Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Watu wenye uelewa mdogo na masuala ya utawala wanapotosha mambo, siyo kwamba wametumwa hapana, shule ni ndogo sana.
Mwarami Mohamed alikuwa Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, wakati huo kocha akiwa Kim Poulsen, benchi la ufundi lilipovunjwa kwa matokeo mabovu, Mwarami, Nsajigwa waliondolewa pia.
Wakati huo Simba haikuwa na Kocha wa Makipa, Mwarami alichukuliwa na Simba bila mashabiki, wanachama kujua. Kwa sababu hayo ni mambo ya ndani ya klabu, siyo kila jambo litakuwa hadharani, kwa mfano sikuona haja kwa Simba kutangaza kuingia mkataba wa kisheria na Mwarami wakati ilikuwa ikifanya kazi naye kwa muda maalum.
Kwenye uongozi kuna mambo utawaeleza mashabiki na kuna mambo yatabaki siri, na kuna mengine ni ya kawaida tu, hayawezi kutangazwa, mfano ujenzi wa uwanja sasa hivi unakwenda vizuri tu, lakini suala hilo halijafikia hatua ya kutangazwa.
Tuviachie vyombo vya dola viendelee na uchunguzi, kama Simba wanasema walikuwa naye kwa mwezi mmoja, CEO wake ataitwa athibitishe ukweli wa barua yake kuhusu Mwarami.
Lakini kubwa zaidi, Mwarami amedaiwa kukamatwa na unga haramu na wenzake, Mahakama haijathibitisha makosa hayo, hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa bila kusikilizwa. Mwarami siyo mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni 'accessory to the fact' tu.
Hoja za kisheria zitawasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka ambao watatakiwa kuthibitisha pasi na shaka kuhusu mashtaka na mshtakiwa Mwarami na wenzake watawasilisha utetezi wao, Mahakama itasikiliza ushahidi wa pande zote mbili na baadaye itatoa hukumu.
Mtu mmoja kufanya kosa isionekane kuwa taasisi nzima ndiyo inahusika, ingawa uchunguzi ukiendelea chochote kinaweza kutokea. Mfano wewe ni mtumishi wa kampuni ya ulevi, ukishikwa na bangi mtaani ndiyo tuamini taasisi nzima inahusika? Mwanao ajihusishe na Panya Road halafu baba naye aingizwe kwenye kundi la Panya Road, hapana.
Ushauri wangu, masuala ya kisheria yaachwe kwa wanasheria, siyo kila jambo muone mna uwezo wa kulichambua, nyie mambo ya uchumi mmo, siasa mmo, sheria mmo, mpira mmo, mnadhihirisha kuwa nyie ni makanjanja tu.
Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app