Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Ishu ya machinga ni ngumu kuitatua. Inatakiwa zitumike mbinu nyingi mchanganyiko ili kutatua hilo tatizo. Ila hata mimi sijui hata mbinu hata moja. Labda ngoja wengine waje kufikiria.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio poa kabisa kuwadhulumu watu haki yao ya kupata rizki.Umeongea kwa uchungu sana,wala Machinga Tanzania hata hapo kariakoo ni wastaarabu sana,watu wanajitafutia riziki wanaitwa uchafu
Wewe ni kipapa maku ya mamako.Takataka ni kitu chochote ambacho kipo mahali kisipostahili kuwepo!
Kukosa ajira sio kibali cha kufanya biashara katikati ya barabara hadi watembea kwa miguu wanashindwa kupata maeneo ya kupita!
Kukosa ajira sio kibali cha kujenga vibanda hovyo bila mpangilio maalum hadi kwenye njia za magari au sehemu zilizohifadhiwa kwa shughuli maalum.
Ni lazima kuishi kwa utaratibu! Ambaye haishi kwa utaratibu ni mnyama tu asiye na akili!
aIshu ya wamachinga ilileta vuguvugu ambalo liliwatoa Marais katika nchi ya Algeria na Misri kama sikosei
JPM aliwapa jeuri ipi?
Unajua kwamba wamachinga nao ni raia wa nchi hii?
Kama hijui usiongee, JPM alitoa maelekezo sahihi kabisa hata SSH anajua
Una mimba ya JPM? Mbna kila mda unamponda sana, hiyo mimba si uitoe tuJPM aliwapa jeuri sana..
Sasa mnavuna alichopanda hayati..
Ni vizuri kutafuta suluhisho la kufikirisha juu ya hili suala kubwa. Lakini ni muhimu sana kufahamu vizuri "machinga" ni nani hasa.Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k
Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.
Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.
Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo
1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.
2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.
Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.
3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.
4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.
Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.
Naomba kuwasilisha
Mhh ndugu unajuamini sana asee sio kwa comment kama hiiUna mimba ya JPM? Mbna kila mda unamponda sana, hiyo mimba si uitoe tu
Nimeona mama naye ameuma na kupuliza tu kiukweli hawa watu wanaoitwa machinga ni watu wabishi sana na kuiendelea kuwabembeleza ni kujienga majanga zaidiHizi ni bla bla za midomoni tu.
Sheria za uzururaji zipo.
Kila mtu anataka kufanya biashara popote, utaongeaje na mtu huyo.
Hataki kujenga frame wala kulipa kodi, hayo mazungumzo yatakuwa vipi.
This is a mass migration from rural areas to towns /cities.
Chukua hao vijana wote peleka JKT walime na wazalishe, hata wakiwa laki tano.
Hasira ya nini ww!!!??Una mimba ya JPM? Mbna kila mda unamponda sana, hiyo mimba si uitoe tu
Kama hawako tayari kuambiwa wasichotaka hapo maamuzi mengine yatafanyika. Maamuzi shirikishi ni jambo la muhimu Kwa sasa ili kuepuka migongano isiyo ya lazima!Ni vizuri kutafuta suluhisho la kufikirisha juu ya hili suala kubwa. Lakini ni muhimu sana kufahamu vizuri "machinga" ni nani hasa.
Kiuhalisia hawa "machinga" ni watu wanaotaka uhuru mkubwa sana wa kufanya biashara nje ya mifumo na taratibu zilizowekwa kisheria. Ni sekta isiyo rasmi kweli kweli. Wahusika wanataka waingie na kutoka katika biashara hiyo bila taratibu wala vibali rasmi, wafanye biashara popote panapopitika na wakati wowote bila udhibiti (kandokando ya barabara, katikati ya magari barbarani, katika njia za waenda kwa miguu, pembeni ya majengo, mbele ya maduka, nje ya masoko rasmi, n.k.). Wengi ni wahamaji hamaji (hawkers). Wanafuata penye wateja wengi kutegemeana na wakati wa siku. Wakizigundua hizo "hot spots", watajazana kama kama nzige hadi kumiminikia pasipostahili (barabarani, kwenye mifereji ya maji machafu na kuziba vituo vya mabasi na njia za waenda kwa miguu).
Sasa hii lugha ya kutafutiwa maeneo ya mazuri ya biashara kwa wamachinga haina maana. Hawawezi kuelewa wala kukubali. Hawako tayari kukalishwa sehemu moja muda mrefu huku wanasikia biashara imechanganya mahali kwingine. Na kwa vile wanaishi kwa kauli ya serikali iliyowaruhusu kufanya biashara bila kubughdhiwa na wameshaambiwa wao ni muhimu sana kama wapiga kura (fallacy), basi hawako tayari kuambiwa wasichotaka. Wako tayari kwa mapambano.
Hakuna jambo serikali ikiamua inashindwa. Ni kufanya maamuzi na kuyasimamia tu!Suala la wamachinga ni hatari kama watu wanavyoweza kutupia lawama mamlaka.za miji. Ukitaka kuamini nenda vijijini vijana woote wamehama wamejirundika mjini hata upange vipi haiwezekani miji imezidiwa
Hakuna cha ubishi! Ni serikali tu kufanya maamuzi ambayo ni shirikishi na kuyasimamia. Wewe hujawai kujiuliza kwa nini mwenge Kuna machinga ila Lugalo barabara nzima Haina machinga? Kama ni wabishi kwa nini hawafanyi ubishi wao eneo la Lugalo?Nimeona mama naye ameuma na kupuliza tu kiukweli hawa watu wanaoitwa machinga ni watu wabishi sana na kuiendelea kuwabembeleza ni kujienga majanga zaidi
Kweli mliohamia mijini na mbio za mwenge mnajinasibu.