Suala la Ihefu: Mtu mkubwa Serikalini amewekwa mfukoni?

Suala la Ihefu: Mtu mkubwa Serikalini amewekwa mfukoni?

Suala eneo la Ihefu, chanzo cha mto mkuu wa Ruaha, limekuwa likilalamikiwa kwa miaka sasa.

Najua serikali imekuwa ikilishughulikia hili tatizo la kuingiliwa Ihefu kwa nyakati tofauti, lakini ni kama imekuwa funika kombe wanaharamu wapite.

Nashindwa kuelewa, inakuwaje mtu, watu wanachepusha mto mzimaa!!!
Na serikali hiyohiyo ipo.

Wafugaji wenye makundi ya ng'ombe 3,000 hadi 10,000 wameshidwa kudhibitiwa kwa miaka!

Kweli?

Serikali na vyombo vyake vyote imeshindwa kulitatua suala la Ihefu.

Sasa tunashituka Kidatu maji hakuna, Bwawa la Nyerere linatishia kuwa a white eleohant!
Hivi kuna uhujumu uchumi zaidi ya huu?

Cha kuchekesha kama si kufadhaisha, hivi inabidi Waandishi wa habari wateme ukweli kuwa kuna ka Gang of 12 walioikaba nchi wakati huu wa ukame?

Haingii akilini, lazima kuna mtu mkubwa kawekwa mfukoni!
Hili tatizo linaweza likawa na mizizi mikubwa zaidi ya tunavyofikiria
 
Wamerudi au walikuwepo? Nani aligusa hapo? Mwendazake au?

Tuendelee hivi hivi Kukosa umeme na kumlaumu January ili akili zikae sawa..

But Nina matumaini Kama Samia kaweza Kwa Masai hapa Ihefu Ni Jambo dogo tuu kwake.

..Dr.Ssh na Jm ndio waliokuwa na dhamana ya mazingira wakati wa Mwendazake.

..huenda alishawekwa mfukoni wakati akiwa makamu.
 
Wakati mwingine ukiona imelazimika waandishi kutumika kuibua uozo mkubwa kiasi hiki maana yake njia za kawaida imeshindikana! Maana yake hao watuhumiwa ni sawa na wale Mzee Pinda alisema wakiguswa nchi itatikisika.

Hii nchi kuna watu wametugharimu sana na kuunda mitandao inayotuvuruga mno! Kuna kazi nzito ya kufanya.
Inahitaji hii nchi tupate kiongozi mwenye roho kama Samwel Doe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Vp hao watu 12 bado tajwa tu [emoji1]

Issue itaishia kusema watu 12

Ova
 
Back
Top Bottom