Suala la Machinga, yafanyike haya

Suala la Machinga, yafanyike haya

Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.

Magufuli alikuwa ni mpiga porojo na mpenda sifa za bei rahisi. Alikuwa anajua kabisa wamachinga ni washabiki wa cdm, namna pekee aliona ni bora awaruhusu wafanye biashara holela kama njia ya kuwafanya wasisupport cdm. Kama alikuwa sio mpiga porojo angawepeleka kwenye vile viwanda vyake 8,000+ alivyokuwa anaoongopea umma.
 
Mama D, uraia si kificho cha kufanya jambo lolote. La sivo unasema tutumie uraia wetu kufanya kila mtu anavotaka. Je majengo tujenge bila vibali? Si ni raia hawa hawa hata hubomolewa nyumba zao ili barabara, nguzo za umeme na mabomba ya maji yapite??

Wanaotaka mabadiliko kuhusu wanachinga wanataka mambo yadhibitiwe kabla hayajaharibika. Sasa hata majengo mazuri mijini, sehemu za wazi hakuna tena. Mabanda yenye plastic za blue yamejaa pembeni ya barabara na juu ya mitaro. Njia za wenda kwa miguu haziko tena wapita njia wanatumia barabara ya gari kutembea. Sehemu nyingine dereva hapati hata mita moja kutoka kwa mtu na meza yake hakafu maonyo kama “nigonge uone” yakitolewa. Mabanda ya vyakula kila sehemu huu ya mitaro ya maji yaliyosimama. Hali ni mbaya!

Kila jambo liwe na wakati wake na nafasi yake! Hiyo ndio sayansi, tuache emotions!! Tuwe na mpangilio.

Yote uliyoandika hapo yalielekezwa kwenye hiyo video kama hujaisikiliza isikilize sasa ndio uje uandike tena

Wamachinga ni raia, taratibu za kuwasimamia ziliwekwa ila watendaji wameamua kulala
 
Na huu ndo uwe mkakati wa serikali kwa kundi hili.

Iwe kuwafanya kuwa walipa kodi hadi walipa kodi wakubwa kabisa badala ya kuendelea kuwa wachuuzi wasiolipa kodi.

Serikali ikifanikiwa kuwaweka hawa watu kwenye maeneo rasmi, yaliyojengwa na kupangwa vizuri na wakawapanga vizuri, ni rahisi sana kuanza kuwatoza kodi!

Sio hili tu! Serikali ikiweka utaratibu wa vibali vya kufanya biashara kwenye maeneo fulani tena kwa miongozo na taratibu maalum ni chanzo kingine kizuri kabisa cha kodi na mapato
s
Ila si mbaya lina faida zake...
Wakipangwa watalipa kodi
Mapato yataongezeka vibaya mnoo tozo irudi shule
 
😂😂😂😂 kwani Bibi ana chuki na watu wa Chato😂😂😂,Mama hana akili,na huku mtaani hakubaliki kabisa,kwanza hakupigiwa kura
Kwani yule kiongozi muovu alipigiwa kura, au yeye alinajisi box la kura?
 
Yote uliyoandika hapo yalielekezwa kwenye hiyo video kama hujaisikiliza isikilize sasa ndio uje uandike tena

Wamachinga ni raia, taratibu za kuwasimamia ziliwekwa ila watendaji wameamua kulala
Mama D upo?
 
Kwa hio wana haki kuliko watu wanaolipa kodi?...
Machinga hawalipi kitu ila wanataka potential areas that other citizens pay millions for..

Wana haki kama raia, kama ni issue ya kulipa kodi kila hata kwenye salaried employees wapo ambao hawalipi, na wapo wanaolipa kidogo na wanaolipa kubwa pia

Mnatamani msilipe kodi kama wao wakati mnaishi na kumiliki mitaji tofauti kabisa na wao. Kama hutaki kulipa kodi sababu unashindana na mmachinga na wewe kuwa mmachinga ili upate hiyo raha
 
TRA na maofisa biashara wa Halmashauri wapitie upya aina za biashara zisizo za kimachinga alafu watoze kodi /leseni kama ambavyo wafanyavyo kwenye viduka vidogo mijini.

Tarura katika miji mikubwa wanayo mamlaka ya kukataza kufanya biashara kwenye kingo za barabara /waweke tozo kama wafanyavyo kwenye parking za magari. mfano wanaweza kutoa leseni za parking /uwazi wa eneo kwa wenye maduka /ofisi ili kuzuia machinga kupanga/kuweka huduma /bidhaa zao.

Maofisa afya/TFDA wanayo mamlaka ya kuzuia biashara holela za vyakula katika maeneo yasiyo rasmi, ubora na viwango.

Wakurugenzi wa halmashauri katika miji mikubwa kwa kushirikiana na watendaji walio chini yao hasa mipango miji wana wajibu wa kutenga maeneo au kubuni njia mbadala za Machinga kufanya shughuli zao. mfano maduka /vibanda vinavyo tembea au kuteua mtaa mmoja kwa ajili ya machinga.

Wakuu wa mikoa /wilaya wana wajibu wa kuratibu maeneo na aina ya biashara ili kuondoa mwingiliano wa bidhaa na huduma kurundikana sehemu moja.

Jeshi la zimamoto linao wajibu wa kutoa elimu juu ya majanga ya moto ambayo yanweza sababishwa na ujenzi holela wa vibanda vya machinga au kuzagaa kwa machinga karibu na maeneo yenye vituo vya mafuta mijini./miundombinu ya Umeme.

Tume ya Ushindani na wakala wa vipimo na TBS nao wana wajibu wa kusimamia /kutoa elimu ya namna ya kuboresha biashara ndogo ndogo ili zikuwe na kuondoa dhana ya Umachinga wa wajasiriamali wadogo wadogo.
 
TRA na maofisa biashara wa Halmashauri wapitie upya aina za biashara zisizo za kimachinga alafu watoze kodi /leseni kama ambavyo wafanyavyo kwenye viduka vidogo mijini.

Tarura katika miji mikubwa wanayo mamlaka ya kukataza kufanya biashara kwenye kingo za barabara /waweke tozo kama wafanyavyo kwenye parking za magari. mfano wanaweza kutoa leseni za parking /uwazi wa eneo kwa wenye maduka /ofisi ili kuzuia machinga kupanga/kuweka huduma /bidhaa zao.

Maofisa afya/TFDA wanayo mamlaka ya kuzuia biashara holela za vyakula katika maeneo yasiyo rasmi, ubora na viwango.

Wakurugenzi wa halmashauri katika miji mikubwa kwa kushirikiana na watendaji walio chini yao hasa mipango miji wana wajibu wa kutenga maeneo au kubuni njia mbadala za Machinga kufanya shughuli zao. mfano maduka /vibanda vinavyo tembea au kuteua mtaa mmoja kwa ajili ya machinga.

Wakuu wa mikoa /wilaya wana wajibu wa kuratibu maeneo na aina ya biashara ili kuondoa mwingiliano wa bidhaa na huduma kurundikana sehemu moja.

Jeshi la zimamoto linao wajibu wa kutoa elimu juu ya majanga ya moto ambayo yanweza sababishwa na ujenzi holela wa vibanda vya machinga au kuzagaa kwa machinga karibu na maeneo yenye vituo vya mafuta mijini.

Tume ya Ushindani na wakala wa vipimo na TBS nao wana wajibu wa kusimamia /kutoa elimu ya namna ya kuboresha biashara ndogo ndogo ili zikuwe na kuondoa dhana ya Umachinga wa wajasiriamali wadogo wadogo.
Mawazo mazuri sana!
 
Hangaya hana ubavu wa kuwatoa machinga. Hii thread nitawakumbusha
Watu wanatoa mawazo yao ili nchi iwe bora na Safi kwa wote wewe umekalia na chuki dhidi ya Rais.

Kunywa juice ya ndimu tu! Huyo ndo Rais wako hadi 2030
 
Na huu ndo uwe mkakati wa serikali kwa kundi hili.

Iwe kuwafanya kuwa walipa kodi hadi walipa kodi wakubwa kabisa badala ya kuendelea kuwa wachuuzi wasiolipa kodi.

Serikali ikifanikiwa kuwaweka hawa watu kwenye maeneo rasmi, yaliyojengwa na kupangwa vizuri na wakawapanga vizuri, ni rahisi sana kuanza kuwatoza kodi!

Sio hili tu! Serikali ikiweka utaratibu wa vibali vya kufanya biashara kwenye maeneo fulani tena kwa miongozo na taratibu maalum ni chanzo kingine kizuri kabisa cha kodi na mapato
s

Huu mkakati mnaoutamani utawafikisha mnakotaka

Mtakaposhindwa kuanika hata nguo kwenye kamba bila kuwa na ulinzi, mtakapokua mkiibiwa saidimiraz mkiwa kwenye foleni mabarabarani ndio mtaelewa

Wamachinga wawepo ila viongozi wa serikali katika kila eneo wahakikishe hizo njia za waenda kwa miguu zinabaki wazi.

Acheni kuwafitini binadamu wenzenu sababu ya uwezo wao mdogomdogo, hata wao wanatamani kuwa na mitaji mikubwa
 
Wana haki kama raia, kama ni issue ya kulipa kodi kila hata kwenye salaried employees wapo ambao hawalipi, na wapo wanaolipa kidogo na wanaolipa kubwa pia

Mnatamani msilipe kodi kama wao wakati mnaishi na kumiliki mitaji tofauti kabisa na wao. Kama hutaki kulipa kodi sababu unashindana na mmachinga na wewe kuwa mmachinga ili upate hiyo raha
Mi wala sitamani kutolipa kodi...cause i know ignorance of the law is not an excuse...bora ujielimishe na ufuate accordingly before people come and decide for you

ila i see the danger of baby sitting machingas
Lazima ifike mahala wajue nchi ina taratibu na wanatakiwa kuzifuata kama raia wengine

Na kwa kua wao ndo hawajui taratibu watapangwa tu

nafikiri Mama ameanza nao vizuri

Hapa ndo tutaona kama tuna wapanga miji smart nchi hii au la......

ila my dear huwajui machinga vizuri
Kuna watu si machinga ni wafanyabiashara wanaingiza mamilioni barabarani

am happy cz watapangwa watafuatiliwa na kodi sasa watailipa kisawa sawa...si wanataka maeneo potential?yana gharama zake
Ajira watapata ila
kwa Income tax watanyoooka
And i think ita better that way
 
Huu mkakati mnaoutamani utawafikisha mnakotaka

Mtakaposhindwa kuanika hata nguo kwenye kamba bila kuwa na ulinzi, mtakapokua mkiibiwa saidimiraz mkiwa kwenye foleni mabarabarani ndio mtaelewa

Wamachinga wawepo ila viongozi wa serikali katika kila eneo wahakikishe hizo njia za waenda kwa miguu zinabaki wazi.

Acheni kuwafitini binadamu wenzenu sababu ya uwezo wao mdogomdogo, hata wao wanatamani kuwa na mitaji mikubwa
Wote hatukatai machinga wasaidiwe mana ajira ni issue
Ila taratibu zifuatwe my dear

hata km wewe ungekua kiongozi leo haiwezekani..lazma wapangwe ama watolewe#Social control
 
Mi wala sitamani kutolipa kodi...cause i know ignorance of the law is not an excuse...bora ujielimishe na ufuate accordingly before people come and de

ila i see the danger of baby sitting machingas
Lazima ifike mahala wajue nchi ina taratibu na wanatakiwa kuzifuata kama raia wengine

Na kwa kua wao ndo hawajui taratibu watapangwa tu

nafikiri Mama ameanza nao vizuri

Hapa ndo tutaona kama tuna wapanga miji smart nchi hii au la......

ila my dear huwajui machinga vizuri
Kuna watu si machinga ni wafanyabiashara wanaingiza mamilioni barabarani

am happy cz watapangwa watafuatiliwa na kodi sasa watailipa kisawa sawa...si wanataka maeneo potential?yana gharama zake
Ajira watapata ila
kwa Income tax watanyoooka
And i think ita better that way

Utaratibu ndio unaotakiwa ila sio kuwachukia na kuwanyanyapaa wala kuwadharau

Hao wanaotakiwa kuwapanga na kuwasimamia nao wanakula mishahara bure, kazi zao hawafanyi halafu wanataka machingaz waonekane kero kumbe wenyewe ndio kero
 
Huu mkakati mnaoutamani utawafikisha mnakotaka

Mtakaposhindwa kuanika hata nguo kwenye kamba bila kuwa na ulinzi, mtakapokua mkiibiwa saidimiraz mkiwa kwenye foleni mabarabarani ndio mtaelewa

Wamachinga wawepo ila viongozi wa serikali katika kila eneo wahakikishe hizo njia za waenda kwa miguu zinabaki wazi.

Acheni kuwafitini binadamu wenzenu sababu ya uwezo wao mdogomdogo, hata wao wanatamani kuwa na mitaji mikubwa
Nani kasema wazuiwe kufanya biashara mama D ?
Mbona unaniangusha sana wakati najua una upeo mzuri tu wa ufahamu?

Kinachosemwa hapa ni kila mtu kufuata utaratibu na ikiwezekana kuwa katika mazingira ya kulipa kodi katika kipato anachojiingizia.

Sisi ni binadamu, tumeumbwa na tumepewa utashi wa kuishi Kwa taratibu! Haiwezekani kuwe na maisha bila utaratibu!

Tunajenga miji yetu kwa gharama kubwa sana , tunajenga barabara kwa gharama kubwa sana! Hatujengi ili tuviharibu na kuvichafua hata thamani yake isieleweke au kuonekana!

Jambo linalopendekezwa hapa linawasaidia hata wao sio tu kufanya biashara zao kwenye mazingira bora na salama Ila inawapa nafasi ya kukua kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa sababu wanapowekew miundombinu Bora, inawapa nafasi ya kutanuka kimawazo na hata kibiashara. Inawapa nafasi pia ya kufanya biashara katika mazingira mazuri yanayotunza hadhi yao Kama binadamu wengine na kuwapa heshima yao Kama binadamu wengine!
 
Nani kasema wazuiwe kufanya biashara mama D ?
Mbona unaniangusha sana wakati najua una upeo mzuri tu wa ufahamu?

Kinachosemwa hapa ni kila mtu kufuata utaratibu na ikiwezekana kuwa katika mazingira ya kulipa kodi katika kipato anachojiingizia.

Sisi ni binadamu, tumeumbwa na tumepewa utashi wa kuishi Kwa taratibu! Haiwezekani kuwe na maisha bila utaratibu!

Tunajenga miji yetu kwa gharama kubwa sana , tunajenga barabara kwa gharama kubwa sana! Hatujengi ili tuviharibu na kuvichafua hata thamani yake isieleweke au kuonekana!

Jambo linalopendekezwa hapa linawasaidia hata wao sio tu kufanya biashara zao kwenye mazingira bora na salama Ila inawapa nafasi ya kukua kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa sababu wanapowekew miundombinu Bora, inawapa nafasi ya kutanuka kimawazo na hata kibiashara. Inawapa nafasi pia ya kufanya biashara katika mazingira mazuri yanayotunza hadhi yao Kama binadamu wengine na kuwapa heshima yao Kama binadamu wengine!
Utaratibu ndio unaotakiwa ila sio kuwachukia na kuwanyanyapaa wala kuwadharau

Hao wanaotakiwa kuwapanga na kuwasimamia nao wanakula mishahara bure, kazi zao hawafanyi halafu wanataka machingaz waonekane kero kumbe wenyewe ndio kero

Tumeelewana kabisa Lord denning✍✍✍✍✍
 
Hizi ni bla bla za midomoni tu.

Sheria za uzururaji zipo.

Kila mtu anataka kufanya biashara popote, utaongeaje na mtu huyo.

Hataki kujenga frame wala kulipa kodi, hayo mazungumzo yatakuwa vipi.

This is a mass migration from rural areas to towns /cities.

Chukua hao vijana wote peleka JKT walime na wazalishe, hata wakiwa laki tano.
Nako huko kuwe na mfumo wa elimu kuwaendeleza hao vijana ambao hawakuendelea kielimu, pamoja na kuwafunza na kutekeleza kazi za uzalishaji. Umachinga wa kuuza bidhaa za china, bila kuwa ktk mfumo rasmi na kulipa kodi hauna tija kwa maendeleo ya taifa hili.
 
Back
Top Bottom