balozi zinazowakilisha nchi zao au mashirika ya ukimbizi kwa madai ya kuteswa (persecution). Kwa tafsiri ya jumla kwa kiingereza inaakisi yafuatayo: "...... is the act of harassing or oppressing a person or a group of people, especially because of their identity. Throughout history, people have faced persecution because of their religion, race, ethnicity, political beliefs, sexual orientation, and many other factors. ........ "

Hili suala lisichukuliwe juu juu kutokana na historia ya aina ya viongozi husika na malengo yao; hivyo kwa maoni yangu kama raia nashauri Serikali iwasiliane na taasisi ambazo zinawapokea wakimbizi hao kwa kuzingatia sheria za kimataifa, kidiplomasia, sheria za nchi na utamaduni kupitia wazee na viongozi wa kiroho ili kubaini sababu halisi kuliko hizi zinazotolewa na ufumbuzi utafutwe haraka iwezekanavyo kuepusha Taifa kuingizwa kwenye mfarakano wa kijamii, kiuchumi na kimahusiano na mataifa mengine.

Inatakiwa utafutwe ukweli ni akina wanawatishia hao viongozi wa kisiasa, kwanini na malengo ni yapi.

Sina uhakika kama Tanzania kuna hali ya hatari kisiasa endapo wahusika hawavunji sheria ambapo hata hivyo si kigezo cha kutishiwa. Serkali msifumbie macho kwa maana haba na haba hujaza kibaba mwishowe kunaweza kutengenezwa vikundi vya uasi na ugaidi na kuhatarisha wananchi wasio na hatia kwa sababu za wachache wanaotafuta kupata mamlaka ya utawala wa nchi kwa nia OVU.

[The great thinkers of this renowned transparent fora are solemnly appealed to thrive with constructive arguments to mend tthe ongoing animosity segragation which a few individuals are determined to plunge teh nation civil unrest without apparent and justifiable reasons to advance the longed ambitions at hooks and crooks.]

Nawasilisha
Usithubutu Kukutwa mkuu,We andika tu ila usiombe yakukukute.Amini nakuambia yaki kukuta utalia na kusaga meno na hakutakuwa na JF ya kuweko hii POST.Kwa taarifa yako hii uloandika hapa ndo cover story.Any way letsee.Mashujaa wataibuka
 
Hili pia litabuma!

Seif alitwambia kafika hadi UN,
Lisu yeye tukaambiwa kwa vile kahojiwa hard talk basi haki itakuwa mbaya sana.

Msichokijua ni kwamba, huko wanakotegemea watapata msaada wao wenyewe wapo hapa hapa nchini na wanaona kila kitu. Na wao wapo kwa faida siyo kwa ajili ya kina Lema.

Kiufupi hiki wanachofanya kina Lema watakuja kujiona wajinga sana baadae.
Yaani nashindwa hata nianzie wapi kuandika. Kitu ninacho weza sema ni kwamba serikali inatakiwa iangalie kwa makini sana vitendo vinavyo fanywa na wakenya dhidi yetu.

Mpaka sasa sijaelewa, wakenya wana nia gani na sisi au tuseme serikali ya Magufuli, maana naona mda wote wako mstari wa mbele sana kuwa-support wapinzani kwa kila uongo wanao upeleka kwao.

Tunajua mitandao yote ya kimataifa ambayo inarusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili ina brunches zao Nairobi Kenya, tukianza na; BBC, VOA, DW na Al Jazeera.

Wakenya kuwa na mitandao hii ya kimataifa nchini mwao wanaona ni opportunity kubwa sana kwao kuvitumia vyombo hivi kutuharibia sisi sifa ambayo tumejijengea kimataifa. Kibaya zaidi ni kumharibia Rais Magufuli nia yake ya kutuletea sisi watanzania maendeleo ya kweli.

Wakenya ambao wako kwenye level ya Establishment, kusema kweli, hivi sasa wanahaha kuona Rais Magufuli anavyo elekea kutuvusha sisi.

Vijana wengi nadhani hawatalijua hilo, kuwa toka Tanzania iingie kwenye mfumo wa kisoshalisti, wazungu walianza kuijenga Kenya ili iwe challenge kwetu katika vita ya ki-Ideology kama walivyo fanya kati ya nchi za Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mashariki wakati wa cold war.

Ningependa ifahamike kuwa kipindi kirefu, kwenye macho ya wabaya wetu, nchi yetu baada ya Mwalim Nyerere kuondoka, ilionekana kama ni nchi ambayo imelala na ambayo inazama taratibu, kwani tulionekana ka kwamba tumekwisha poteza nguvu na mwelekeo wa kuwa taifa lenye watu wenye msimamo wa kujitambua wenyewe, kitu ambacho kilikuwa ni furaha yao.

Lakini toka madaraka yachukuliwe na Rais Magufuli na kuona jinsi tunavyo piga hatua kuelekea kwenye maendeleo ya kweli, hofu kubwa imewajaa, maana wanaona kuwa sasa tumerudi tena kwenye jukwaa la mapambano. Kitu hiki wabaya wetu hawakifurahii na ndiyo maana mda wote wanajaribu kwa kila hali kutuharibia dreams zetu.

Wakenya na mabeberu wao wanao watuma wanajua kuwa sisi ni very strong kwa kila kitu na hawatuwezi. Hivyo hawatataka kuona kuwa sisi tuko zaidi yao. Wamejiaminisha wenyewe kwa kumda mrefu sana kudhani kuwa sisi ni primitive na tutabaki kuwa primitive. Shock kubwa imewajaa sasa kuona kuwa sisi tunaibuka tena.

Mambo mengi mabaya juu ya Rais wetu na nchi yetu ambayo tunayasikia kwenye ulimwengu wa wazungu msra nyingi huwa yanatolewa na kusambazwa na ndugu zetu wakenya, japo kuwa naweza sema, wakenya wa maisha ya kawaida wao hawako huko.
Walioko huko ni wakenya wanao shikilia nadaraka.

Haya yote ya akina Tundu Lissu na wengineo hayatokei bure, bali wakenya ndiyo supporter wao wakubwa. Huko nyuma nchi nyingi za Europe ziko ikiwemo Amerika pia na lengo lao ni kuzuia maendeleo ya waafrika. Hawataki kuona nchi yoyote ya Afrika inajitegemea yenyewe.

Naiomba serikali ya Magufuli kuwaangalia kwa makini sana wakenya ambao wako kwenye elite positions matendo yao. Hawana nia nzuri na sisi. Wao kwa vile wana excess kwenye hiyo mitandao ya kimataifa kwao, hivyo wamejipanga barabara kuitumia mitandao hiyo kutuangamiza sisi.

Hawa wapinzani wasinge kuwa na mbwembwe hizo nyingi kama wakenye wasinge wapa support kubwa hivyo. Conspiracies nyingi dhidi yetu zinapangwa Kenya na hii taasisi ya haki za binadam iliyopo Kenya. Hii taasisi ina kazi moja ya kutuchafua sisi. Matatizo yote ukiukwaji wa haki za binadam unaofanyika Kenya wao hawauoni kabisa, isipokuwa ule unao fanywa na serikali ya Magufuli tu.

Naviomba vyombo vya serikali yetu kuwa makini na kushirikiana na serikali ya Kenya kukusanya vithibitisho vya uhalifu vinavyo fanywa na hii taasisi ya haki za binadam Kenya dhidi yetu ili kama chochote kitatokea huko mbele tuweze toa kama ushahidi wa matendo yao maovu.

Rais Magufuli chonde chonse Rais wetu usikae kimya na ukiwaangalia wakenya wanatuua taratibu ki psycolijia. Fanya kitu Mzee kujilinda mwenyewe na nchi yako. Watanzania wanakutegemea na wanaimaninkubwa sana na wewe. Usituangushe.

Mimi kusema kweli sielewi kwa nini sisi watanzania tunawapendea wakenya, wakati wao miaka yote wamekuwa wakitufanyia mambo mabaya sisi. Nafikiri sasa wakati umefika wa kuwafanyia wao vitendo kama wao wanavyo tufanyia sisi.

Vitendo wanavyo fanya wakenya huo sio ujirani mwema hata kidogo!
 
Jiwe hana muda wa kuongea na yeyote, na hatishiki na hao called mabeberu...

Wapinzani wakitaka kuishi kwa raha wampigie magoti kumwomba msamaha na wamtambue kwamba ni Rais halali na waitangazie dunia kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki..
..

Haya ndiyo anayoyataka yeye!! Kuishi bila kuhoji Why and How...kwani kufanya hivyo ni kijipalia makaa mwenyewe... na ndiyo maana wapinzani targeted wameona wajisalimishe kuokoa roho zao..kufa kijinga nao ni ujinga pia.
Sasa wacha tuine mwisho wa hili game....
 
Back
Top Bottom