Suala la Karim Mandonga: Vyombo vya habari vimechemka

Suala la Karim Mandonga: Vyombo vya habari vimechemka

Sisi mashabiki wa mandonga tupo nae hadi afie ulingoni, mandonga mtu kazi
 
I'lo jambo alifanya chumbani kwake

Hao watu wa media walimwona wapi
Hujaona promo za kwanza kabla ya kupigwa lile pambano la kwanza? Hakuna mwandishi anayekuja kukufanyia promo ya level ile bure unless ameona kuna fursa ya trafic sababu tayari ww unafuatiliwa na akikufatilia ni habari kwake. Mandonga alijipa thamani ndio waandishi wakaendeleza alipoishia.
 
Hujaona promo za kwanza kabla ya kupigwa lile pambano la kwanza? Hakuna mwandishi anayekuja kukufanyia promo ya level ile bure unless ameona kuna fursa ya trafic sababu tayari ww unafuatiliwa na akikufatilia ni habari kwake. Mandonga alijipa thamani ndio waandishi wakaendeleza alipoishia.
Mandonga ajielewe mambo ya kutumiwa na waandishi na kuachwa yapo sana hata ww mtu kama hana manuufaa kwako utaendelea hangaika nae
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kwani hawamlipi wanapompa hizo kazi kwa sasa? kama wanamlipa, palipobaki ni jukumu la Mandonga mwenyewe.
 
Popote mlipo, vyombo vya Habari na waandishi wote wa Habari nchini hamjatumia weledi katika kuripoti Habari ya Mandonga. Hamjatusaidia na wala hamjatupa elimu ya kutosha katika hili. Mmekuwa kama kasuku. Lakini ni kawaida yenu. Imefika hatua sasa, kila mtu anataka kuwa hodari wa kuelezea jinsi ya kufanikiwa katika maisha.

Hivi ni chombo gani cha Habari kimemwambia Mandonga ajifunze kujenga misingi ya maisha, na asitegemee hizi ngekewa ambazo nyingi ni za muda mfupi? Kwa nini hammwambii kuwa hayo makampuni yatamtumia na kisha yakiona haingizi pesa yatamwacha? Media za Kitanzania sijui ni lini mtabadilika. Ndio maana watu tulishajikita kuangalia BBC na media nyingine makini kwa sababu ya huu 'utopolo' wenu.

Ngoja niwape mifano.
Hakuna asiyejua kuwa mapeperi (makampuni) yanaweza kukutumia kwa faida zao. Na wakati huna manufaa kwao, watakupa kama gunia lililooza la viazi.
Wako wapi hawa?
1. Dr. Shika (Marehemu. Alitumiwa na kuachwa)
2. Pierre Liquid (haifai tena kwao)
3. Mzee Mpili (haifai tena kwao)
4. Karim Mandonga (ana manufaa kwao leo, lakini baadae atakuwa hafai).

Sasa, mbona hamsemi kuhusu ili? Mbona hamtaki kutufundisha tuwe na misingi imara ili tusijekutumiwa na kuachwa kama wengine?

Hakika vyombo vya Habari na waandishi wa Habari hamjawa sawa katika kutoa Habari hii.
Badilikeni basi. Nyie mna nguvu. Mmshauri Mandonga na wengine watakaofuata kuwa wajenge misingi ya maisha toka chini. Msiwe kama kasuku kila siku mnamsifia.
Suala la kujijenga kimaisha ni la kwake,hakuna kazi ya milele,hata urais una mwisho wake,walioajiriwa wanajua kuwa kuna siku watastaafu ndo maana wanakumbika kujenga na kusomesha watoto,sasa yy kam anasubiri kuna mtu aje amwambie huo umaarufu una mwisho hilo ni tatizo lake binafsi!!tukutane uzeeni!!
 
Mandonga ajielewe mambo ya kutumiwa na waandishi na kuachwa yapo sana hata ww mtu kama hana manuufaa kwako utaendelea hangaika nae
Waandishi wanatengeneza pesa ni kazi yake kuhakikisha kuna win win.
 
Kazi ya kubaki kileleni ni yake. Mandonga inabidi aitumie hii nafasi vizuri na abaki kileleni. Kwanza yule inaonekana ana kipaji cha ukomedi. Pia awe consistent kwenye ngumi. Ndo atabaki kwenye picha kwa muda mrefu.
by consistent, you mean aendelee kudundwa 😀 😀 😀 😀 ? Maana mpaka sasa hivi umaarufu wake umekuja kupitia mikwara mingi kabla ya pambano na kudundwa kwenye hilo pambano.
 
by consistent, you mean aendelee kudundwa 😀 😀 😀 😀 ? Maana mpaka sasa hivi umaarufu wake umekuja kupitia mikwara mingi kabla ya pambano na kudundwa kwenye hilo pambano.
Non kupigwa au kushinda ni matokeo. Wangapi wamepigwa na hawakutrend ?Jamaa alijiuzaa sana kwa mdomo kabla ya pambano.Huyu jamaa hata akishinda ataendelea kuwa habari ya mjini.
 
Jamaa akipata awekeze. Mfano akifungua mgahawa atumie promo mfano '' hapa mmeingia na maatumbo meupe kwenye mgahawa wa mandonga, hapa ni mtangula ndonga na michuzi mpaka mvimbiwe na kukaa''.
[emoji736][emoji736][emoji736]
 
Kwa umri alionao kama bado hajatambua hili hata vyombo vya habari vikimfunza hatosikia
 
Swala ni kwamba ukishapata nafasi ukawekwa kwenye mainstream unawezaje kuendelea kutumia hiyo fursa kufanya mambo yako yaende?,, unaweza kusimama mwenyewe na kuendelea kutumia fame uliyopata?…au unataka uendelee kubebwa!
 
Mimi niliamini Shabani Kaoneka kweli kayakanyaga hata gemu yao sikuangalia nilijua Mandonga ataua mtu kuamka asubuhi naambiwa yeye ndio kapigwa nilishangaa sana wacha apate hela kaifanyia kazi...maana kwanza sikujua kwamba lile pambano lao sio la utangulizi...
 
Shaban Kaoneka umeyakanyaga, muandalieni kaburi huyu, Mungu anakataza tusiuane lakini huyu nitamtoa roho.
 
Back
Top Bottom