Suala la maji wanyonge hatuna pa kusemea

Suala la maji wanyonge hatuna pa kusemea

Hata nguvu ya kusalimia sina.....

Mji mzima kila mtu analalamika maji hakuna.....

Hatuogi, hatufui, hatupiki....maji yamekuwa kama madini.....mtaani hayapatikani, na watu wa magari wanaosambaza hawauzi tank moja la lita 1000 ni kuanzia lita 3000 tena kwa 120000 hizo lita 3000.

Hivi kweli sisi wanyonge wa nchi hii tutaishije? Ni kweli tuna raisi na viongozi wengine wanaojua matatizo yetu au ni kwamba wao wakishakaa kwenye viyoyozi ofisini na kwenye ma vieiti basi wanasahau kwamba kuna watu wanataabika huku mtaani?

Serikali imekosa utatuzi wa hili tatizo kweli? Week zaidi ya 3 maji hakuna bombani? Hata kwa kukosea tu wameshindwa kutupatia maji??

Mbona maisha yamekuwa magumu sana?

Ninaandika kwa uchungu mwingi sana.
Halafu mnajikuta wanaharakati! Kumbe pumba tu
 
Siyo Mji Mzima sema Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Ila kule Kigamboni,Temeke hata Ilala Maji yapo Watu walijitengenezea Mfumo binafsi usiokuwa unategemea serikali kwa maana Watu walichimba visima na Wakiobahatika kupata Maji yasiyo ya Chumvi walisambaza Kama wafanyavyo Dawasa .

Hivyo huwezi sikia kero ya Maji Ilala Temeke Wala Kigamboni na Kama ikitokea ni Mara chache Sana . Ebu fikiri Watu wa Mbagala walivyo Wengi vile lakini Wapo kimya au kule Gezaulole au kule Gongo la mboto. Kwa ufupi Manispaa ya Kinondoni na Ubungo ndizo hasa waathirika zaidi hivyo Ondoa neno Mji Mzima.
 
Endeleeni kuogopa kuandamana hadi itapifikia kilo ya mchele inauzwa elfu 10
 
ilala maeneo ya amana hakuna maji mwezi mzima yaani hata hatujui tupo dunia ipi?
 
Ndo maana kajiuliza wa magari wao wanapata maji ila sisi wa majumbani maji hakuna.... maajabu hayataisha tanzania hii

dawasa wanawauzia watu wa malori na mikokoteni wameshajua utamu wa pesa sasa mjiandae watakuwa wanakata maji ili wauze na maji hawafungui leo maana wanalamba asali
 
ilala maeneo ya amana hakuna maji mwezi mzima yaani hata hatujui tupo dunia ipi?
Milipuko ya kipindupindu dar itaanza...
Halafu kuna mjinga mmoja huko juu amedai eti ilala mna maji kwakuwa mnatumia ya visima....sijui alimaanisha ilala ipii
 
Najiuliza hivi serikali haiwezi kutengeneza bomba kutoka ziwa viktoria la kusambaza Maji sehemu ambazo Maji safi hakuna
 
Najiuliza hivi serikali haiwezi kutengeneza bomba kutoka ziwa viktoria la kusambaza Maji sehemu ambazo Maji safi hakuna
Maji yapo mengi sana bahari ya hindi mto msimbazi sema nyie watu wa dar mnadeka sana
 
Najiuliza hivi serikali haiwezi kutengeneza bomba kutoka ziwa viktoria la kusambaza Maji sehemu ambazo Maji safi hakuna
Kuna Mikoa kanda ya ziwa maji yake ni ya ziwa Victoria Ila napo hayatoki.

Hili suala mama Samia anapaswa aelezwe sio suala la ukame, Bali uzembe wizara ya maji
 
Jana kikao cha dharura kilikaa kikiongozwa na mkuu wa kaya......Mjadala ulikuwa ajali ya ndege.

Ukiangalia baada ya ile ajali ya ndege kesho yake mpaka jana nov 14 kulikuwa na ajali za barabarani mara watu 7, mara 3,mara 8 nk.... Uliona tamko?

Kufikia hapo ndo tujipime tupo na viongozi wa aina gani.... Garama za maisha zipo juu ..kila kitu kimepanda bei. Umeme mgao na maji ni tatizo sio huko ulipo tu. Tujipe pole
 
Back
Top Bottom