Suala la mishahara linakuzwa mno, tuzungumzie maslahi ya watumishi kwa ujumla

Suala la mishahara linakuzwa mno, tuzungumzie maslahi ya watumishi kwa ujumla

Mjadala na propoganda ya mishahara kwa watumishi wa umma inakuzwa mno na Wapinzani kama mtaji wao kwenye kampeni hizi bila kuzingatia hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano kuhusu uboreshaji wa maslahi kwa Watumishi wa Umma. Ieleweke kuwa mishahara ni sehemu tu ya maslahi katika utumishi wa umma.

Wapinzani wanasahau upandishwaji madaraja yanayoendana na mabadiliko ya mishahara, pia mabadiliko mapya ya posho mbalimbali zilizoongezeka, kupungua kwa Paye kutoka asilimia 11 hadi 9 na mengineyo mengi ambayo kimsingi yametumia fedha za umma na fedha za walipa kodi.

Tunapojadili mishahara tuzungumze kwa kujumuisha maslahi yote tutaeleweka tusibague manufaa mengine.
Umeandika kishabiki mno pasi kuangalia sheria ya ajira inasemaje! Hivi increments nayo ni hisani kwamba mpaka mtu aone amefurahije? Nn maana ya kitu kuwepo kwa mujibu wa sheria? Jema lipongezwe na la ugoro pia likemewe tusikae kupamba tu kama makondoo
 
Hoja hapa ni kwamba maslahi ya watumishi ni mapana ukiwemo mshahara ni vizuri kuangalia kwa kina hatua zilizochukuliwa na serikali ikiwemo posho na marupurupu mengineyo,mazingira ya kazi, pensheni, mikataba ya kazi na upandishwaji vyeo nk.

Tatizo watu wamechukua eneo moja tu la mshahara kwa sababu za kisiasa zaidi na kulishadidia.Hata hivyo nani kafanya utafiti wa kina kuhusu suala hili atupe matokeo tujadili kwa takwimu na taarifa za kisayansi.
wewe umetumwa kuandika usichokijua, kaa pembeni watumishi hawawezi kukuelewa kwa upupu uluoandika hapa.
 
Back
Top Bottom