Suala la PEPMIS: Serikali ikae chini ikatafakari upya

Suala la PEPMIS: Serikali ikae chini ikatafakari upya

jina baya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
573
Reaction score
377
Habari za wakati wajumbe.

Hili suala la PEPMIS naona kwa mtazamo wangu kama lina maswali mengi sana kuliko majibu.

Japo lengo la serikali ni zuri kabisa, la kutumia mifumo ya tehama na teknolojia kufanya performance appraisal lakini niishie kusema kwa mfumo huu naona kabisa halitatimia.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaibua sintofahamu juu ya uhalisia wa mfumo huo na namna unavyofanya kazi

1. Watumishi wengi hawana mafunzo muhimu kuhusu jinsi ya kutumia mfumo huo ipasavyo.
2. Kulazimisha mfumo uanze kufanya kazi mapema ilhali watu hawana uelewa nao.
3. Mfumo kutokuwa stable na unakuwa mzito mno.
4. Kutumia mfumo kupima watumishi jambo ambalo haliwezi kuwa kipimo sahihi cha kupromote watumishi kwasababu watumishi wengi wanaforce kujaza asilimia zifikie 60+

USHAURI
1. Serikali iandae fomu maalum zitakazojazwa na watu tofauti (supervisors) ili itumike kama atachment ya uthibitisho wa kazi.
2. Serikali itoe mafunzo kwa ngazi zote na itoe muda zaidi ili watu wauelewe huo mfumo.
3. Kurekebisha hali ya mfumo kuzidiwa.
4. Kwa kuzingatia changamoto zilizopo sasa ni uhakika kwamba promotions za mwaka huu zina walakini, hivyo kwa kuanzia serikali iangalie namna bora zaidi ya kukwepa lawama kutoka kwa watumishi.

Serikali hoyeeeee
CCM HOYEEEEEEE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIII
 
Huu mfumo kwakuwa una dosari nyingi na unaleta taharuki ni heri ufutwe. Kuanzia mwezi Julai watumishi tutakuwa busy kila wiki kujaza huo utahira. Wanaotaka huduma ofisi za umma kazi wanayo.
 
Hii nchi ukitaka kuwa serious utskufa siku Si zako....nimeona Viongozi wanahamasisha watu wafikie 100😁😁😁 Sasa wewe unaduburi Nini kujaza ufike 100! Maisha ni hayahaya! Wapo watu wanahalalisha propozo' lao la PEPIMISO'!
 
Hii nchi ukitaka kuwa serious utskufa siku Si zako....nimeona Viongozi wanahamasisha watu wafikie 100[emoji16][emoji16][emoji16] Sasa wewe unaduburi Nini kujaza ufike 100! Maisha ni hayahaya! Wapo watu wanahalalisha propozo' lao la PEPIMISO'!
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna uhalisia mkuu, afadhali OPRAS kulikuwa na shahidi anabalance kidogo pale mambo yaende ila huu hapana kwakweli...
 
95
Hii nchi ukitaka kuwa serious utskufa siku Si zako....nimeona Viongozi wanahamasisha watu wafikie 100😁😁😁 Sasa wewe unaduburi Nini kujaza ufike 100! Maisha ni hayahaya! Wapo watu wanahalalisha propozo' lao la PEPIMISO'!
95 inatosha tukutane July Mosi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna uhalisia mkuu, afadhali OPRAS kulikuwa na shahidi anabalance kidogo pale mambo yaende ila huu hapana kwakweli...
kwani si kuna KPIs ambazo unapaswa kuzifikia na kuweka maripoti au huo mfumo wenu ukoje huku vijana wakimaliza wanaenda kuoga na sabuni ya unga wanaonyesha kila mtu kafanya kazi ngapi nawalipa posho wanasanzuka tutaonana kesho asubuhi
 
Mwl jitahidi uendane na mifumo
Muhimu,,,lakini kwa upande wa walimu sidhani kama utendaji unaweza ukapimwa kwa pepmiss maana kinachojazwa ni tofauti na kinachotekelezwa,,,na kama wametumia pepmiss believe me or not wachapakazi wengi wameachwa na tunakoelekea watu wataconcentrate kujaza matango pori kwenye pepmiss na kuwasahau wanafunzi
 
Habari za wakati wajumbe..
Hili suala la PEPMIS naona kwa mtazamo wangu kama lina maswali mengi sana kuliko majibu.
Japo lengo la serikali ni zuri kabisa, la kutumia mifumo ya tehama na teknolojia kufanya performance appraisal lakini niishie kusema kwa mfumo huu naona kabisa halitatimia.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaibua sintofahamu juu ya uhalisia wa mfumo huo na namna unavyofanya kazi
1. Watumishi wengi hawana mafunzo muhimu kuhusu jinsi ya kutumia mfumo huo ipasavyo.
2. Kulazimisha mfumo uanze kufanya kazi mapema ilhali watu hawana uelewa nao.
3. Mfumo kutokuwa stable na unakuwa mzito mno.
4. Kutumia mfumo kupima watumishi jambo ambalo haliwezi kuwa kipimo sahihi cha kupromote watumishi kwasababu watumishi wengi wanaforce kujaza asilimia zifikie 60+.

USHAURI
1. Serikali iandae fomu maalum zitakazojazwa na watu tofauti (supervisors) ili itumike kama atachment ya uthibitisho wa kazi.
2. Serikali itoe mafunzo kwa ngazi zote na itoe muda zaidi ili watu wauelewe huo mfumo.
3. Kurekebisha hali ya mfumo kuzidiwa.
4. Kwa kuzingatia changamoto zilizopo sasa ni uhakika kwamba promotions za mwhani udgdaka huu zina walakini, hivyo kwa kuanzia serikali iangalie namna bora zaidi ya kukwepa lawama kutoka kwa watumishi.

Serikali hoyeeeee
CCM HOYEEEEEEE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIII
Nadhani umeliwa kichwa kama mie
 
Huu mfumo umenizuia nikose mshahara mwezi wa tatu na sababu unazopewa jaza subtasks sasa sijui ni mtu gani asiyejitambua kwa mwezi wa tatu awe hajajaza hizo vitu zao kama wanavyotaka.
 
Back
Top Bottom