Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nina tatizo la waandishi wa habari wa Tanzania - huwa hawajui kufuatilia mambo, na mara nyingi wanaishi kwa ajii ya siku iliyopo tu.
Sasa turudi kwa Waziri wetu wa Mambo ya Nje Mulamula; Mwezi August mwaka huu 2021 aliongea na waandishi wa habari kwamba kuna mwelekeo mpya kuhusu suala la uraia pacha, na kwamba kabla ya mwisho wa 2021 litakuwa limepatiwa ufumbuzi. Hivi ni waandish wangapi wamerudi kwa Malamula na kuomba mrejesho wa ahadi yake?
Je tutamlaumu Raisi Mkapa pale alipowaponda waandishi wa habari wa Tanzania?
Refer: Mwelekeo mpya kwa uraia pacha
- Kuna wakati kurugenzi ya Habari ilitangaza kwamba Chancellor wa Germany Angela Melkel kaongea na Magufuli kujenga kiwanda cha mbolea mwaka 2022. Hakuna aliyefuatilia suala hili limeishia wapi
- Kuna wakati tulisikia Mkurugenzi mmoja amemuua muumini wa Sabato kwa risasi, hakuna anaefuatilia suala hilo limeishia wapi
- Ahadi za SGR, ahadi za kutokatika umeme, ahadi za umeme wa Stiegla, ahadi za hiki na kile, bure!