Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

TUMJADILI MUGALU KWENYE
Mechi ya Simba vs Al mereik 3:0

Iyo mechi Simba walishambulia Sana, na kuutawala kabisa mchezo.

1. Simba walipiga JUMLA ya mashuti 11.

Cha ajabu, MUGALU alipiga shuti moja tu on target na ndo lilikua goli.

2. mugalu hakupiga key pass yeyote ile pamoja na kua Simba walkua kwny rythm nzur ya mchezo.

3. Tofauti na goli alilofunga, MUGALU alkua na pass accuracy mbovu kabisa ya passi 13 TU, sawa na 68%

4. Mugalu bado suala la kumiliki MPIRA lilimsumbua Sana, akiwa na possession lost Mara 10.
Ambapo kwa nafas anayocheza iyo Ni BIG SHAME.

5. Kuwaumbua mabeki,
Mugalu ameshindwa kabisa kugombea mipira na mabeki wa Tim pinzani.

- kwenye ground duels (mipira ya chini) 8, amewin 2 TU sawa na 25%

-kwenye aerila duels (mipira ya juu) 4, amewin 1 TU sawa na 25%

6.KEY PASSES,
pamoja na Simba kudominate Sana ule mchezo,
bado mugalu ameshindwa ata kutoa key pass yeyote sawa na 0%

NAWEZA KUHITIMISHA KUA IYO MECHI, Mbali na kufunga Lile goli, performance bado ilkua chini.

mugalu alibebwa na performance ya wenzie

NMEAMBATANISHA TAKWIMU HAPA CHINI[emoji116]
 
Mi pia naungana na wewe,
Huenda kocha anamuandaa kwa matumizi ya baadae.
 
MUGALU Hana ball control kabisa, -Mtu ana possession lost Mara 10,
Ila lazima uzingatie kwamba mpira huanzia nyuma na kuishia mbele, kwa hiyo it is likely kwa striker kupoteza mipira zaidi kuliko beki au kiungo, maana striker lazima ufanye jitihada kuingiza mpira wavuni, wakati beki na kiungo wanafanya jitihada kuupeleka kwa striker
 
Mkuu nimekuelewa sana katika hoja zako na namna ya uwasilishaji wako.

Safi sana.
 
Mpira wa kisasa unachezwa KISAYANSI

Zamani ilikua ni kama kazi ya striker ni kufunga tu....... yaani usipofunga wewe hufai

Lakini siku hizi hata striker wasio funga sana wanakua na majukumu yao uwanjani kwa mujibu wa mbinu za kisayansi za mwalimu

Hata hivyo hakuna kazi rahisi duniani kama kuwa mchambuzi wa soka

Mpira kabla haujaanza utaipa simba kila sifa na sababu za kushinda
Mpira ukiisha simba kafungwa unamtafuta mtu wa kumbebesha lawama ama awe kocha kapanga vibaya au Chama alicheza chini ya kiwango
 
Tatizo kubwa nnaloliona kwa MUGALU,
Ni kukosa chemistry nzuri na LUIS Mikson.

Najaribu kufuatilia Player performance rating za mechi zote 5 za caf alizocheza Simba.

Utagundua kua,
Wote Mikson na Mugalu wakianza,
mmoja wao atang'aa uku mwingine atafifia.

Yaani,
-miksoni akiwa kwenye PEAK, uyu MUGALU atapoteana.

-Mugalu akiwa kwenye PEAK, Luis Mikson atapoteana.

Ningumu kabisa wote wawe kwenye peak in the same match.

Tizama takwimu hapa chini[emoji116]
 
Ni too much ukilinganisha na wenzie, kwa maana Simba Haina striker mmoja.
 
Kocha anatakiwa afanye kazi kubwa ya kuwaunganisha Luis Mikson na Kris MUGALU wacheze pamoja kwa high performance.

Inavoonekana hawana chemistry nzuri wakicheza pamoja.

Mikson akiwa kwny Utamu wake,
MUGALU anaonekana galasa.

Kwa lugha nyepesi,
MUGALU ANAFUNIKWA NA UWEPO WA MIKSONI.
 
naona mnamponda tuu Mugalu ila naona ni mtu anayewapa presha sana mabeki na kuwafanya miksoni na chama wawe huru kufanya wanachotaka

Angalia hata jinsi anavyojiposisheni huwezi mfananisha na Kagere hata kidogo Kagere mda mwingi anatumia kukimbia kimbia na kupiga makofi kama Pimbi

Mugalu Kagere na Bocco namuweka Bocco sababu hakosi nafasi hovyo.

Mugalu anapata nafasi na ataendelea kupata nafasi sababu akiwa uwanjani hawapi nafasi mabeki wa timu pinzani kupanda kusaidia mashambulizi na ndo sababu kocha anamtumia maana akianza anawafanya wachezaji wengine wawe huru.

Ni sawa na beki mshambuliaji
 
Ni too much ukilinganisha na wenzie, kwa maana Simba Haina striker mmoja.
acha uongo

unataka useme Kagere ambaye hata kutuliza mpira awezi anamzidi possesion Mugalu

kagere ambaye anasubiria mpira uwe mbele yake tena chini ndo aweze kucheza
Kagere hana tofauti na Sarpong tofauti timu tuu
 
... lakini anayecheza uwanjani ni mmoja at a time
Simba wanatumia 4-4-2 kwa maana ya 2 strikers mbele.

Ambae Ni MIKSONI na MUGALU.

Ndo maana nkasema, Kuna mmoja ANAFUNIKWA mwenzie.

Au labda kocha anatumia ile mbinu ya false striker,

yaan kwenye line up inaonekana wako striker 2,
ila ukiangalia uchezaji wao mipira kule mbele analishwa mmoja TU na mwingine anashuka chini.

Ndo maana sometimes,

hii inawezekan ikaw ndio Siri ya ushindi anayoitumia kocha kupata matokeo mara KWA Mara kwa kuwavuruga wapinzani.

Na anaonekana wote kuwahitaji kwa kila mechi na kwa wakati mmoja.

Kikubwa, Simba inapata matokeo.

Mbinu za kocha inapaswa ziheshimiwe.
 
acha uongo

unataka useme Kagere ambaye hata kutuliza mpira awezi anamzidi possesion Mugalu

kagere ambaye anasubiria mpira uwe mbele yake tena chini ndo aweze kucheza
Kagere hana tofauti na Sarpong tofauti timu tuu
Lete takwimu mkuu, tubishane kwa takwimu
 
Simkubali mugalu hata kidogo kufunga magoli.
Umegusa maeneo yote muhimu kiufundi. Makocha kama mourinho wanatumia mfumo wa build from the back and safety first.. yaani move inanzia kutoka kwa beki-kati-forward-striker-goli, namfananisha mugalu na jesse lingard hawa muda wote wanachase mpira ndani ya final third na hivyo kusababisha mabeki wasiwe na utulivu muda wote na kuwa na hali ya Kuondoa hatari golini haraka na kupeleka kwenye usalama, kwahiyo move ya kutengeneza goli inaharibika na hivyo timu kushambuliwa mara chache sana.

Mkishambuliwa move ikiharibika mpira unarudishwa kwa mabeki ili wahold na wachezaji warudi kwenye position zao then move inaanza upya, sasa kama mbele kuna mkabaji mzuri anayewin mipira inakuwa ngumu kurudisha mpira na hivyo timu pinzani inacheza ikiwa na presha na disorganized muda wote. Tumeona vita hawakuwa na utulivu muda wote na baada ya mugalu na mkude kutoka vita walipata utulivu na kuwa organized kuliko kipindi cha kwanza

Kikingine wanawazuia mabeki kupanda mbele kuongeza mashambulizi. Simba imefanikiwa sana hapa.
Kuna vitu vingi vinatokea uwanjani lakini huwezi kujua sababu ni nani
 
Simba inatumia mfumo wa Striker mmoja hasa kwa kutumia 4:2:3:1, mfumo huu ni Mugalu tu ndio anauweza vzr pale Simba, lbd na Bocco kidogo sana!

Kagere hauwezi kwasababu amezoea Striker wawili, Kagere hana utulivu kule mbele anapenda kuzunguka sana na kuwafanya mabeki kuwa huru muda mwingi!

Ukitaka kujua umuhimu wa Mugalu angalia mechi na Ali ahly baada ya Mugalu kutolewa akaingia Kagere tulishambuliwa sana,hii ilitokana na Mabeki kuachwa huru muda mwingi na kufanikiwa kuanzisha mashambulizi dhidi yetu bila kubughudhiwa na Striker
 
Miq amepewa uhuru wa kuzunguka na kufanya chochote uwanjani, utamkuta kulia, kushoto, Kati anarudi nyuma kukaba na anawin mipira karibu yote na kila position anaimudu yaani amechukua uhuru wa chama kwa asilimia kubwa.. morrison nae alianza kucheza Kati akaja kulia na baadae kushoto na kutoa assist ya goli.. kocha ana vielementi vya total football kila mchezaji yupo active muda wote na hukuna majukumu specific ndio maana unaona beki, kiungo, forward, striker wote wanafunga idadi sawa ya magoli.. bonge la kocha
 
Kuhusu mkude nadhani wale jamaa walikuwa wanafika sana miguuni bila kumpa utulivu

Ibenge anajua kazi ya mkude ivyo alikuja na plan ya kumnyima utulivu

Kocha naona aliamua kuzidi kumpa nafasi kwa sababu mara nyingi pasi zake ni sahihi zaidi kuliko mzamiru, mbali na kucheza ovyo ila niliona lwanga alipata utulivu na kutocheza faulo nyingi kama mechi zilizopita.

Kuhusu mugalu nadhani wanachambua ivyo kwa vile timu inapata matokeo

Yote kwa yote wachambuzi wetu ndio walivyo
 
Naomba kila ukiwa unapost mambo ya soka uwe unani tag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…