Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Hatau tulipofikia Simba kwasasa timu inatakiwa iwe makini zaidi kwa kila eneo.
Kwa mfano Al Ahly huwa wanabadilika wanakua hatari na wabaya mno wanapofika nafasi kama ya robo na nusu fainali.
Washindi wa pili(runers)kwenye makundi hatua hii ya robo unakuta ndo washindi wa kwanza kuingia hatua ya makundi nusu fainali,hatua hii timu zinabadilika sana kwakweli.
 
Umesoma hizo screenshot, umesikiliza wachambuzi? Mbona wachambuzi wengi walikosoa. Sijajua mnatumia reference ipi. Redioni kuna wachambuzi waliomkosoa na khba wengine walimpa credit. Hata humu kuna wanaomkosoa na kuna wanaoona bado abastahili. Tatizo la wanaomkosoa kutaka kila mtu acheze ngoma wanayoitaka wao. Sisi sio nyumbu tuende sehemu moja. Kila mtu ana mtazamo tofauti latika kila jambo.
 
Wanasimba wakati tunajadili timu yetu embu tupeane taarifa,kombe la VPL pale Karume ofisi za TFF lipo salama?
Maana kuanzia jana baada ya mechi pale kwa Mkapa kumeibuka wimbi la vibaka!
View attachment 1749165
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kuna watu utakuta wanasema mara bora huyu kibonde.. mara oooh sijui yule kibonde, lakini hii hatua ni ngumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Ally Mayai na Amri Kiemba (wachambuzi waliocheza mpira) wanasemaje kuhusu Mugalu ?

Ngoja nikupe ya amri kiemba mkuu, Ally mayay aliongea hii kitu ya striker kuling na midfield na kumpa credit mugalu kwenye hilo. Ka kumshauli alifanyie kazi suala la scoring.
 
Kwahiyo Ikitokea umeulizwa kutoa maoni bila kuweka siasa (ambazo naona zimekukaa sana), juu ya eneo gani ambalo Simba inapaswa kulifanyia kazi Kati ya Safu ya mabeki,Kiungo na ile ya Ushambuliaji utagusia Safu ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio kwamba naleta siasa. Maoni yangu yameelemea rasilimali watu iliyopo sasahivi.

Ila kwa swali uliloniuliza, kwa maoni yangu ni kwamba Simba inatakiwa kufanya maboresho yafuatayo:-

Kutafuta mshambuliaji hatari mmoja ambaye uwezo wake uko juu ya Mugalu na Kagere (kama tutafanikiwa kumpata, maana watu hawa ni adimu mno barani Afrika, wengi wanakimbilia Ubelgiji, Ufaransa na Uturuki na nchi zingine za ''soft Europe'').
Tukimpata huyu, basi mmoja kati ya Meddie na Mugalu tumuache.

Je, Mtu huyu awe Dube ?
Kama tukimpata Dube, itakua safi, yeye ni striker wa kisasa (Kagere na nduguye mCongo ni old fashioned) ataisaidia sana kwa nafasi ambazo timu inatengeneza.
Ana footwork nzuri na ni goal attacker mzuri (Ni Haaland wa Kizimbabwe).
Ila ana changamoto ya majeraha, lakini pia hela atakayoitaja Mzee Bakhressa itakua ni balaa.

Sehemu nyingine ni kule upande wa Zimbwe, anahitaji msaidizi ambaye angalau anamkaribia ubora, Gadiel ameshuka sana kiwango. Siku Zimbwe akiumia na tuna mechi ngumu na kubwa itakua balaa.

Upande wa Kapombe Sina shida nako sana kwa sababu Nyoni, Ame na Duchu wote ''wanaweza wakacheza'' eneo hilo. (Japokua sio kwa ubora uleule).

Nafasi ya Mkude na Mzamiru bado Sijaona mchezaji wa ndani anayeweza kuwa bora zaidi ya hao. Na kuleta asiyemzawa maana yake tutatakiwa kumuacha mgeni mmoja kati ya wale kumi wa ligi ya ndani. Bado sijaona ni nani wa kuachwa so far.

Tukiweka pembeni ''siasa'', yangu ni hayo mkuu.
 
Alafu anamuongelea dube, hii ligi ya bongo ambayo mugalu anahitaji dkk 15 tu za mchezo ili ashinde goli. Kweli wanampima mugalu kwa VPL iwe repracement kwa ajili ya champions league.
 



Usipate shida mkuu, walisema hivi.
 
Tatizo raia wagumu kuelewa..Mugalu hastahili kuanza na Kagere ni bora kuliko Mugalu....Kagere muda wowote anakupa goli..angalia takwimu zake za vpl msimu huu, kacheza games chache kuliko washambuliaji wengi ila bado anakimbiza...Hii inshu ya kuwa simba ikicheza na Kagere inakuwa haitengenezi nafasi ni unazi na uongo wa kiwango cha SGR....Roho zinawasuta.

Kazi ya striker ni Kufunga..Kufunga na Kufunga..mengine mbwembwe..ni kama ilivyo kazi ya Goalkeeper ni kulinda lango mpira usiingie...Sasa unapomtetea mtu ambae hafanyi jukumu lake la kwanza effectively ni matumizi mabaya ya utetezi..

Hivi ingekuwa Manula anafungwa magoli ya kizembe (Kama vile ambavyo Mugalu anakosa magoli ya wazi), je bado Manula angeendelea kupangwa eti kisa tu ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma? 🤣🤣🤣🤣

Hebu kuweni serious..Mfumo wa guardiola unataka kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma..ila haujiulizi kwanii BRAVO anakaa benchi licha ya kuwa ni mzuri kwenye build up....Jibu ni rahisi, hafanyi vizuri kwenye jukumu lake mama ambalo ni kulinda goli ndio maana anakaa benchi na kapotea kabisa.

Sisi tunamshambulia Mugalu kwa kushindwa kuwa mfanisi kwenye jukumu lake la kwanza...hayo mambo ya kuwa anatengeneza nafasi nyingi sana kwa wenzie ni porojo maana hayana justifications...Ana assists ngapi?...kapiga penetration passes ngapi?...ana shots on target ngapi? au kasababisha rebounds ngapi?....


Tunapowaambia kuwa ubovu wa Mugalu unafichwa na performance ya timu muwe mnaelewa...Liverpool for the past two seasons walikuwa moto sana...Firmino alikuwa hafungi sana lakini bado hakuna shabiki wa liverpool aliyemnyooshea kidole...matokeo ya timu yaliwapa upofu...ila msimu huu mambo yamegeuka, timu ikaanza kusuasua na firmino hafungi ndipo hapo upofu wa mashabiki ukaisha wakaanza kumtaka Jotta achukue nafasi ya firmino.....ila mwanzoni ilikuwa mapambio kama yote mara firmino uwepo wake pale mbele ni faida kubwa isiyoonekana kwa macho ya kawaida na blah blah kama hizo.

Mara mia kidogo hata firmino alikuwa ana shots on target, ana assist na anawin battles kule mbele..sasa huyu Mugalu ndo kabisaa haeleweki anafanya nn kule mbele...ni kazi gani ambayo sisi hatuioni...basi sawa kocha anaiona..ila Time will tell na tutaufufua huu uzi.
 
Mkude kaloga hadi wachambuzi nikiona amepangwa nakuwa roho juu Mkude alikuwa yule wa miaka miwili iliyopita sio sasa
 
Acha kumfananisha Drogba na Mugalu. Drogba alikuwa hapotezi nafasi kipuuzi kama Mugalu. Drogba ilikuwa nafasi moja goli.
 
Simba watafute mshambuliaji aina ya Okwi ambaye ana uwezo wa kupangua beki na kufunga.
Usajili wa Simba umejikita kwenye viungo washambuliaji zaidi, msimu ukiisha tuongeze washambuliaji wachezaji kama Ajibu tuachane nao kwani tunao wenhi
 
Acha kumfananisha Drogba na Mugalu. Drogba alikuwa hapotezi nafasi kipuuzi kama Mugalu. Drogba ilikuwa nafasi moja goli.
Naongelea mifumo mkuu sijaongelea uwezo binafsi.

Naongelea majukumu yao uwanjani kama Namba tisa wenye jukumu la kuficha mipira na kuwachezesha shadow strikers.
 
Nonsense
 
Mi pia naungana na wewe,
Huenda kocha anamuandaa kwa matumizi ya baadae.
Mugalu siyo mzuri kivile lakini ukimweka kwenye mizani moja na kagere ni afadhali Mugalu Mara 100 ukilinganisha na kagere! Wote tulishuhudia alichokifanya kagere kwenye mechi na Al Ahyl!!
 
Mugalu siyo mzuri kivile lakini ukimweka kwenye mizani moja na kagere ni afadhali Mugalu Mara 100 ukilinganisha na kagere! Wote tulishuhudia alichokifanya kagere kwenye mechi na Al Ahyl!!
Kumbe angeanza Mugalu tungewafunga Al-Hilaly kama goli 3 hivi.
Na yote yangewekwa kambani na Mugalu.
Na tusingefungwa hata goli moja kwakuwa Mugalu anakabia juu.
 
Haya jana Kagere ameanza na nazani mmeona kilichotokea. Kuna watu utawasikia,
1. mara oooh kagere sio mzuri akicheza lonely striker...
2. mara ooh akianza kagere timu haitengenezi nafasi.....
3. mara ooh mtibwa sio kipimo kizuri.

sasa tumpime kagere kwa kipimo gani? ikiwa CCL Mugaru kapata play time ya kutosha tangu mtoano ila ana goal 2..Kapata play time ligi ya ndani ila bado anazidiwa goals na Kagere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…