Suala la Machinga, yafanyike haya

Suala la Machinga, yafanyike haya

Sisi wanunuzi wa bidhaa zao tuna uwezo wa kuwafanya wafanye biashara kwenye maeneo maalum yaliyotengwa na njia rahisi ni kwasisi kuacha kununua bidhaa zao kwa wale wamachinga waliopanga bidhaa kwenye njia za waenda kwa miguu.

Tuhamasishane na ili likifanikiwa hao wamachinga watatii Sheria walizowekewa
Hilo haliwezekani
 
Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.
Angewapenda angewajengea chinga city jangwani na karume sio kuwaacha wauze vitunguu mpaka kwenye kuta za ikulu.
 
Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k

Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.

Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.

Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo

1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.

2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.

Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.

3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.

4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.

Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.

Naomba kuwasilisha
Wapo wataalamu wa town planners, na urban designers,watumieni wawape solutions, alafu Hili ni tatizo la councils ambapo madiwani na mameya wanahusika, RC na DC Hawana ubavu wa kusolve hii tatizo
 
Hizi ni bla bla za midomoni tu.

Sheria za uzururaji zipo.

Kila mtu anataka kufanya biashara popote, utaongeaje na mtu huyo.

Hataki kujenga frame wala kulipa kodi, hayo mazungumzo yatakuwa vipi.

This is a mass migration from rural areas to towns /cities.

Chukua hao vijana wote peleka JKT walime na wazalishe, hata wakiwa laki tano.
Wakitoka jkt unawapeleka wapi?
 
Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k

Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.

Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.

Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo

1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.

2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.

Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.

3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.

4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.

Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.

Naomba kuwasilisha
Mkuu nakuheshimu Sana unanikera unapoipongeza serikali, mambo ya kupongeza ni ya watu wajinga wasiojua majukumu ya serikali
 
Wapo wataalamu wa town planners, na urban designers,watumieni wawape solutions, alafu Hili ni tatizo la councils ambapo madiwani na mameya wanahusika, RC na DC Hawana ubavu wa kusolve hii tatizo
Hao town planners na urban designers unaowasema ndo hawa wanaoenda kupima viwanja vya makazi kwenye maeneo yenayopitiwa na mafuriko? Au wengine?
 
Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.
Machinga ni takataka waende wakalime huko,walikuwa misukule ya jpm kwa kuwachaji 20000 .that was a corruption
 
Ukiona hivyo basi kwenye hup ukuta wa ikilu wateja wapo,
Hali inatisha. Ukipita Posta maeneo ya chuo cha ifm kuelekea ikulu vimejaa vibanda kote! Alafu bora vingekuwa vimejengwa kwa mpangilio na standard moja inayofanana. Ni uchafu mtupu, watu wamejaza vibanda vilivyojengwa hovyo bila mpangilio na sasa vimefanya watu watembee barabarani yanapopita magari.

Miaka ya 90 na 2000 mwanzoni yake maeneo ndo tulikuwa tunaenda kupunga upepo na kutembea lure fresh Ila sasa hivi ni kero na uchafu mtupu
 
Mkuu nakuheshimu Sana unanikera unapoipongeza serikali, mambo ya kupongeza ni ya watu wajinga wasiojua majukumu ya serikali
Nashukuru Mkuu! Ila sio mbaya kupongeza pale watu wanapoanza kufanya vitu sahihi ambayo Kwa kipindi vimekuwa havifanyiki
 
Hali inatisha. Ukipita Posta maeneo ya chuo cha ifm kuelekea ikulu vimejaa vibanda kote! Alafu bora vingekuwa vimejengwa kwa mpangilio na standard moja inayofanana. Ni uchafu mtupu, watu wamejaza vibanda vilivyojengwa hovyo bila mpangilio na sasa vimefanya watu watembee barabarani yanapopita magari.

Miaka ya 90 na 2000 mwanzoni yake maeneo ndo tulikuwa tunaenda kupunga upepo na kutembea lure fresh Ila sasa hivi ni kero na uchafu mtupu
Miaka ya 90 ukimaliza chuo unapata ajira, udsm unasoma bure unapewa na chai ya maziwa na makate wenye blue band, sasa hivi hayapo wacha tu tupange nguo hadi ikulu,
 
Kwa nini hampangi nguo maeneo ya Lugalo? Kwa nini mkapange ikulu na mwenge?
 
JPM aliwapa jeuri ipi?

Unajua kwamba wamachinga nao ni raia wa nchi hii?

Kama hijui usiongee, JPM alitoa maelekezo sahihi kabisa hata SSH anajua

Yan mwendazake aliiharibu inchi kila machinga wametapakaa kama siafu.
 
JPM aliwapa jeuri ipi?

Unajua kwamba wamachinga nao ni raia wa nchi hii?

Kama hijui usiongee, JPM alitoa maelekezo sahihi kabisa hata SSH anajua

Mama D, uraia si kificho cha kufanya jambo lolote. La sivo unasema tutumie uraia wetu kufanya kila mtu anavotaka. Je majengo tujenge bila vibali? Si ni raia hawa hawa hata hubomolewa nyumba zao ili barabara, nguzo za umeme na mabomba ya maji yapite??

Wanaotaka mabadiliko kuhusu wanachinga wanataka mambo yadhibitiwe kabla hayajaharibika. Sasa hata majengo mazuri mijini, sehemu za wazi hakuna tena. Mabanda yenye plastic za blue yamejaa pembeni ya barabara na juu ya mitaro. Njia za wenda kwa miguu haziko tena wapita njia wanatumia barabara ya gari kutembea. Sehemu nyingine dereva hapati hata mita moja kutoka kwa mtu na meza yake hakafu maonyo kama “nigonge uone” yakitolewa. Mabanda ya vyakula kila sehemu huu ya mitaro ya maji yaliyosimama. Hali ni mbaya!

Kila jambo liwe na wakati wake na nafasi yake! Hiyo ndio sayansi, tuache emotions!! Tuwe na mpangilio.
 
Kwa hio wana haki kuliko watu wanaolipa kodi?...
Machinga hawalipi kitu ila wanataka potential areas that other citizens pay millions for..
 
Umesema vyema kabisa
Mama D, uraia si kificho cha kufanya jambo lolote. La sivo unasema tutumie uraia wetu kufanya kila mtu anavotaka. Je majengo tujenge bila vibali? Si ni raia hawa hawa hata hubomolewa nyumba zao ili barabara, nguzo za umeme na mabomba ya maji yapite??

Wanaotaka mabadiliko kuhusu wanachinga wanataka mambo yadhibitiwe kabla hayajaharibika. Sasa hata majengo mazuri mijini, sehemu za wazi hakuna tena. Mabanda yenye plastic za blue yamejaa pembeni ya barabara na juu ya mitaro. Njia za wenda kwa miguu haziko tena wapita njia wanatumia barabara ya gari kutembea. Sehemu nyingine dereva hapati hata mita moja kutoka kwa mtu na meza yake hakafu maonyo kama “nigonge uone” yakitolewa. Mabanda ya vyakula kila sehemu huu ya mitaro ya maji yaliyosimama. Hali ni mbaya!

Kila jambo liwe na wakati wake na nafasi yake! Hiyo ndio sayansi, tuache emotions!! Tuwe na mpangilio.
 
Ila si mbaya lina faida zake...
Wakipangwa watalipa kodi
Mapato yataongezeka vibaya mnoo tozo irudi shule
 
Back
Top Bottom