Nakadori
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 8,778
- 21,010
Hata nguvu ya kusalimia sina.
Mji mzima kila mtu analalamika maji hakuna.
Hatuogi, hatufui, hatupiki....maji yamekuwa kama madini.....mtaani hayapatikani, na watu wa magari wanaosambaza hawauzi tank moja la lita 1000 ni kuanzia lita 3000 tena kwa 120000 hizo lita 3000.
Hivi kweli sisi wanyonge wa nchi hii tutaishije? Ni kweli tuna raisi na viongozi wengine wanaojua matatizo yetu au ni kwamba wao wakishakaa kwenye viyoyozi ofisini na kwenye ma vieiti basi wanasahau kwamba kuna watu wanataabika huku mtaani?
Serikali imekosa utatuzi wa hili tatizo kweli? Week zaidi ya 3 maji hakuna bombani? Hata kwa kukosea tu wameshindwa kutupatia maji?
Mbona maisha yamekuwa magumu sana?
Ninaandika kwa uchungu mwingi sana.