Suala la Simba kuzindua jezi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro sio suala la kimichezo ila ni la kiroho litakaloathiri sana siasa za Taifa letu

Halafu Kuna watu wataona jamaa kaandika pointi kweli!
 
Chuma liko kileleni linaunguruma na ndio mwanzo wa watu majikw kushika haramu ya kutafuta chakula na madume yanakula yanatia mimba yanasepa na vita ya wanaume baina yao itakuwa kubwa na taifa litazaana sana na umri wa kuishi utashuka, fisi wataongezeka, wanaume majabali watawatoa mimba wanawake wenye mimba za wengine ili wapandikize zao. Na nchii hii itabarikiwa kwa kutembelewa na wageni wengi sana
 
Mkuu nikiangazia bandiko lako Simba ki asili ilikua timu ya waarabu ndio kusema kwamba kupandisha bendera yao pale Kibo ni mwanzo wa utawala wa kiarabu/kisultani katika ardhi ya Tanganyika?
Good observation
 
Hivi huu ujinga wa simba na yanga waswahili mtaucha lini?watu mnaacha mambo ya msingi nchi inauzwa mko busy simba yanga hizi time hata ukizijumlisha zote uwezi pata timu moja,lakini mko busy sana na huu ujinga.
 
Huu Uzi Nimeelewa Sana Ila lazima uwe na mtazamo wa kiroho.
 
La Simba SC sijui ila la Mwenge huwa naamini hivo! Huwa nashangazwa sana eti VIONGOZI wanakula kiapo mbele ya torch ... 😁😁😁97
Na ukishaingia anga hizo unakuwa ..kama mashabiki wa Yañga ukimwondoa Mzee Manara na Kikwete!
Mwwnge ni kajini fulani kanushirikina wa moto chungiza hata wenye miradi binafsi waliopeleka mwenge ukazindue rudi baada ya miaka hata miwili unakuta mradi umefubaa kama watu wanavyochafuka miguu wakikesha kwenye mwenge. Itokee kiongozi autupilie mbali haya mambo ya kusonga na tulioyakuya ni utumwa
 
Hivi huu ujinga wa simba na yanga waswahili mtaucha lini?watu mnaacha mambo ya msingi nchi inauzwa mko busy simba yanga hizi time hata ukizijumlisha zote uwezi pata timu moja,lakini mko busy sana na huu ujinga.
Nchi ikiuzwa Tutapewa chetu kila mtu atatembea mwendo wa pesa. Ukiona inauzwa jiweke kwenye timu ya wauzaji hukosi maokoto😂😂
 
Mwenge wa uhuru ulivyozinduliwa kupitia ushauri wa kishirikina wa waganga wa kienyeji, tambiko lake lilikamilika kwa kwenda kuuweka katika kilele cha mlima Kilimanjaro. Kitu ambacho timu ya Simba inakifanya kina kila dalili ya ushirikina. Yaani badala ya wao kujikita katika masuala ya kiufundi katika soka wao wamebadili gia na kukimbilia mambo ya ndumba. Soka ya kileo ni sayansi, hizo sarakasi ya kichawi haziwezi kuwafikisha sehemu yoyote ile.

Ni mwaka jana tu mchezaji wa kizungu aliwakimbia kutokana na madai ya "black magic"! Sasa hivi wachezaji wao watashindwa hata kukaa vyema vitini kutokana kuchanjwa chale nyingi katika makalio yao.
 
Nchi ikouzwa Tutapewa chetu kila mtu atatembea mwendo wa pesa. Ukiona inauzwa jiweke kwenye timu ya wauzaji hukosi maokoto😂😂
Basi Jana yanga day mtu anaacha kazi zake anaenda kwenye huu ujinga,ccm wanawachora mkijakustu kila mtu kauzwa kwa mwarabu.
 
Basi Jana yanga day mtu anaacha kazi zake anaenda kwenye huu ujinga,ccm wanawachora mkijakustu kila mtu kauzwa kwa mwarabu.
Kwa wenye mapenzi haiwi ujinga maana ndio kitu anapenda na siwalaumu ccm kwakua hata hapo mwanzo bandari ilikua inaendeshwa na tikisi kibaya ni mkataba ambao utatuumiza baadae tutakapotaka kumtoa dipii wolidi na kumleta mwingine na vipengele vya maslahi kama hivyo
 
Sema swala la viongozi wa simba kufeli kufika kileleni na kuwaachia wabeba mizigo waende nazo lazima liighalimu sema kiroho
Kwani Nyerere, Kawawa, Bibititi & co. walifika kileleni?
 
Umesikia huko kuna mzungu kapewa heka million sita, hivi Usalama wa Taifa ndio wasaidizi wa mama chausiku katika kuuza ardhi ya Tanganyika?
Muwege mna uliza kabla ya kuropoka ..
Freedkin yupo Tanzania miaka zaidi ya 20 ...vitalu anavyo zaidi ya miaka 20...
 
Ile ilikuwa ni ibada ya "kimajinuni" ambayo imefanywa na Simba kuizidi Yanga na timu nyinginezo Afrika...

Watu wa Msimbazi wametimiza maneno ya miungu yao, haina uhusiano wowote na rangi nyekundu wala nyeupe...

Kiroho mtu anayeweza kufanya tambiko la kiibada juu ya kilele cha Kilimanjaro, ni kielelezo cha kutawala anga la Afrika nzima kwa kuwa ile ndio sehemu ya juu kuzidi zote juu ya bara la Afrika...
 
Kwani Nyerere, Kawawa, Bibititi & co. walifika kileleni?
Lakini alienza kuupandisha mwenge toka chini ndie aliyefika nao kileleni tofauti na Simba ambao wamebeba kibegi toka chini lengo ufike keleleni upige na picha harafu unaishia njiani kisa umechoka
 
Nimesoma nimeelewa ila tusubiri yajayo yatakuwwa mazuri kwa taifa letu.
Mama anaona mbali na anatupenda na kutulinda kama Simba anavyolinda ufalme wake msituni.
YAJAYO NI MAZURI TUSUBIRI MATOKEO.
hii nimeielewa vizuri, inawezekana SSC lengo lao la uziduzi likawa tofauti kabisa na hoja ya mleta uzi lakini nayaona mafunuo hapo. lengo la SSC ni kuwa juu kileleni lakini bado ni jambo gumu kwao kwa usajiri waliofanya.
 
hii nimeielewa vizuri, inawezekana SSC lengo lao la uziduzi likawa tofauti kabisa na hoja ya mleta uzi lakini nayaona mafunuo hapo. lengo la SSC ni kuwa juu kileleni lakini bado ni jambo gumu kwao kwa usajiri waliofanya.
Walishindwa kufika kileleni badala yake waliofika ni Wasaidizi wasindikizaji

Maana yake Azam FC ndio watang'ara Juu ya Simba SC 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…