Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Naelewa, na nakubaliana na yet kua mkude performance Ni NDOGO mno.

Ila
Nlichokua nabishana na mtoa mada.

Ni suala la yeye kuja kuwadis wachambuz alafu Hana takwimu yoyote kusapoti.

Ndo maana nmemsaidia kumuwekea takwimu.

ANACHOLALAMIKIA MTOA MDA KINA MANTIKI KUBWA SANA.
 
Tafadhali leta na Pass accuracy ya Lwanga kama ulivyoleta ya Mkude....halafu ndipo utaelewa ninachomaanisha.
Pass accuracy ya TADEO LWANGA ilkua NI 92.4%[emoji116]
 
hahahah na mtoa mada ndo mimi hapa ambae nashukuru umeelewa...sema poa mkuu,,, next time nita attach stats ili kuweka msisitizo kwenye hoja yangu...ila kwa wale walioangalia game hawakuhitaji hata statistics...pamoja mkuu.
 
Kwa Mugalu sina neno ila kiufupi ni kwamba ni mwendawazimu pekee atakayeamin kuwa Mugalu ni Striker wa kutisha.

Kuhusu Mkude nakubali kabisa, jamaa alishapotea toka dakika ya kwanza mpaka ya mwisho, hakuwa mchezoni kabisa.
Nnachoona MUGALU anaonyesha Sana poor performance tofauti na wenzie wanaocheza the same number.
 
hahahah na mtoa mada ndo mimi hapa ambae nashukuru umeelewa...sema poa mkuu,,, next time nita attach stats ili kuweka msisitizo kwenye hoja yangu...ila kwa wale walioangalia game hawakuhitaji hata statistics...pamoja mkuu.
Mi game sjaangalia, ila Ni mfuatiliaji mzur wa takwimu.
 
Basi hapo ndio tumepishana mkuu.
Mi game sjaangalia, ila Ni mfuatiliaji mzur wa takwimu.
Ila naamini hata kama ungeangalia wala usingehitaji takwimu kabisaa...Mambo yote yalikuwa wazi
 
Kazi ya striker ni kufunga magoli. Ni kweli kabisa. Lakini hii kauli ni kauli ambayo ingefaa kutumika kwa mtu mwenye traditional approach katika mpira. Yani mtu mwenye mtizamo ya kizamani kuhusu mfumo wa soka.

Kwasasa tupo katika zama za mpira ambazo wameibuka ma technicians wengi waliobadilisha kabisa approach ya soka mfano tukianzia na Frank Riijkard, Pep Guardiola, Jurgen Klopp na wengineo wengi tu.

Mifuno au style za uchezaji wa team za hawa makocha ni tofauti kabisa na zile ambazo zinategemea target man kama striker awe ndio main source ya kufunga magoli katika team.

Ndio maana hii mifumo ya kisasa utakuja kugundua mipira mirefu hutumika mara chache sana. Style hizi za kisasa za mpira zinahitaji ku build up play kuanzia nyuma na wachezaji ku interchage position na pass kwa haraka kuelekea goli la mpinzani au ku retain possesion wakati wakitafuta njia ya kuipita defense ya upinzani.

Hii ndio sababu katika team za namna hii utakuta hata distribution ya magoli kwenye team ni kubwa tofauti na mifumo ya kizamani ambayo unakuta kwenye team striker ndio amefunga magoli zaidi ya 80% kwenye team.

Ndio maana siku hizi si ajabu kukuta wachezaji wa nafasi za kiungo (play makers) wakiwa na magoli mengi kuliko hata (goal getters).

Kwahiyo mkuu mimi nadhani Mugalu pamoja na kuwa anakosa sana nafasi za kufunga lakini ana umuhimu sana kwenye team kama alivyo Kagere.

Mwisho wa siku ni kuwa team glory ndio muhimu kuliko personal glory. Nikimaanisha team kupata matokeo ndio kitu cha msingi zaidi kuliko kuangalia nani amefunga magoli.

Angalia pale Liverpool mtu kama Bobby Firmino yeye ndio striker lakini hafikii hata 1/3 ya magoli ya Mo Salah ambae ni winger. Lakini kocha anampanga kila siku kwakuwa anajua katika mfumo wake Bobby anafanya majukumu yake kama inavyotakiwa na ndio maana Salah au Mane wanafunga. (Huo ni mfano mmoja kuna mifano mingi kwenye team nyingi).

So mkuu sikubaliani na wewe. Na pia chakujiuliza wewe pia ni kuwa je wewe unajua sana mpira au ukocha kumshinda Da Rosa?
 
Mkuu..kwa busara na hekima uliyoitumia kuandika post yako...kwa akili kubwa ya soka uliyoitumia kutetea hoja yako...na kwa ubobevu wa soka ulioonekana kwenye comment yako....Haukustahili kumaliza kwa kuandika hiyo mistari miwili ya mwisho.

Hivi mtu akiwa amevaa suti imemkaa smart, na kiatu kimemkaa poa halafu suruali ikawa haina zipu, huyo mtu anabaki kuwa smart au kuna jina jingine?
 
ball control na kumiliki mpira kuweza kusumbua mabeki ndio kinampa namba na sio uwezo wake wa kufunga au kukosa na simba haitegemei magoli yake sana bali kazi yake
MUGALU Hana ball control kabisa,

-Mtu ana possession lost Mara 10,

-ata kupambania mipira na mabeki bado tu anafeli sana,

Cheki aerial duels, takwimu zake haziridhishi.

Pia
Tizama eti katika ground duels 9 anafaulu 1 TU[emoji848]

- ameshindwa hata kudribble MPIRA wowote mechi nzima.[emoji116]


 
Kuhusu Mkude wachambuzi wetu wanaturudisha enzi zile mipira haionyweshi live, Mkude anashindwa kutoa hata pasi, uchezeahaji wake ni aina moja pasi ndefu za pembeni
 
weka na mechi mbili zilizopita
 
mkuu...we jamaa unajua soka
 
Hahaha samahani mkuu. Lakini labda nimetumia maneno mabaya kufikisha ujumbe wangu.

Labda niseme tu kuwa kutokana na Simba kumpa dhamana ya kuifundisha team na kuisimamia katika mechi basi yeye kocha ambae ndio anafanya mazoezi na wachezaji anajua ni mchezaji gani amtumie lini na sehemu gani.

Hivyo Da Rosa ambae nina uhakika ana elimu ya mpira kutushinda wengi ni wazi kuwa kuna kitu anakiona kwa Mugalu na ndio sababu anampanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…