Elections 2010 Suala la Uraia laingia CHADEMA

Elections 2010 Suala la Uraia laingia CHADEMA

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Tovuti ya BBC Kiswahili inaripoti kuwa wakati kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania zikiwa zimeanza rasmi chama tawala nchini humo CCM kimezidi kuongeza idadi ya wabunge hata kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika.


Hayo yametokea baada ya mmoja wa waliokuwa wakiwania ubunge kupitia chama cha upinzani CHADEMA Bw Ezekiah Wenje wa jimbo la Nyamagan a mkoani Mwanza kuenguliwa kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa si r aia wa Tanzania.


Hatua hiyo inamfanya Bwana Lawrence Masha ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kupitia CCM , akipambana na Bwana Wenje kupita bila kupingwa na hivyo kusubiri kuapishwa hata ya u chaguzi wenyewe unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.


BBC Swahili - Habari - CCM chaongeza idadi ya wabunge Tanzania
 
Hivi wananchi wakimkataa mgombea pekee patakuwa na mbunge hapo ? Hawa BBC mbona wanataka kuwa presumptious na kuforce notion ya kwamba wananchi ni lazima wamchague "mgombea pekee" ?
 
kwani kwetu inajalisha umepata kura za NDIO za zaidi ya asilimia 50%
 
Lawrence Marsha ataingia Bunge lijalo kunatokana na Sheria ya Uchaguzi inayotamka sasa kwamba Mgombea asipopingwa na mgombea mwingine, anatamkwa kwamba ameshinda Uchaguzi.

Kipengele hiki cha Sheria kinastahili kurekebeshwa ili Mgombea ambaye hapingwi na Mgombea mwingine, apigiwe kura na Wapiga kura kwa kusema "NDIYO" au "HAPANA". Hasa katika jamii inayothubutu kumteka au kumzuiya Mgombea ili asiwasilishe Fomu zake kwa Msimamizi wa Uchaguzi, ni lazima wapenda demokrasia tupiganie rekebesho hilo katika Sheria ya Uchaguzi.

Kilasara:smile-big:
 
Wanaojua sheria ya uchaguzi watujuze. Mimi nakumbuka kuwa endapo mgombea ni mmoja katika nafasi hiyo, basi uchaguzi wa ndiyo au siyo haufanyiki. 'Automatically' anakuwa mshindi...
 
Lawrence Marsha ataingia Bunge lijalo kunatokana na Sheria ya Uchaguzi inayotamka sasa kwamba Mgombea asipopingwa na mgombea mwingine, anatamkwa kwamba ameshinda Uchaguzi.

Kilasara:smile-big:

kwa maana hiyo jimbo la masha na wengine waliopita bila ya kupingwa hawatapigiwa kura? kura zitakuwa za Rais tu?
 
Back
Top Bottom