Suala la Simba kuzindua jezi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro sio suala la kimichezo ila ni la kiroho litakaloathiri sana siasa za Taifa letu

Suala la Simba kuzindua jezi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro sio suala la kimichezo ila ni la kiroho litakaloathiri sana siasa za Taifa letu

Kisa kagusa timu pendwa
Katoa geography ya uwongo...mount everest ni mrefu kwa futi (au meters from sea level) hamna milima inayounganishwa urefu...mwambie akasome geography ya la sita ajue tofauti ya volcanic mountains na fold mountains na formation zake
 
Nje ya mada
 
Kiroho ieleweke mlima Kilimanjaro ni lango kuu la kuingilia kuzimu.
Ila haya mastori ya mtindo huu nimeyasikia sana ila bado atasielewi vizuri ko inawezekana ikiwa ni lango, elezea kidogo viashiria
Kuna mchizi wangu mmoja kipindi madarasa imemkolea aliniambia mfalme suleimani WA Israel alifika mlima Kilimanjaro kuja kuyazika majini matukutu
 
Hii ni hadi uzame zaidi au uwe mdau wa mambo ya kiroho mfano ya kutaka umaarufu, utajiri,upako,nguvu za mamlaka, uwezo wa kutenda miujiza ndo utayaelewa mambo haya.
Na mengine ikiwemo kwann mkoa wa MBEYA, Morogoro na Singida haipiti mwezi ajali.
Utaelewa kuhusu Gamboshi,Ngende Lindi,Nyumba nitu Njombe vinaconnection gani.
 
Duh!
 
Wasalaam.
Wanasema kila jambo fulani liwe zuri au liwe baya basi hutanguliza alama, dalili, viasharia na taarifa fulani za kimafumbo ambazo ni lazima watu wazima wakae chini, wapasue vichwa vyao kuweza kuzi uncode hizo secret codes.

Mwaka 1961 Nyirenda alipandisha bendera ya Tanganyika na mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na kupelekea kilele hicho kuitwa Uhuru Peak.

Lile lilikuwa na sura ya kusherehesha sherehe za uhuru. Tulipandisha mwenge ili umulike mpaka nje ya mipaka yetu. Tulipandisha mwenge Mlima Kilimanjaro ili ulete amani palipo na chuki, ulete tumaini pasipo na tumaini. Jiulize mwenge unawezaje kuleta amani na tumaini?

Kumbe kwenye ulimwengu wa kiroho mwenge ulikuwa na lengo la kupumbaza na kufubaza fiķra za wengi.

Wakikandamizwa waone sawa tu, wakiburuzwa na kuonewa waone sawa tu, yaani wayapuuzie matatizo yao. Kwa njia hiyo tu ndio amani na utulivu vitapatikana.

Mwaka 1964 tulipoungana na Zanzibar hatukupandisha mwenge wala bendera, Tanganyika ikafa kimyakimya.

Tumepita kwenye misukosuko ya kila namna, furaha na vicheko hatimaye umefika mwaka 2023.

Simba ambaye ni mfalme wa nyika kapanda kwenye kilele. Kaenda kuweka bendera yake nyekundu kule kileleni.

Nyirenda mwaka 1961 aliweka bendera yenye rangi ya kijani, njano na nyeusi, utawala wa twiga mnyama mrembo lakini goigoi akatawala kuanzia hapo. Wote tumesguhudia jinsi taifa letu lilivyo na watu wavivu na goigoi, hadi wawekezaji wanasema hawataki kufanya kazi na Watanzania kwani hawataki kufànya kazi kwa bidii ila wanataka wakuibie.

Kwa ujio huu mpya kiroho, uelekeo wa kitaifa unabadilika. Spirit ya mapàmbano imetamalaki.

Sasa pale kileleni ni pekundu na pana Simba mfalme wa nyika. Tutaziona rangi zote.

Mabadiliko makubwa sana yanakuja kwenye siasa zetu na uongozi kwa ujumla, mabadiliko haya mtaanza kuyaona siku sio nyingi.

Wenye macho ya rohoni tumeona.
Gwappo Mwakatobe , Mshana Jr, Pascal Mayalla , Rakims
Mabadiliko makubwa sana yanakuja kwenye siasa zetu na uongozi kwa ujumla, mabadiliko haya mtaanza kuyaona siku sio nyingi.

Wenye macho ya rohoni tumeona[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom