Suala la Bodaboda kuingia mjini kati; Wabunge wetu mnakosa viwango!

Suala la Bodaboda kuingia mjini kati; Wabunge wetu mnakosa viwango!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya wabunge wakiongozwa na Jerry Silaa kutaka bodaboda ziendelee kuwa kero jijini Dar es Salaam.

Suala hili limebebwa vile vile na Spika Tulia Ackson, kutetea baodaboda kuendelea kuwa kero katikati ya miji mingi nchini.

Siyo siri bodaboda ni kero kubwa, hawafuati sheria popote pale, si barabarani mijini wala vijijini.

Uliza wenye magari waliovunjiwa vioo-rear sight mirrors.
Waliokwaruzwa ubavuni.
Mishkaki ndo usiseme, kwenye traffic lights polisi walisha nyoosha mikono.

Wabunge wetu wanakosa viwango katika kutatua masuala ya mass transport.
Bodaboda haiwezi kuwa mbadala wa mass transport.

Tufikirie katika muelekeo huo, na wabunge wetu lazima kuwa critical thinkers, na si kuwa madalali wa kura kurudi bungeni tu.

Wengine wanaona bodaboda kama mtaji wa kisiasa.

Sasa katika ufinyu tu wa kufikiri, MACHINGA KWA NINI TULIWAONDOA?

Watanzania tunashindwa kuvumilia hii double standards.
 
Huu uzi ni taka taka kabisa, kila mtu yupo huru kutumia chombo Cha usafiri anachokimudu sehemu yoyote ile ya nchi bila kumzuia, kukataza boda boda kuingia katikati ya mji ni upumbavu wa kiwango Cha SGR, Kuna watu wanajiona sana kwa MBA nch ni ya kwao hii.
 
Lakini lazima kuwe na matumizi sahihi na siyo hovyo hovyo
 
Huu uzi ni taka taka kabisa, kila mtu yupo huru kutumia chombo Cha usafiri anachokimudu sehemu yoyote ile ya nchi bila kumzuia, kukataza boda boda kuingia katikati ya mji ni upumbavu wa kiwango Cha SGR, Kuna watu wanajiona sana kwa MBA nch ni ya kwao hii.
Ni takataka kwa msio na viwango.
Kesho mtaingiza mikokoteni mjini.
 
Suala la wao kutokufuata sheria hata wewe haufuati sheria.Suala la wao kuwa kero hata wewe ni kero.ILA NJE ya yote SERIKALI kushindwa kusimamia sheria kwa umakini kisiwe sababu ya kuleta ubaguzi dhidi ya kundi la watu kwa maslahi yao ya kisiasa.
 
Sisi boda boda tunaendelea kupiga kazi msitusumbue kama mnatuona ni kero acheni kutumia barabara
 
Sawa bodaboda zinatoa ajira kwa wengi, na wasiposinamiwa vizuri wanageuka kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Kwa mtazamo wangu nadhani hili ni jukumu la polisi wa usalama barabarani kuhakikisha hapawepo na makosa hayo, fine na adhabu nyingine ziwepo kwa ajili ya wale wasumbufu.

Makosa ya wachache yasitumiwe kama kigezo cha kuwaadhibu hata wale wastaarabu, wacha kila mmoja wao ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe.
 
... sheria ya mipango miji inasema kuhusu usafiri mijini? Kama haiwatambui bodaboda na bajaji waondolewe wala haihitaji mjadala; lau kama haiwatambui na kuna umuhimu wa wao kutoa huduma mijini sheria iboreshwe watambuliwe rasmi; that simple!

Vinginevyo, wanasiasa wataendelea kutumia mwanya huu wa kisheria kujikomba kwa hawa jamaa kwa maslahi binafsi na kuwaweka wasimamizi wa sheria kwenye sintofahamu. It is clear ni kwanini Jerry Silaa (Ukonga) alitoa hoja ile Bungeni; sio kwamba anawapenda sana bodaboda ila ana agenda yake behind.
 
Sawa bodaboda zinatoa ajira kwa wengi, na wasiposinamiwa vizuri wanageuka kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Kwa mtazamo wangu nadhani hili ni jukumu la polisi wa usalama barabarani kuhakikisha hapawepo na makosa hayo, fine na adhabu nyingine ziwepo kwa ajili ya wale wasumbufu.
... hawa jamaa wanazidi kuongezeka exponentially; sijui wataajiriwa askari wangapi kuwadhibiti. Angalia barabara kama ya Nyerere linganisha idadi ya askari wa barabarani na idadi ya bodaboda zinazokatiza per unit time; dah!

Ni sawa na msimu wa kumbikumbi wakianza kutoka kwenye mashimo yao; hata kunguru wajitahidi vipi kuwala hawawamalizi mwisho wa siku kunguru wanazidiwa.
 
Mkuu usipokuwa na viwango hata level of thinking inajionyesha.
Thinking yako ni poor , mnaacha kufikiria kwa Nini boda boda zinaongezeka ,unafikiria kuzizua boda boda , kwa taarifa yako graduate kibao tumejiajiri huku kwenye boda boda, mnataka mjitanue barabarani au walikwaruza gari yako utajiju.
 
Unadhihirisha tu mada yenyewe mkuu.
Hatuendi kwa maslahi binfsi, tunataka Tanzania ya next level, si ya machinga na bodaboda.
Huko ni kukosa viwango.
 
Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya wabunge wakiongozwa na Jerry Slaa kutaka bodaboda ziendelee kuwa kero jijini Dar es Salaam...
0.51835300 1626784048.png

Huyu dogo hana viwango kweli.
Next atatetea kupinga msimamo wa mama Samia kuondoa machinga Jijini.
 
... hawa jamaa wanazidi kuongezeka exponentially; sijui wataajiriwa askari wangapi kuwadhibiti. Angalia barabara kama ya Nyerere linganisha idadi ya askari wa barabarani na idadi ya bodaboda zinazokatiza per unit time; dah!

Ni sawa na msimu wa kumbikumbi wakianza kutoka kwenye mashimo yao; hata kunguru wajitahidi vipi kuwala hawawamalizi mwisho wa siku kunguru wanazidiwa.
Hilo nalo ni jukumu la jeshi la polisi kuhakikisha linaajiri askari wengi ili kuendana na mahitaji ya wakati.

Hata hivyo ukizunguka huko vituoni, utakuta wapo askari karibia wanne au watano wote wamekaa kaunta kupiga story za mipira.

So, kwanza hao wasio na kazi wapunguzwe kupelekwa kwenye mahitaji, kama hali ya mahitaji ikiwa bado haitoshi, waajiriwe wapya.
 
... hawa jamaa wanazidi kuongezeka exponentially; sijui wataajiriwa askari wangapi kuwadhibiti. Angalia barabara kama ya Nyerere linganisha idadi ya askari wa barabarani na idadi ya bodaboda zinazokatiza per unit time; dah!

Ni sawa na msimu wa kumbikumbi wakianza kutoka kwenye mashimo yao; hata kunguru wajitahidi vipi kuwala hawawamalizi mwisho wa siku kunguru wanazidiwa.
Kweli mtupu.
Huyu Jerry sijui ana akili gani.
 
Back
Top Bottom