Hayo mambo yaliyojadiliwa kwenye familia ya Mwinyi kama kweli yalijadiliwa, ni siri yao.
Lakini kimsingi, siku zote mtoto lazima azikwe pale walipozikwa wazazi wake, huu ndio utamaduni wetu, unalazwa pale walipolazwa ndugu zako wengine.
Sasa leo Mwinyi badala ya kuzikwa Mkuranga anaenda kuzikwa Zanzibar, kisa alisoma huko, hebu tuambie, kwa uamuzi wenu huo, hivi hamuoni kama mmemtenga na ndugu zake wengine waliozikwa huku Bara?
Ndugu yake yupi tena atakaekwenda kuzikwa nae Zanzibar, kama ni Rais Dr. Mwinyi, hamuoni pia hawa wawili mtakuwa mmewatenga na ndugu zao wengine waliozikwa huku Bara?
Hapo ndipo unapopata picha kwamba, huu uamuzi wa kumzika Mzee Mwinyi Zanzibar, ni purely political motivated.
Ndio maana kwasababu hizo za kisiasa, watajikuta ni wao wawili pekee, baba mtu na mwanae [kama nae atataka kuzikwa huko, sababu wanasema anaogopa baba yake kuzikwa bara sababu naye ataonekana sio mzanzibar na maadui zake kisiasa, sijui akiondoka madarakani hiyo hofu itabaki au ataondoka nayo] kama itabaki, ndio wawili pekee watakaozikwa Zanzibar, huku ndugu zao wengine wote wakizikwa Bara.
I never thought kama siasa ina nguvu kiasi hiki, au ni uoga tu wa mwanasiasa mwenyewe anayeamua kuchukua maamuzi yatakayokwenda kinyume na mila na desturi zetu, kwa maslahi yake ya kisiasa, hiki kilichofanyika kwa Mzee Mwinyi, binafsi sijakipenda, tunatakiwa siku yetu ya mwisho sote tulazwe pale walipolazwa ndugu zetu kama nafasi ipo.
Na ndio maana pia, wengine wetu ambao hawana uwezo wa kusafirisha ndugu zao, hupeleka udongo wa pale alipozikwa ndugu yao nyumbani kwao uende kuzikwa huko, yote hii ni ili kuonesha umuhimu wa kumzika marehemu pale alipozaliwa, nashangaa na kusikitika kwanini wamemuondolea Mzee Mwinyi haki yake hii, ikiwa uwezo wa kumsafirisha na kumzika nyumbani kwao Mkuranga upo, sio fair.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app