KERO Responded Suala la chemba kutiririsha maji taka Mitaa ya Nyamwezi na Mhonda - Kariakoo, Mamlaka husika zinachukulia poa?

KERO Responded Suala la chemba kutiririsha maji taka Mitaa ya Nyamwezi na Mhonda - Kariakoo, Mamlaka husika zinachukulia poa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
289
Reaction score
415

Kipindi hiki cha mvua hali sio shwari kwenye baadhi ya Mitaa ya Kariakoo, Watu tupo hatarini kupata magonjwa kutokana na chemba kadhaa kutiririsha maji kwenye maeneo ya karibu na biashara zetu sambamba na kwenye njia ambazo watu tunapita, hali hii inaleta kero kubwa.

Mfano katika Mitaa ya Nyamwezi na Mhonda mlango kuingilia Soko Kuu (Shimoni) chemba zilianza kutiririsha mwishoni mwa Mwezi Machi 2025, kabla ya Sikukuu za Idd, kuna siku tuliyoa taarifa DAWASA wakaja wakaangalia miundombinu yao wakaondoka, tulijua wamekuja na suluhu lakini kero hiyo iliendelea kama kawaida, ambapo kwa sasa maafisa hao hawajarudi.

Huo ni mfano wa eneo hilo lakini kero hii imejitokeza kwenye maeneo mengi ya Kariakoo hali ambayo inasababisha Watu wengi kuchukia mazingira kutokana na kuwa na hofu ya kupata magonjwa kutokana na uchafu wa mazingira.

Licha ya chemba hizo, lakini pia hali ya mazingira ya usafi kwa jumla eneo la Kariakoo sio ya kuridhisha hata kidogo ikilinganishwa na hadhi ya eneo hilo maarufu.

Tukumbuke eneo la Kariakoo kutoka na uzito wake kiuchumi lilipewa hadhi ya kuwa Mkoa maalum wa kikodi, ambapo umekuwa ukiingiza fedha nyingi kwa manufaa ya Taifa letu.

Mfano kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ilitolewa katikati mwa Januari 2025, walikusanya Tsh. Bilioni 71.5 Sawa na 104% katika kipindi cha miezi sita cha mwaka mpya wa fedha 2024/25.

Mapato hayo ni kiashiria tosha ambacho kinaonesha wazi na kutuma ujumbe kwa mamlaka mbalimbali kuhusu kulipa umuhimu eneo hilo kwa manufaa ya kiuchumi. Mamlaka mbalimbali kutowajibika ipasavyo na kuliacha eneo hilo katika mazingira yanayoonekana kuzingurwa na kero inatuma ujumbe hasi.

Sanjari na hilo, karibia kila fremu Karikoo tumekuwa tukitozwa kiasi cha Tsh. 20,000/= kila Mwezi kwa ajili ya taka, lakini inashangaza mazingira mengi yamejaa taka na uchafu huku harufu mbaya ikiwa imetawala maeneo mengi.

Lakini pia asilimia kubwa ya wafanyabiashara tuliopo Karikoo tumekuwa tukilipia Ada ya Huduma (service Levy), ambayo kwa kiwango kikubwa tungetarajia kipaumbele kikubwa katika matumizi ya fedha hizo kikawe ni kuboresha miundombinu na mazingira yetu, lakini kwa sasa unakuta mitaro imejaa maji machafu yanatoa harufu, chemba zinatiririsha maji.

Unaweza kujiuliza ni kweli wahusika hawaoni umuhimu wa eneo hilo kuwa na miundombinu rafiki?

Kwa niaba ya wenzangu tunaomba kutoa wito kwa mamlaka husika hasa Dawasa, Halmashauri ya Jiji watimize wajibu wao kwa kuwajibika ipasavyo kuboresha miundombinu hasa ya maji taka, ili kuepusha kero na uchafuzi wa mazingira unaoweza kupelekea watu wengi kupata magonjwa.

Pia soma ~ Chemba iliyokuwa inatoa majitaka Kariakoo imezibwa baada ya kuripotiwa JF
 
President Trump : "My father always used to tell me...'Son, when you walk into a restaurant & you see a dirty front door, don’t go in. Because if the front door is dirty, the kitchen is dirty also.'...If our capital is dirty, our whole country is dirty."
 
Back
Top Bottom