Suala la Bandari TEC hawakupata kama walivyozoea

Hapa ukisoma vzr mzee mudi anavaa kofia ya kuzuga anaelimisha juu ya historia ya Tanganyika lkn deep down anafanya harakati uchara za kidini...kupagawa udini ni jambo baya sana skiageni tu
 
Hapa ukisoma vzr mzee mudi anavaa kofia ya kuzuga anaelimisha juu ya historia ya Tanganyika lkn deep down anafanya harakati uchara za kidini...kupagawa udini ni jambo baya sana skiageni tu
Mpaji...
Fikra zako ni dhana tu.
Ikiwa una ushahidi uweke hapa.
 
History is written by the victors...............wazee wa uamsho mmechelewa saana japo mnajitahidi ku recover
 
History is written by the victors...............wazee wa uamsho mmechelewa saana japo mnajitahidi ku recover
Nab...
Usemi wa mdomo haumkatai bwana wake.

Mimi nimeiandika historia ya uhuru wa Tanganyika na tunaijadili hapa toka mwaka wa 2008.

Kitabu cha Abdul Sykes kinakwenda toleo la nne.

Kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni wala hakijulikani kilipoishia.
 
Nab...
Usemi wa mdomo haumkatai bwana wake.

Mimi nimeiandika historia ya uhuru wa Tanganyika na tunaijadili hapa toka mwaka wa 2008.

Kitabu cha Abdul Sykes kinakwenda toleo la nne.

Kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni wala hakijulikani kilipoishia.
sijasema kwamba ni uongo ila mambo yalivyo ni kama kulikua na pande zinashindana na mshindi ndo akaandika historia,,,,,hivyo ndo dunia ilivyo,,,,,,,,,,,.....historia unayotoa sio mbaya japo inaonyesha kuegemea upande wa dini/ ukanda fulani na hapo ndo shida inapokuja, uhuru wa Tanganyika ulianza kupiganiwa tokea enzi za wakina mkwawa na wazee wa majimaji huko
 
Naby...
Hapajapata kuwa na kushindana kuandika historia ya TANU.

Mtu wa kwanza kunyanyua kalamu kueleza historia ya African Association alikuwa Kleist Sykes.

Aliacha mswada uliokuja kuwa sehemu ya kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," mwaka wa 1973.

Kleist hakuandika kwa kuwa alikuwa mshindi.

Aliandika kueleza maisha ya baba yake na kikosi cha Wazulu kilivyofika Germany Ostafrika mwishoni mwa miaka ya 1800.

Historia hii haiegemei Uislam ila ndivyo ilivyokuwa kuwa wao ndiyo waliounda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Hivi ndivyo ilivyokuwa na waasisi wa vyama hivyo vyote viwili walikuwa Waislam akina Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Hawa wote walikuwa watu wa Dar-es-Salaam na huu ni ukweli huwezi kuukataa.

Mkwawa jina lake ni Abdallah na alisilimishwa na Abushiri bin Salim aliyekuwa adui mkubwa wa Wajerumani.

Majemadari wa Maji Maji walinyongwa na Wajerumani na kuzikwa kaburi la halaiki Songea.

Kiongozi wao jina lake Abdulrauf Songea Mbano.

Bahati mbaya ikiwa kuna watu wanataabika kwa kuandikwa historia hii kama ilivyostahili kuandikwa kwa kuwa Waislam wanaonekana mstari wa mbele.
 
Ndo maana nikasema mshindi ndie huandika historia,,,,,uzuri historia unayoleta inatufunulia mambo mengine kuhusu huu mfumo wa sasa, maana kwa hayo yote ila mwishoni waliokuja kuushika mfumo ni watu wengine ,basi kila mtu alikua anacheza karata zake natamani kujua ikawaje waasisi wakazidiwa kete wakati ndo walikua ma alwatan
 
Naby...
Haya si mambo ya kueleza shingo umetoa.

Unatakiwa mjadala wa taratibu usichochee jamii ikatazamana kwa uadui kwa yale yaliyopita zamani.

Jambo likishapita halidhuru.
Hapakuwa na kupimana nguvu.

Kuwa imekuwa hivi ni jambo la kusikitisha si jambo la kumkweza mmoja kuwa ni mjanja na mwingine ni mjinga.

Mtu haibiwi kwa kuwa ni mjinga.

Kuwa Abdul Sykes alijizuia kueleza historia yake alipokuwa hai si kwa kuwa alikuwa mjinga.

La hasha.
Uungwana ulimtaka afanye vile.
 
Bado palepale mshindi huandika historia......
 
Bado palepale mshindi huandika historia......
Naby...
Historia ya TANU ni hii nimeandika mimi kwa niaba ya wazee wangu.

Ikiwa wewe unashikilia historia ni hiyo ya Chuo Cha CCM Kivukoni mimi sikukatazi.

Historia ya Kivukoni iko Kivukoni na Maktaba ya CCM Dodoma.

Historia niliyoandika mimi iko katika Dictionary of African Biography (2011), Cambridge Journal of African History (1998), Library of Congress na kwingi vyuoni ulimwenguni.
 
Wewe mzee ni Mfano mbaya kwa wajukuu wako maana wakati watu wakipigana kujitoa katika ukoloni na utumwa wa kifikra lakini wewe unapigana kuuleta utumwa wa kifikra kisa tu dini naamini waarabu wakikufunga minyororo shingoni wewe na wajukuu zako utajiona wa maana kisa alokufunga ni vijukuu vya mtume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…