Suala la Polepole linadhihirisha hata Rais afanye nini ni vigumu kuwavutia team Magufuli

Suala la Polepole linadhihirisha hata Rais afanye nini ni vigumu kuwavutia team Magufuli

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Niongezee kidogo..... Swala la gazeti la Uhuru kusema Samia hatagombea nazani ndio hisia na takwa halisi la mfumo ulioachwa...

Kwenye suala la chanjo Polepole hana hoja yoyote ile ya kisayansi au kitabibu. Anachotaka ni kuuambia umma kuwa kiongozi aliyepita alikuwa Bora kuliko huyu.

Nilisikia michango yake bungeni pia. Ametumia muda mwingi kutetea mitazamo ya Magufuli kuliko kupigania maswala ya kitaifa.

Uzalendo wa kizamani ni imani mbovu sana inayoingia na kutawala ndani ya roho za watu. Watu uanza kuamini Ngozi yao ni Bora kuliko zingine, Taifa lao ni Bora kuliko mengine, Chama chake ndio sahihi kuliko vingine na Baadae yeye na kiongozi wake ni Bora kuliko wengine.

Imani hii hujenga chuki kubwa Sana kwa mtu mwenye mtazamo tofauti.

Kwa wasiojua historia waambiwe jinsi Ujerumani yenyewe na dunia zilivyoangaika kuitoa Imani Kali ya kidikteta ya Kinazi miaka mingi baadae baada ya kufa muasisi wake Adolf Hitla.

Polepole katumia chanjo kuonesha hisia zake.
 
Laana ya kumbambika Mbowe ugaidi itamfuata huyo mama hadi siku ya mwisho , kumbuka kwamba bilionea Polepole hata akivuliwa ubunge hatojali kitu , huyu aligawana pasu kwa pasu na wasaliti kutoka kwenye kitita walichohongwa ili kuisaliti Chadema , anamiliki hela kibao
 
CCM ni moja.....

Ndg.yetu Kamarada Polepole tunamkumbusha kuwa AIHESHIMU SERIKALI KAMA ALIVYOIHESHIMU AWAMU YA 5......

Polepole anajua....
Polepole hajasahau kuwa CCM ni chama cha kijamaa na si cha kiliberali.....MWENYEKITI NI KIOO CHETU.....

#SiempreCCM
#HastaLaVictoriaCCM
#MwenyekitiWaCCMNiKiooChetu
 
Iko wapi chanjo ya ukimwi? Ugonjwa ambao umekuwepo toka 80's na umewatesa watu wengi sana, imekuwaje ugonjwa hauna hata miaka miwili upate chanjo?
Kwa hiyo wewe unajifukiza?
 
Mama atatapika alicholishwa na mzungu ili apewe chanjo, tunaomba watz mkachanje kuepusha mgogoro kati ya amiri jeshi na mataifa makubwa (donor country).
 
Kama amemdharirisha au kumdharau mwenyekiti wa chama chenu, kweli mnaweza kumtolea povu; lakini kama ametoa mawazo na mtazamo wake kuhusu chanjo, hata kama mtazamo wake unakinzana na mtazamo wa mwenyekiti, hiyo ni demokrasia. Heshimuni maoni na mtazamo wake, hakuna sababu ya kutoa povu.
 
Back
Top Bottom