Suala la Q Chila na madhara ya kupiga ramli

Suala la Q Chila na madhara ya kupiga ramli

Kuhusu kurogwa na Diamond hilo namuunga mkono. Kwasababu Diamond alimroga Michael Jackson akafa, baadae akamroga R. Kelly akafungwa jela, sasa hivi kamroga Hermonize kaachwa na Kajala kabaki kuvuta bangi tu kama chizi. Ndio maana Ali Kiba hataki kumpa mkono anaogopa kuibiwa nyota na mbalamwezi zake. Hoo!
Aisee🤣😅
 
Bado huwezi linganisha Nyimbo za Q chillah na diamond Q chillah is real talented .

Drugs ndo zimeua Future yake plus wanawake so hizo nyingine ni sababu . Tu. Hazina maana

Maaana Jaydee kazimiwa clouds na still yupo strong than ever.
Jide ana discipline na anaheshimu career yake acha kumlinganisha na takataka kama Q Chillah.
 
Mkuu ungetufafanulia na sisi watu wazima Huyo Q Chilla ni nani au maana yake nini? Maana vijana mna lugha za kificho sana. Umeelezea kama sote hadi Sisi tunamfahamu huyo jamaa yako. Anahusika na nini?
You're on the wrong page, I mean if you don't understand then it wasn't meant for you.
 
Kuhusu kurogwa na Diamond hilo namuunga mkono. Kwasababu Diamond alimroga Michael Jackson akafa, baadae akamroga R. Kelly akafungwa jela, sasa hivi kamroga Hermonize kaachwa na Kajala kabaki kuvuta bangi tu kama chizi. Ndio maana Ali Kiba hataki kumpa mkono anaogopa kuibiwa nyota na mbalamwezi zake. Hoo!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Noted.
 
Alitoka kimuziki mwaka 2002 na wimbo wake " Ulinikataa". He was very big in the industry and he made a lot of money ( KWA viwango vya wakati huo)

Then baada ya miaka kadhaa akapotea hewani.

SABABU HALISI ILIYO FANYA Q CHILA AFE KISANII.

1. Alikuwa anatumia pesa zake vibaya bila mipango. Legend has it that aliwahi kupangisha nyumba kama tano KWA ajili ya michepuko.

2. Kibri na kugombana na wanamuziki wenzake mfano Jaffarai. Jaffarai alimualika CHILA afanye chorus ya wimbo wake baadae wakapishana kwenye malipo CHILA akaona suluhisho ni kuichukua hiyo chorus na kuitengenezea wimbo mpya akiuita ' my boo'. CHILA alijipambanua kama Msanii mwenye jeuri na kibri asiye weza ku keep urafiki na wasanii wenzake. So wasanii wengi wali m side line.

3. Dharau, jeuri na kibri KWA wadau wa muziki ( KWA maoni yangu hii ndio SABABU HALISI ya anguko la Q CHILA)

Legend has it that Q CHILA aliwahi kumzaba kibao Marehe Ruge Mutahaba ( Rest In Peace) jijini Mwanza or something baada ya show ya Fiesta. Kisa? Baada ya show Ruge alisema wasanii wote waliopanda jukwaani watalipwa kesho yake CHILA akasema yeye pesa yake huwa hailali nje then baadae issue ika escalate mpaka CHILA akampiga kibao Ruge.

Mimi Naamini hapo ndipo lilipo zaliwa anguko la CHILA kwenye muziki.

HE WAS BLACK LISTED

SOME YEARS LATER.

Ngoma za Q CHILA zikawa hazipigwi tena redioni.

Hakuna show wala simu ya show.

Hakuna endorsement.

Mwaka nenda mwaka rudi.

REACTION YA Q CHILA:

Kwenda KWA mganga kupiga ramli. Akaambiwa amefungwa.

Oga dawa oga dawa na wewe hakuna kinacho badilika.

CHILA akaona njia rahisi ni ku escape his problem through imagination, na kitu pekee kinge timiza hilo ni kuingia kwenye drugs.

CHILA akawa drug addict. Habari zikasambaa nchi nzima kwamba CHILA amekuwa teja.

CHILA ANA TUHUMU KUROGWA NA DIAMOND.

Mwaka 2009 Diamond Platnum anatoka kimuziki.

Mwaka 2013 Diamond akiwa juu sana kimuziki anahojiwa " kabla hujaingia kwenye muziki nani alikuwa role model wako?"

JIBU LA DIAMOND: Q CHILA.

Q CHILA ANATOA TAMKO KUHUSU DIAMOND KUMTAJA KAMA ROLE MODEL WAKE.

Miezi kadhaa baadae Q CHILA anasema AMEROGWA NA DIAMOND. Kwamba CHANZO CHA YEYE KUSHUKA KIMUZIKI NI KWA SABABU DIAMOND AMEIBA NYOTA YAKE. YANI ULE UKUBWA WA DIAMOND WA KIPINDI KILE ULIPASWA KUWA NDIO UKUBWA WAKE LAKINI HAKUWA HIVYO KWA SABABU DIAMOND AMECHUKUA NYOTA YAKE NDIO ANAITUMIA.

NSIO SABABU DIAMOND AMESEMA ALIKUWA ANAMUONA CHILA KAMA ROLE MODEL WAKE.

KITU GANI KILIPELEKEA CHILA KUTOA KAULI HIYO? CHILA atakuwa alienda kupiga ramli na mganga akaamua kucheza na akili yake na kumwambia Diamond ndio kachukua nyota yake (Kumbuka hiki ni kipindi ambacho CHILA alikuwa amekaa bila show ya maana KWA almost miaka mitano au sita hivi) Hii ina maana alikuwa na frustration na alisha kwenda kwa waganga kutafuta mchawi kumbe mchawi ni yeye mwenyewe.

REACTION YA DIAMOND: " SIWEZI KUIBA NYOTA YA TEJA"

KAULI ya CHILA dhidi ya Diamond ilizidi kumzika CHILA ktk ulimwengu wa muziki.

KWA sababu:

1. Diamond alikuwa anapendwa sana kipindi hicho kama Fei Toto alivyo kuwa anapendwa mashabiki ya Yanga. Kumsema Diamond vibaya kulisababisha aonekane hater wa Diamond lakini pia kilifanya mashabiki wa Diamond wamchukie CHILA.

2. KAULI ya Diamond " Siwezi KUIBA NYOTA ya TEJA " ilizidi kufanya CHILA azidi kupuuzwa KWA sababu ilithibitisha kwamba kumbe kweli CHILA ni teja, na teja ni mtu ambae hawezi kuaminika. Kampuni haiwezi kufanya kazi na teja. Hakuna kampuni yenye akili ingeweza mpa CHILA show wala ubalozi.

Ni kama vile Diamond aliwaambia wadau wa muziki acheni kufanya kazi na CHILA KWA sababu ni teja.

Isitoshe kitendo cha CHILA kusema kaibiwa nyota na Diamond tena hadharani kilionyesha yeye ni teja kweli kwa sababu mtu mwenye akili timamu asingeweza kuzungumza hivyo...

CHILA AJA NA MPYA MWAKA 2022.

Anasema SASA amekuwa Shareef Mganga.

Anatibu watu wenye matatizo mbalimbali.

Anaondoa vifungo n.k ( ,😂😂very funny wakati yeye mwenyewe anaonekana yupo kwenye kifungo)

Anasema amepewa mkoba na mizimu ya kwao ( ubabani)

Vita yake kuanzia kushuka KIMUZIKI HADI kuingia kwenye uteja inatoka KWA watu ubabani kwake KWA sababu hawakutaka yeye achaguliwe kupewa huo uganga ndio maana wakamtupia jini limkate mapema ILI huo uganga uende KWA mtoto mwingine ( wa ndani ya ndoa)

Ila pamoja na yote anasema tayari mizimu ya kwao imempa mkoba na.sasa yeye ni mganga kamili.

HAYO NDIO MADHARA YA KUPIGA RAMLI KWA WAGANGA.. OBVIOUSLY HII ISHU YA UGANGA NI MGANGA WAKE NDIO KAMWAMBIA KWAMBA ANA MAJINI WA UGANGA WANATAKA AWE MGANGA. NA KWAMBA NDUGU ZAKE WALIKUWA HAWATAKI APEWE UGANGA YEYE NDIO MAANA WAKAWA WANAMROGA ASIFANIKIWE NA NDIO SABABU YA KUSHUKA KIMUZIKI NA KUWA TEJA.

Watu wengi Wana amini CHILA amechanganyikiwa.

NDIO MAANA VITABU VYA DINI VINASEMA RAMLI NI HARAAM.
Kwa hiyo masister du wote aliotoka nao enzi hizo waelewe tu walitoka na kalumanzira Q- chila..🤣🤣🤣😅
 
We mjinga hujui hata nilichomaanisha
Mjinga wewe na ukoo wako wote. Ulichoandika kiko crystal clear na Q Chilla ni takakata na alipo ndipo stahiki yake, kupanga ni kuchagua.
Discipline discipline ........., anavuna alichopanda.
 
Kitu nilichojifunza kwenye maisha,wakati wako ukipita,kama hujafanya Cha maana,kuwa mpole tu,
Maisha hayana kanuni,
Hawa wahenga wa bongofleva,wawe wapole,kipindi wanawika,1999,2000+,kulikuwa hakuna social media,vyombo vya habari vilikuwa vichache,mziki ulikuwa hauna platform kubwa ya kujiuza kama sasa,tekinolojia ya mziki ilikuwa Bado ndogo sana,
Zama zimepita,ama wakalime matikiti,au wafungue vibanda vya mpesa maisha yaendelee,
Qchief,Duly Sykes,mandojo,Mr nice,Dudu baya,D knob,
 
Ila hela wamepata.

Hawa enzi zao walikuwa wanauza album kwa bei ya jumla kwa distributor

Milioni 50 wamezishika sana.

Master jay alikuwa anawasema wagosi wakaya na wasanii wengi wa zamani.. walikuwa wakipiga hela za kuuza album zao wanamfata master jay awauzie magari. Master jay anawaambia nunueni viwanja mjenge majumba wanamuona mkoloni.

Mwana fa kajisomesha ifm na mpaka masters uingereza kwa hela za mziki

Proff jay kajenga nyumba zaidi ya 3 zamani sana kwa hela za mziki wa kabla ya social media
 
Mkuu ungetufafanulia na sisi watu wazima Huyo Q Chilla ni nani au maana yake nini? Maana vijana mna lugha za kificho sana. Umeelezea kama sote hadi Sisi tunamfahamu huyo jamaa yako. Anahusika na nini?
Watu wazima wenzio wanafanya maridhiano ya kitaifa ww unatusumbua vijana mambo yetu ya qchilla
 
Enzi hizo za kale nilikuwa na rafiki yangu anajuana Q, kuna siku tukapita kwake kumsalimia, picha linaanza nyumba imejaa watu kibao (machawa), hapo amepanga kighorofa K,nyama... Ila Q was so humble, mcheshi, ye anasmile muda wote....tukamkuta Yuko na mdada hivi ukimuona tu unajua ni Ile midada ya mjini, midangaji.
Nakazia kilichomshusha ni bangi na wanawake.
 
Mkuu ungetufafanulia na sisi watu wazima Huyo Q Chilla ni nani au maana yake nini? Maana vijana mna lugha za kificho sana. Umeelezea kama sote hadi Sisi tunamfahamu huyo jamaa yako. Anahusika na nini?
Sema ufafanuliwe wewe mtu mzima na sio sisi watu wazima,watu wazima wanapigania katiba mpya wewe ni mzee muhuni tu
 
Sema ufafanuliwe wewe mtu mzima na sio sisi watu wazima,watu wazima wanapigania katiba mpya wewe ni mzee muhuni tu
Sasa unadhani hiyo mikakati ya katiba mpya mmoja ya wanaopanga ni nani kama si mimi mzee komeo? Nyie vijana msione mnapumua tu kwa mbele na kwa nyuma watu tunahangaika sana.
 
Huwez kuwa serious, hakuna namna nyingine ya kumwelezea q chilla , tofauti na alivo elezea mtoa mada . Muzic wa bongo fleva kama hukuufuatilia miaka ya 2000's .. kuendelea Basi apa utatoka mtupu
 
Back
Top Bottom