Baada tu ya kufunga ndoa inatakiwa kushirikiana au kuweka mawasiliano namna mtakavyotumia fedha zenu kama wanandoa lakini ukiona mwanamke ameanza kujenga kwa Siri bila mume wake kujua hapa kuna tatizo ,na hasa ni mwanaume inawezekana siku za mwanzo tumekubaliana vizuri lakini kadiri siku zilivyoendelea mambo yameenda kombo.
Kwa mfano mwanamke amebaini kuwa mume wake anachepuka sambamba na kumjengea huyu mchepuko nyumba,pia mwanamke ikitokea shida au tatizo upande wa kwao wewe mwanaume umekuwa hutoi msaada wowote hapo ni balaa jingine.
Vilevile mwanamke akishakuchoka yaani amevumiliaaaaaa sasa anasema liwalo na liwe basi anaamua kujenga kwa Siri na kutafuta mchepuko kwa Siri hivyo ndoa hiyo lazima ivunjike kwa hiyo mkuu hapo hauna msaada mwingine zaidi ya kuvunja ndoa sijui kwa ndani hizi ndoa lakini kwa hatua hiyo mwanamke alikuwa anasubiri tu wewe ugundue ili iwe sababu.
Yaani hakupendi tena moyo wake umekufaaaaa yote kwa yote hapo juu kuna dada zetu tafuta pm mmoja andaa ndoa ya mkataba.
Asante