Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Kazaliwa bara ila kwao ni visiwani
 
Hoja yako yote imejengwa katika wosia wa Mwinyi ambao hujaweza kuthibitisha upo.

Ni hoja ya kizushi tu.
 
Haya mengine ni matatizo ya kisaikolojia tu.
 
Hayo ni maono yako mtoa mada,nakumbuka nilipokuwa nasoma kule st mathew mbagala kila week mzee mwenye nilikuwa namwona na king'ora chake anaenda mkuranga kwao...hii ya znzbr imenishangaza kidogo...yasemwayo yapo .....
 
Upo sahihi mkuu
 
Hayo ni maono yako mtoa mada,nakumbuka nilipokuwa nasoma kule st mathew mbagala kila week mzee mwenye nilikuwa namwona na king'ora chake anaenda mkuranga kwao...hii ya znzbr imenishangaza kidogo...yasemwayo yapo .....
Mkuranga ipo ndani ya JMT na Zanzibar pia ipo ndani ya JMT. Sasa hapo tatizo liko wapi?

Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar walitokea mikoani, na wengi waliokufa wamezikiwa hapa hapa Dar, mbona hamshangai au kuuliza kuhusu hilo?
 
Kasema nani kwao na Mwinyi ni Mkuranga?
Kasema mwenyewe kipindi cha kuzindua kitabu cha maisha yake. Anasema alipelekwa katika kisiwa hicho kwa lengo la kusoma dini ya kiislam. Ndiomaana unaona kuna mjadala wa watu kushangaa kwanini azikiwe Zanzibar na sio kwao Mkuranga.

Miaka 1950 kushuka chini Zanzibar ndio ilikuwa kitovu cha mafunzo ya dini ya kiislam. Hivyo wazazi wengi waliopenda dini kutoka katika nchi mbali mbali waliwapeleka watoto wao wakasome dini katika kisiwa hicho.

Historia inasema hata Abeid Amani Karume alipekwa Zanzibar na wazazi wake kusomea dini. Abeid Amani Karume asili yake ni Malawi, kutoka kabila la wayao wa upande wa Malawi, maana kuna wamalawi wa upande wa Tanzania pia.
 
Uzikiwe popote pale ila matendo yako ndio yatakayokusaidia huko kaburini.

Allah amjaalie qauli thabit mzee wetu, amuingize katika pepo!
 
Je sisi tulio zaliwa Tanganyika tukifa tunazikwa wapi maana saivi Tanganyika haipo Kuna Tanzania na Zanzibar. 😂😂 Muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar umeleta Tanzania na Zanzibar kazi iendelee. Kuzikwa ni kuzikwa tu.
 
Akhsante sana ndugu Nguruvi3 .
Kongole kwa mchango bora sana.
Mjadala huu ufungwe sasa.
 
Alisema na kitabu kinasema alizaliwa Mkuranga- kuzaliwa hakuna mahusiano na kwao mtu ni wapi. Wapo watu wamezaliwa Kenya lakini kwao ni Tanzania kwa mazazi na sheria.
 
Alisema na kitabu kinasema alizaliwa Mkuranga- kuzaliwa hakuna mahusiano na kwao mtu ni wapi. Wapo watu wamezaliwa Kenya lakini kwao ni Tanzania kwa mazazi na sheria.
Kumbe unaandika kwa mifano ya mtu kuzaliwa Kenya. Mimi nilijua utakuja na uthibitisho wa kuonesha kuwa Mwinyi alizaliwa tu Mkuranga lakini wazazi wake ni wazanzibar.

Kama hauna vithibitisho vya kuonesha kuwa wazazi wake ni wazanzibar, basi hauna haki ya kunifanya mimi niamini ulichoandika.

Mimi nimethibitisha kwanza kupitia kuzaliwa, na pili kauli yake mwenyewe ya kupelekwa Zanzibar kusoma dini. Sasa na wewe thibitisha kwanza uzanzibar wake kupitia wazazi wake, na pili uniambie aliposema kuwa nilipelekwa nyumbani Zanzibar kusomea dini. Zaidi ya hapo utakuwa umeamua tu kubishana huku ukweli wa kile nilichoandika ukiwa unaujua moyoni mwako.
 
Sio familia yake ni yeye.kwa mfano uamuzi wa wewe kuzikwa Sehemu sio ya familia ni wako.
Lakini kumbuka uamuzi pia hubadilika. Ndomaana unaweza kusikia mtu anakwambia amebadili maamuzi yake.

Nikiwa na maana kwamba huenda kabla ya kukata roho watoto wake walikaa nae wakamshauri azikiwe Zanzibar na yeye akabadilisha uamuzi na kuridhia kile walichomshauri au kumuomba akubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…