Jana Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM ametoa ahadi nyingi za mambo ambayo Serikali yake itatekeleza katika kipindi cha siku 100 za mwanzo.
Moja kati ya mambo hayo ni kuhakikisha kuwa itaondoa utaratibu uliopo sasa wa kuzuia miili ya Marehemu ambayo haijalipiwa, kuchukuliwa na ndugu zao.
Kwamba Serikali itakuja na mpango ambao itaondoa utaratibu huo lakini pia kuhakikisha kuwa Ndg wa marehemu wanalipa gharama baada ya mwili wa marehemu kuchukuliwa.
Hata hivyo, Samia hakufafanua wazi mbinu watakazotumia kuhakikisha Ndg wa marehemu wanalipa gharama baada ya Ndg yao kutolewa hospitali, jambo ambalo pia limeacha maswali kwa wananchi pamoja na kwamba mpango huo ni mzuri.
Hali iliyopo Sasa ya hospitali kuzuia miili ya Marehemu ambao hawajalipiwa gharama imekuwa ni changamoto kubwa miongoni mwa jamii ya watanzania hususani maskini.
Mtu unakuta kauza raslimali zake Kijijini kumuuguza ndugu yake mpaka ikafika hatua anakosa cha kuuza. Pengine ugonjwa ni wa muda mrefu. Mwisho Mungu anamchukua. Ni mtihani mkubwa kwa ndugu wanaobaki. Wanakuwa na huzuni, simanzi mara mbili. Kufiwa, gharama walizotumia kumtibu, deni wanalodaiwa hospitali
Hili jambo ni kero kwa wananchi wengi maskini, ni jambo jema kama hao CCM ndio wameliona sasa kuwa ni kero na kulitumia kama moja ya mikakati ya kuomba kura.
Watakaoenda kutiki acha waende, na wanaosema sijui nini nao tuwaache na NRE yao maana kushiriki Uchaguzi ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura, lakini pia siyo lazima..