Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k
Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.
Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.
Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo
1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.
2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.
Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.
3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.
4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.
Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.
Naomba kuwasilisha