Suala la Machinga, yafanyike haya

Suala la Machinga, yafanyike haya

Swala la Machinga ni swala gumu sana kulizungumzia kwa matakwa ya kidola, inaitaji Busara kubwa sana kuli-solve .

Serikali ikitaka kupambana na tatizo hili wafanye yafuatayo.
1.Ajira kwa vijana, watengeneze viwanda vidogovdogo vingi ili vijana wakafanye kazi.
2.Serikali itoe exposure kwenye kilimo kwa vijana . Ili hao vjana wakafanye shughuli za kilimo
Wakifanya haya mbona vijana watapungua mjini tyu.
 
Takataka ni kitu chochote ambacho kipo mahali kisipostahili kuwepo!

Kukosa ajira sio kibali cha kufanya biashara katikati ya barabara hadi watembea kwa miguu wanashindwa kupata maeneo ya kupita!

Kukosa ajira sio kibali cha kujenga vibanda hovyo bila mpangilio maalum hadi kwenye njia za magari au sehemu zilizohifadhiwa kwa shughuli maalum.

Ni lazima kuishi kwa utaratibu! Ambaye haishi kwa utaratibu ni mnyama tu asiye na akili!
Wewe ni kipapa maku ya mamako.
 
Sisi wanunuzi wa bidhaa zao tuna uwezo wa kuwafanya wafanye biashara kwenye maeneo maalum yaliyotengwa na njia rahisi ni kwasisi kuacha kununua bidhaa zao kwa wale wamachinga waliopanga bidhaa kwenye njia za waenda kwa miguu.

Tuhamasishane na ili likifanikiwa hao wamachinga watatii Sheria walizowekewa
 
Hivi machinfa complex viongozi wanashindwa kuirolea kauli yoyote maana ipo ipo tu...kuna muda nqjichekeaga mwenyew kama zombi
 
Rejea niliposema kwenye mada juu ya Tatizo la viongozi wetu kuwa wazembe, wavivu, kukosa commitment na exposure
Ishu ya wamachinga ilileta vuguvugu ambalo liliwatoa Marais katika nchi ya Algeria na Misri kama sikosei
a
 
Suala la wamachinga ni hatari kama watu wanavyoweza kutupia lawama mamlaka.za miji. Ukitaka kuamini nenda vijijini vijana woote wamehama wamejirundika mjini hata upange vipi haiwezekani miji imezidiwa
 
Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k

Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.

Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.

Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo

1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.

2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.

Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.

3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.

4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.

Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.

Naomba kuwasilisha
Ni vizuri kutafuta suluhisho la kufikirisha juu ya hili suala kubwa. Lakini ni muhimu sana kufahamu vizuri "machinga" ni nani hasa.

Kiuhalisia hawa "machinga" ni watu wanaotaka uhuru mkubwa sana wa kufanya biashara nje ya mifumo na taratibu zilizowekwa kisheria. Ni sekta isiyo rasmi kweli kweli. Wahusika wanataka waingie na kutoka katika biashara hiyo bila taratibu wala vibali rasmi, wafanye biashara popote panapopitika na wakati wowote bila udhibiti (kandokando ya barabara, katikati ya magari barbarani, katika njia za waenda kwa miguu, pembeni ya majengo, mbele ya maduka, nje ya masoko rasmi, n.k.). Wengi ni wahamaji hamaji (hawkers). Wanafuata penye wateja wengi kutegemeana na wakati wa siku. Wakizigundua hizo "hot spots", watajazana kama kama nzige hadi kumiminikia pasipostahili (barabarani, kwenye mifereji ya maji machafu na kuziba vituo vya mabasi na njia za waenda kwa miguu).

Sasa hii lugha ya kutafutiwa maeneo ya mazuri ya biashara kwa wamachinga haina maana. Hawawezi kuelewa wala kukubali. Hawako tayari kukalishwa sehemu moja muda mrefu huku wanasikia biashara imechanganya mahali kwingine. Na kwa vile wanaishi kwa kauli ya serikali iliyowaruhusu kufanya biashara bila kubughdhiwa na wameshaambiwa wao ni muhimu sana kama wapiga kura (fallacy), basi hawako tayari kuambiwa wasichotaka. Wako tayari kwa mapambano.
 
Hizi ni bla bla za midomoni tu.

Sheria za uzururaji zipo.

Kila mtu anataka kufanya biashara popote, utaongeaje na mtu huyo.

Hataki kujenga frame wala kulipa kodi, hayo mazungumzo yatakuwa vipi.

This is a mass migration from rural areas to towns /cities.

Chukua hao vijana wote peleka JKT walime na wazalishe, hata wakiwa laki tano.
Nimeona mama naye ameuma na kupuliza tu kiukweli hawa watu wanaoitwa machinga ni watu wabishi sana na kuiendelea kuwabembeleza ni kujienga majanga zaidi
 
Ni vizuri kutafuta suluhisho la kufikirisha juu ya hili suala kubwa. Lakini ni muhimu sana kufahamu vizuri "machinga" ni nani hasa.

Kiuhalisia hawa "machinga" ni watu wanaotaka uhuru mkubwa sana wa kufanya biashara nje ya mifumo na taratibu zilizowekwa kisheria. Ni sekta isiyo rasmi kweli kweli. Wahusika wanataka waingie na kutoka katika biashara hiyo bila taratibu wala vibali rasmi, wafanye biashara popote panapopitika na wakati wowote bila udhibiti (kandokando ya barabara, katikati ya magari barbarani, katika njia za waenda kwa miguu, pembeni ya majengo, mbele ya maduka, nje ya masoko rasmi, n.k.). Wengi ni wahamaji hamaji (hawkers). Wanafuata penye wateja wengi kutegemeana na wakati wa siku. Wakizigundua hizo "hot spots", watajazana kama kama nzige hadi kumiminikia pasipostahili (barabarani, kwenye mifereji ya maji machafu na kuziba vituo vya mabasi na njia za waenda kwa miguu).

Sasa hii lugha ya kutafutiwa maeneo ya mazuri ya biashara kwa wamachinga haina maana. Hawawezi kuelewa wala kukubali. Hawako tayari kukalishwa sehemu moja muda mrefu huku wanasikia biashara imechanganya mahali kwingine. Na kwa vile wanaishi kwa kauli ya serikali iliyowaruhusu kufanya biashara bila kubughdhiwa na wameshaambiwa wao ni muhimu sana kama wapiga kura (fallacy), basi hawako tayari kuambiwa wasichotaka. Wako tayari kwa mapambano.
Kama hawako tayari kuambiwa wasichotaka hapo maamuzi mengine yatafanyika. Maamuzi shirikishi ni jambo la muhimu Kwa sasa ili kuepuka migongano isiyo ya lazima!
 
Suala la wamachinga ni hatari kama watu wanavyoweza kutupia lawama mamlaka.za miji. Ukitaka kuamini nenda vijijini vijana woote wamehama wamejirundika mjini hata upange vipi haiwezekani miji imezidiwa
Hakuna jambo serikali ikiamua inashindwa. Ni kufanya maamuzi na kuyasimamia tu!
 
Nimeona mama naye ameuma na kupuliza tu kiukweli hawa watu wanaoitwa machinga ni watu wabishi sana na kuiendelea kuwabembeleza ni kujienga majanga zaidi
Hakuna cha ubishi! Ni serikali tu kufanya maamuzi ambayo ni shirikishi na kuyasimamia. Wewe hujawai kujiuliza kwa nini mwenge Kuna machinga ila Lugalo barabara nzima Haina machinga? Kama ni wabishi kwa nini hawafanyi ubishi wao eneo la Lugalo?
 
Back
Top Bottom