HOJA Suala la Mdundo wa Taifa limeishia wapi? Au Kamati ilitumia fedha za walipa Kodi bila kuleta matokeo?

HOJA Suala la Mdundo wa Taifa limeishia wapi? Au Kamati ilitumia fedha za walipa Kodi bila kuleta matokeo?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Hivi suala la Mdundo wa Taifa limeishia wapi? Au fedha za Watanzania zilitumika bure?

Kamati iliundwa, ikazunguka nchi nzima kukusanya sampuli na elements kutoka kwa kila kabila, juhudi zilizolenga kuunda Mdundo wa Taifa, utambulisho wa kipekee wa muziki wa Kitanzania. Lakini Je, huu ni mradi mwingine uliotumia fedha za umma bila kuleta matokeo? Wahusika mnapaswa kutoa taarifa, mdundo ule uko wapi? Na fedha zilitumikaje?


​
Julai 20, 2022, aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, aliteua Kamati maalum kwa ajili ya kuratibu Mdundo wenye asili ya Kitanzania. Kamati hiyo, iliyoongozwa na Dkt. Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji wa BASATA, na kujumuisha wajumbe akiwemo Mwana FA na P. Funky, ilianza kazi siku hiyo hiyo kisha kuzindua na kuukabidhi rasmi Februari 3, 2023, ambapo mpaka leo hakuna kinachoendelea.

Screenshot 2025-07-29 085756.png

Kamati hiyo ilikuwa na jukumu la kuzunguka Tanzania nzima kuchukua sampuli na elements kutoka kwa kila kabila, kisha baadaye kutengeneza Producer Kits zenye milio ya makabila, loops na vingine, kwa ajili ya kuwagawia watayarishaji wa muziki. Lakini kwa kweli, mimi sijasikia chochote kuhusu hilo.


Mtayarishaji Mkongwe wa Muziki Paul Mattysse (P. Funky) akizungumza kupitia Simulizi Na Sauti​
Soma zaidi: Kamati ya Mdundo wa Taifa yaanza kupokea maoni
 
Miaka miwili imeshapita teyari! No response. Kama Nyimbo zetu hazifiki Grammy tunaanza kuwalaumu waandaaji kwamba hawako fair. Kama tu swala la Kupata sampuli ya Mdundo wa Taifa linachukua 2+ years bila response yoyote ni kweli tunataka kufikisha Mziki wetu Duniani au we got some other objectives ? Mataifa ya Barani Afrika ambayo yamaeendelea kwenye Sanaa ya Muziki like Nigeria and South Africa tayari Wana Identify yao ya Aina ya Muziki ambao unafahamika World-wide. Hii ishu kwetu imekua Nightmare. Until today we don't know our style that is well known World-wide!
 
Back
Top Bottom