Smith Rowe
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 4,319
- 9,003
ball control na kumiliki mpira kuweza kusumbua mabeki ndio kinampa namba na sio uwezo wake wa kufunga au kukosa na simba haitegemei magoli yake sana bali kazi yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naelewa, na nakubaliana na yet kua mkude performance Ni NDOGO mno.sasa hapa huoni kama alikuwa na kiwango kidogo kuliko wenzake wote..au unatishwa na hizo namba 6.1 unaiona kubwa?...sasa wewe jiulize kwa ubovu ule wa mugalu pamoja na kukosa magoli mengi bado kamzidi Mkude...na angalia hata hapo katikati sehemu ambapo kazi kubwa ilifanyika, ni mkude tu ndio mwenye maksi ndogo kuliko wenzake....Tukija kwa wawa na onyango, rates zao zinaonekana ni ndogo kulinganisha na kapombe na zimbwe kwa sababu vita walikuwa wanapitia sana pembeni...Hata pale katikati walikutana na kazi ya kiume kutoka kwa Lwanga tofauti na mkude aliyekuwa flopy..
we hujiulizi kwann Lwanga ana 7.1 halafu Mkude ana 6.1?
Pass accuracy ya TADEO LWANGA ilkua NI 92.4%[emoji116]Tafadhali leta na Pass accuracy ya Lwanga kama ulivyoleta ya Mkude....halafu ndipo utaelewa ninachomaanisha.
hahahah na mtoa mada ndo mimi hapa ambae nashukuru umeelewa...sema poa mkuu,,, next time nita attach stats ili kuweka msisitizo kwenye hoja yangu...ila kwa wale walioangalia game hawakuhitaji hata statistics...pamoja mkuu.Naelewa, na nakubaliana na yet kua mkude performance Ni NDOGO mno.
Ila
Nlichokua nabishana na mtoa mada.
Ni suala la yeye kuja kuwadis wachambuz alafu Hana takwimu yoyote kusapoti.
Ndo maana nmemsaidia kumuwekea takwimu.
ANACHOLALAMIKIA MTOA MDA KINA MANTIKI KUBWA SANA.
Nnachoona MUGALU anaonyesha Sana poor performance tofauti na wenzie wanaocheza the same number.Kwa Mugalu sina neno ila kiufupi ni kwamba ni mwendawazimu pekee atakayeamin kuwa Mugalu ni Striker wa kutisha.
Kuhusu Mkude nakubali kabisa, jamaa alishapotea toka dakika ya kwanza mpaka ya mwisho, hakuwa mchezoni kabisa.
Mi game sjaangalia, ila Ni mfuatiliaji mzur wa takwimu.hahahah na mtoa mada ndo mimi hapa ambae nashukuru umeelewa...sema poa mkuu,,, next time nita attach stats ili kuweka msisitizo kwenye hoja yangu...ila kwa wale walioangalia game hawakuhitaji hata statistics...pamoja mkuu.
sasa hapa naamini utakuwa umezidi kunielewa vizuri zaidi..Pass accuracy ya TADEO LWANGA ilkua NI 92.4%[emoji116]View attachment 1746671
ila asilimia 90% ya niliowasikiliza au kuwasoma wanasapoti kuanzishwa kwake..wachambuzi wangapi umewasikiliza mkuu ,mbona kwa upande wangu ni wengi tu wamekosoa kuanzishwa kwake
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu..kwa busara na hekima uliyoitumia kuandika post yako...kwa akili kubwa ya soka uliyoitumia kutetea hoja yako...na kwa ubobevu wa soka ulioonekana kwenye comment yako....Haukustahili kumaliza kwa kuandika hiyo mistari miwili ya mwisho.Kazi ya striker ni kufunga magoli. Ni kweli kabisa. Lakini hii kauli ni kauli ambayo ingefaa kutumika kwa mtu mwenye traditional approach katika mpira. Yani mtu mwenye mtizamo ya kizamani kuhusu mfumo wa soka.
Kwasasa tupo katika zama za mpira ambazo wameibuka ma technicians wengi waliobadilisha kabisa approach ya soka mfano tukianzia na Frank Riijkard, Pep Guardiola, Jurgen Klopp na wengineo wengi tu.
Mifuno au style za uchezaji wa team za hawa makocha ni tofauti kabisa na zile ambazo zinategemea target man kama striker awe ndio main source ya kufunga magoli katika team.
Ndio maana hii mifumo ya kisasa utakuja kugundua mipira mirefu hutumika mara chache sana. Style hizi za kisasa za mpira zinahitaji ku build up play kuanzia nyuma na wachezaji ku interchage position na pass kwa haraka kuelekea goli la mpinzani au ku retain possesion wakati wakitafuta njia ya kuipita defense ya upinzani.
Hii ndio sababu katika team za namna hii utakuta hata distribution ya magoli kwenye team ni kubwa tofauti na mifumo ya kizamani ambayo unakuta kwenye team striker ndio amefunga magoli zaidi ya 80% kwenye team.
Ndio maana siku hizi si ajabu kukuta wachezaji wa nafasi za kiungo (play makers) wakiwa na magoli mengi kuliko hata (goal getters).
Kwahiyo mkuu mimi nadhani Mugalu pamoja na kuwa anakosa sana nafasi za kufunga lakini ana umuhimu sana kwenye team kama alivyo Kagere.
Mwisho wa siku ni kuwa team glory ndio muhimu kuliko personal glory. Nikimaanisha team kupata matokeo ndio kitu cha msingi zaidi kuliko kuangalia nani amefunga magoli.
Angalia pale Liverpool mtu kama Bobby Firmino yeye ndio striker lakini hafikii hata 1/3 ya magoli ya Mo Salah ambae ni winger. Lakini kocha anampanga kila siku kwakuwa anajua katika mfumo wake Bobby anafanya majukumu yake kama inavyotakiwa na ndio maana Salah au Mane wanafunga. (Huo ni mfano mmoja kuna mifano mingi kwenye team nyingi).
So mkuu sikubaliani na wewe. Na pia chakujiuliza wewe pia ni kuwa je wewe unajua sana mpira au ukocha kumshinda Da Rosa?
MUGALU Hana ball control kabisa,ball control na kumiliki mpira kuweza kusumbua mabeki ndio kinampa namba na sio uwezo wake wa kufunga au kukosa na simba haitegemei magoli yake sana bali kazi yake
Kuhusu Mkude wachambuzi wetu wanaturudisha enzi zile mipira haionyweshi live, Mkude anashindwa kutoa hata pasi, uchezeahaji wake ni aina moja pasi ndefu za pembeniMimi ni shabiki wa mpira na mpira ninaujua kwa kuutazama na kuucheza uwanjani. Haiitaji elimu kubwa kugundua kuwa Chris Mugalu hafai na hastahili kuanza kikosi cha kwanza kulingana na kiwango chake hasa uwezo wake wa kufunga. Bahati nzuri kwake ni kuwa udhaifu wake unafichwa na ubora wa timu.
Na kwa bahati mbaya zaidi wachambuzi wengi wa soka hapa bongo wamekuwa na 'upofu' katika uchambuzi. Analysis zao nyingi zina base kwenye matokeo. Mfano, hata kama timu ikicheza ovyo kwa dk zote 89, ila ikapata goli na kushinda dakika ya 90..Basi tegemea analyis positive kutoka kwa wachambuzi wetu.. Vice versa is true.
Vivyo hivyo kwenye swala la mugalu, wachambuzi wetu hawajui chochote kuhusu soka. Hata uchambuzi wao juu ya viwango vya wachezaji umemezwa na matokeo ya timu. Wengi utawasikia kuwa Mugalu ni striker mwenye uwezo wa kuhold mpira na kufungua nafasi kwa wengine. Hawazungumzii kabisa ubutu wake golini. Na mbaya zaidi wachambuzi karibu wote wana copy na kupaste opinions zao zinafanana. Katika kipindi hiki, huwezi kuta wachambuzi wanajadili weaknesses za Mugalu, badala yake wanaelezea umuhimu wake na faida yake kule mbele.Najiuliza, Hivi kama hafungi, ana umuhimu gani sasa wa kuanza?, na je kama timu isingekuwa inapata matokeo na bado Mugalu angekuwa anapoteza zile nafasi, bado wasingemuelezea udhaifu wake?...Jibu ni rahisi tu, wana chambua kulingana na matokeo.
Mfano wa pili, ni Jonas Mkude. Kwa mtu anaejua mpira na aliyeangalia ile game, ilikuwa sio rahisi kuamini kama Mkude angerudi uwanjani second half..Alikuwa flopy sana siku ile.
Cha ajabu timu imepata matokeo kwenye comments unasikia uchambuzi kuwa Mkude alifanya majukumu yake vizuri na aliiunganisha vizuri sana safu ya ulinzi na ushambuliaji..Hivi ni mkude huyu huyu aliyekuwa na pass accuracy mbovu kuliko wachezaji wote wa simba siku hiyo? Ina maana wachambuzi hamuoni udhaifu wa wachezaji kisa tu timu imepata matokeo?
Basi kama ni hivyo, hakuna kazi rahisi kama kucwa mchambuzi wa soka bongo.
weka na mechi mbili zilizopitaMUGALU Hana ball control kabisa,
-Mtu ana possession lost Mara 10,
-ata kupambania mipira na mabeki bado tu anafeli sana,
Cheki aerial duels, takwimu zake haziridhishi.
Pia
Tizama eti katika ground duels 9 anafaulu 1 TU[emoji848]
- ameshindwa hata kudribble MPIRA wowote mechi nzima.[emoji116]
View attachment 1746691
mkuu...we jamaa unajua sokaMUGALU Hana ball control kabisa,
-Mtu ana possession lost Mara 10,
-ata kupambania mipira na mabeki bado tu anafeli sana,
Cheki aerial duels, takwimu zake haziridhishi.
Pia
Tizama eti katika ground duels 9 anafaulu 1 TU[emoji848]
- ameshindwa hata kudribble MPIRA wowote mechi nzima.[emoji116]
View attachment 1746691
Sawa, nawekaweka na mechi mbili zilizopita
Hahaha samahani mkuu. Lakini labda nimetumia maneno mabaya kufikisha ujumbe wangu.Mkuu..kwa busara na hekima uliyoitumia kuandika post yako...kwa akili kubwa ya soka uliyoitumia kutetea hoja yako...na kwa ubobevu wa soka ulioonekana kwenye comment yako....Haukustahili kumaliza kwa kuandika hiyo mistari miwili ya mwisho.
Hivi mtu akiwa amevaa suti imemkaa smart, na kiatu kimemkaa poa halafu suruali ikawa haina zipu, huyo mtu anabaki kuwa smart au kuna jina jingine?