Suala la Polepole linadhihirisha hata Rais afanye nini ni vigumu kuwavutia team Magufuli

Suala la Polepole linadhihirisha hata Rais afanye nini ni vigumu kuwavutia team Magufuli

Ni lini utaihimiza serikali itenge bajetii ya kusaidia wataalamu wetu wa kisayansi watengeneze chanjo hapa nchini kukaabili magonjwa yanayotusumbua!? Mheshimiwa Raisi rais wa Iran amechanjwa chanjo iliyotengenezwa na raia wake jana.

Nina imani na Mama atawawezesha wataalamu wetu watuwezeshe watanzania kujitegemea katika masuala mbalimbali likiwemo hili la masuala ya utabibu.
Maabara tu yakuwapima hao virus iko moja tu Tanzania nzima. Sasa unazungumzia kuwa na maabara ya kutengeneza chanjo kweli
 
Laana ya kumbambika Mbowe ugaidi itamfuata huyo mama hadi siku ya mwisho , kumbuka kwamba bilionea Polepole hata akivuliwa ubunge hatojali kitu , huyu aligawana pasu kwa pasu na wasaliti kutoka kwenye kitita walichohongwa ili kuisaliti Chadema , anamiliki hela kibao
Sababu mbowe ni mtakatifu au,mbuzi kweli nyinyi.
 
chanjo ni kinga ya mwili na pia ni ni tiba ya kipato (biashara) hamna mtu atataka umuharibie biashara yake anyamaze tu
Hivi ulivyoenda kuchanja ulipimwa kwanza corona alafu ukachanjwa au ulichanjwa tu ili mradi tumia akili mkuu mnapigwa.
 
Hizi zitakuwa dharau, mbona hakuthubutu kukinzana mawazo na mwenyekiti aliyepita?
Hadi kudundika na kupiga magoti alikuwa anamfuatilizia mwenyekiti.
Kama amemdharirisha au kumdharau mwenyekiti wa chama chenu, kweli mnaweza kumtolea povu; lakini kama ametoa mawazo na mtazamo wake kuhusu chanjo, hata kama mtazamo wake unakinzana na mtazamo wa mwenyekiti, hiyo ni demokrasia. Heshimuni maoni na mtazamo wake, hakuna sababu ya kutoa povu.
 
Maabara tu yakuwapima hao virus iko moja tu Tanzania nzima. Sasa unazungumzia kuwa na maabara ya kutengeneza chanjo kweli
Hili nalo neno.

Lakini, uwepo wa maabara moja ya kupima virusi haizuii serikali kutenga fedha kwenye bajeti kuanzisha kitengo ama taasisi kabisa ya kutafiti na kutengeneze chanjo dhidi ya maradhi yanayotusumbua ikiwemo COVID.
 
Hivi ulivyoenda kuchanja ulipimwa kwanza corona alafu ukachanjwa au ulichanjwa tu ili mradi tumia akili mkuu mnapigwa.
sijasema nimechanja ndugu yangu na mimi si advocate wakuchanja wala kutochanjwa hiyo ni hiari na utashi wa mtu wala sina huo utaalam nafuatilia huku nikipima hoja za kila mmoja ila kwa sababu jambo hili ni la hiari ya mtu inabaki kuwa hivyo ila vita ninayo iona baadaye ni pale tutapoanza kunyanyapaana mitaani kwa wenye chanjo na wasio chanjo
 
Iko wapi chanjo ya ukimwi? Ugonjwa ambao umekuwepo toka 80's na umewatesa watu wengi sana, imekuwaje ugonjwa hauna hata miaka miwili upate chanjo?
kataeni basi na kumeza ARV nyie si mna akili sanaa
 
Kwenye suala la chanjo Polepole hana hoja yoyote ile ya kisayansi au kitabibu. Anachotaka ni kuuambia umma kuwa kiongozi aliyepita alikuwa Bora kuliko huyu.

Nilisikia michango yake bungeni pia. Ametumia muda mwingi kutetea mitazamo ya Magufuli kuliko kupigania maswala ya kitaifa.

Uzalendo wa kizamani ni imani mbovu sana inayoingia na kutawala ndani ya roho za watu. Watu uanza kuamini Ngozi yao ni Bora kuliko zingine, Taifa lao ni Bora kuliko mengine, Chama chake ndio sahihi kuliko vingine na Baadae yeye na kiongozi wake ni Bora kuliko wengine.

Imani hii hujenga chuki kubwa Sana kwa mtu mwenye mtazamo tofauti.

Kwa wasiojua historia waambiwe jinsi Ujerumani yenyewe na dunia zilivyoangaika kuitoa Imani Kali ya kidikteta ya Kinazi miaka mingi baadae baada ya kufa muasisi wake Adolf Hitla.

Polepole katumia chanjo kuonesha hisia zake.
Hata mm niko upande wa Polepole na simkubali huyo Samia wenu kwa lolote maana hakuna anachojua. Magufuli ni mwamba unaoishi ktk mioyo ya Watanzania
 
chanjo ni kinga ya mwili na pia ni ni tiba ya kipato (biashara) hamna mtu atataka umuharibie biashara yake anyamaze tu
Screenshot_20210805-080941.png
Screenshot_20210806-071958.png
 
Hili nalo neno.

Lakini, uwepo wa maabara moja ya kupima virusi haizuii serikali kutenga fedha kwenye bajeti kuanzisha kitengo ama taasisi kabisa ya kutafiti na kutengeneze chanjo dhidi ya maradhi yanayotusumbua ikiwemo COVID.
Sasa sampuli za ujiji zinatumwa dar. Ukipima unapata majibu baada ya wiki mbili. Ukiwa umepona au umekufa kabisa. Sasa Kama wameshindwa kuweka bajeti ata wapime kila mkoa hiyo bajeti ya vifaa vya kumtafiti huyo kirusi watanunu kweli. Kumbuka Afrika hakuna taifa lililotengeza chanjoa. Labda waje wazungu kutujengea huku.
 
Kwenye suala la chanjo Polepole hana hoja yoyote ile ya kisayansi au kitabibu. Anachotaka ni kuuambia umma kuwa kiongozi aliyepita alikuwa Bora kuliko huyu.

Nilisikia michango yake bungeni pia. Ametumia muda mwingi kutetea mitazamo ya Magufuli kuliko kupigania maswala ya kitaifa.

Uzalendo wa kizamani ni imani mbovu sana inayoingia na kutawala ndani ya roho za watu. Watu uanza kuamini Ngozi yao ni Bora kuliko zingine, Taifa lao ni Bora kuliko mengine, Chama chake ndio sahihi kuliko vingine na Baadae yeye na kiongozi wake ni Bora kuliko wengine.

Imani hii hujenga chuki kubwa Sana kwa mtu mwenye mtazamo tofauti.

Kwa wasiojua historia waambiwe jinsi Ujerumani yenyewe na dunia zilivyoangaika kuitoa Imani Kali ya kidikteta ya Kinazi miaka mingi baadae baada ya kufa muasisi wake Adolf Hitla.

Polepole katumia chanjo kuonesha hisia zake.
Samia hawajibiki kuwavutia timu bani na timu nani

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
RIP Magufuli,,, yaani Leo Pole Pole ni wa kutukanwa na kile ki ANDUNJE Steve Nyerere public?
Kisa kukataa chanjo?

Kweli dunia inajizungusha kwa kasi sana.
 
Ifikie sehemu ndugu zangu tuheshimu hisia za watu. Ukitaka kila mtu awe upande wako ni ngumu. Mtu akisimama akasema nachanjwa, hakuna wa kumnanga! Shida mtu akitoa uamzi wake kwamba sichanjwi; maneno yanakuwa mengi! Kwa nini lakini! Chanjo ni hiari! Anayesema nachanjwa publicly, na anayesema sichanjwi publicly wote wako sawa na Mama! Ni ujinga kumsema mtu katika hiari aliyoichagua! Ni ujinga kabisa
 
Back
Top Bottom