Kwahiyo Ikitokea umeulizwa kutoa maoni bila kuweka siasa (ambazo naona zimekukaa sana), juu ya eneo gani ambalo Simba inapaswa kulifanyia kazi Kati ya Safu ya mabeki,Kiungo na ile ya Ushambuliaji utagusia Safu ipi?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu sio kwamba naleta siasa. Maoni yangu yameelemea rasilimali watu iliyopo sasahivi.
Ila kwa swali uliloniuliza, kwa maoni yangu ni kwamba Simba inatakiwa kufanya maboresho yafuatayo:-
Kutafuta mshambuliaji hatari mmoja ambaye uwezo wake uko juu ya Mugalu na Kagere (kama tutafanikiwa kumpata, maana watu hawa ni adimu mno barani Afrika, wengi wanakimbilia Ubelgiji, Ufaransa na Uturuki na nchi zingine za ''soft Europe'').
Tukimpata huyu, basi mmoja kati ya Meddie na Mugalu tumuache.
Je, Mtu huyu awe Dube ?
Kama tukimpata Dube, itakua safi, yeye ni striker wa kisasa (Kagere na nduguye mCongo ni old fashioned) ataisaidia sana kwa nafasi ambazo timu inatengeneza.
Ana footwork nzuri na ni goal attacker mzuri (Ni Haaland wa Kizimbabwe).
Ila ana changamoto ya majeraha, lakini pia hela atakayoitaja Mzee Bakhressa itakua ni balaa.
Sehemu nyingine ni kule upande wa Zimbwe, anahitaji msaidizi ambaye angalau anamkaribia ubora, Gadiel ameshuka sana kiwango. Siku Zimbwe akiumia na tuna mechi ngumu na kubwa itakua balaa.
Upande wa Kapombe Sina shida nako sana kwa sababu Nyoni, Ame na Duchu wote ''wanaweza wakacheza'' eneo hilo. (Japokua sio kwa ubora uleule).
Nafasi ya Mkude na Mzamiru bado Sijaona mchezaji wa ndani anayeweza kuwa bora zaidi ya hao. Na kuleta asiyemzawa maana yake tutatakiwa kumuacha mgeni mmoja kati ya wale kumi wa ligi ya ndani. Bado sijaona ni nani wa kuachwa so far.
Tukiweka pembeni ''siasa'', yangu ni hayo mkuu.