Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Ila wakikaa tu home hakuna forum yoyote ya kuongelea kwa miaka mitano ndio wananchi watakuwa wamewaelewa?
 
Maana yake hapo unahalalisha uchumia tumbo sio? Wanaenda bungeni kufanya nini? Wakakae tu wasubiri posho?

Hawatakuwa na impact yoyote kwenye bunge la CCM so haitakuwa na difference yoyote kama watakuwepo au hawatakuwepo.

Labda kama unamaanisha waende kwa maslahi binafsi.
Na maslahi ya chama pia
 
"Makamanda maandazi" wa CHADEMA mnanikumbusha wakati wa tetesi za Lowassa kujiunga CHADEMA!

"Makamanda maandazi" mlikuwa mnajiapiza kama atajiunga CHADEMA mtahakikisha Mbowe anang'oka!

Baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA, kelele zote zilipotea na Mbowe mpaka leo ni mwenyekiti

Kelele nyingi, matendo zero.

Mbowe alishawajua ninyi ni debe tupu...

Wabunge CHADEMA viti maalum wataenda bungeni na hakuna lolote mtakalofanya zaidi ya kuanza kupongeza na kusema "hatuwezi kumwachia bla bla shamba peke yake". Tunaenda kubanana huko huko!

''Makamanda maandazi'' mna vituko!
 
CHADEMA ni Wabinafsi saana, ndiyo maana wanasema Chadema ni kusanyiko la Wapigaji na wanajiona wao tu wengine no that is ur stupidity
 
Wanawake wanapiginia usawa kitambo sana, kwenye hili wapewe haki ya kuamua na so kulazimishwa na watu ambao wao wamekosa kula yao.
 
IMG_0025.jpg
 
Kuna habari zinatrend mitandaoni kuwa kuna kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini linakula njama za kwenda DODOMA kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAVICHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya viti maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa na ambao tulioshuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na kwenda bungeni ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa ua machaguo ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.
Nikwambie utake usitake nyie manyumbu hamuwezi kuiangusha chadema kwa ujinga wenu, mmembana mwenyekiti kwa tundu lisu mpaka akaamua kumpistiha kisha amepata hasara.

Mnadhani tena atatumia ujinga wenu kususa vit maarumu?

Anawavutia muda tu na ndo.maana mpaka sasa hajaongea kuchunga mdomo usije mponza. Siku akiamka atamfuta Tundu umakamu na kuchagua mwingine na kuwapeleka bungeni wanawake viti maalumu kisha mta kaa chini kama bata kwa aibu nyie vibaraka wa beberu, eidha mmfuate Lisu huko na muiache Chadema iendelee.
 
Jibu ni kwamba unaelekea kuachwa kwenye mataa, alaf hakuna mamilion ya wafuas wa Chadema Kwa wanawake
 
Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowot
Hapa uhuni wa Ndugai unatoka wapi?

Kuugua muugue nyie, halafu afe mwingine??

Chadema ni Chama cha hovyo kinachokandamiza haki ya watu!

Hakuna hata vikao vilivyoamuru na kuweka msimamo wa Chama kuhusu kususia bunge hata kile cha tathimini nacho hakuna!! zaidi Sana ni watu tu wanaibukia mitandaoni kujisemea tu eti tumesusia Bunge

Tangu MM/kiti agalagazwe, hamjawahi hata kuitisha kikao, badala yake baada tu matokeo kutangazwa alikimbilia Ubalozini na hakuitisha kikao

Watu wanasubiri kikao maalumu ili waseme dukuduku Lao na misimamo Yao juu ya Hilo,Ninyi hamitishi kikao, vikao vyenu ni Mitandaoni tu na kila mtu ni msemaji

Hovyo!!!
 
Kigogo anatengeneza tsharuki hakuna kitu kama hicho.
Jamaa style yake ya kutuhumu haijakaa poa.List ya mwanzo alituma akasema wafukuzwe,jana katuma majina baadhi ya mwanzo na mengine mapya;manake hawa ambao wametolewa wangeshakuwa wamefukuzwa kama alivyokuwa anataka si ingekuwa si haki? Mimi nadhani chama makini kisideal na uzushi au fununu
 
Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Nyie watanzania hata hamfiki milioni mbili mnaweza kumtoa mtu heshima kwa watu milioni 60?
We mwenyewe hata wakikupa mchngo wa chama elfu kuminkwa mwezi.huwezi.kulipa iezi mitatu, sasa unataka chama kiendeshwe vipi?
 
Kwanza bora tuelimishane - pengine tunakosea pahala. Hivi viti maalum vinatokana na vigezo gani kwa chama husika - kutokana na idadi ya wabunge chama kilichopata ktk uchaguzi, au kutokana na idadi ya kura za mgombea urais alizopata mgombea wa chama husika?
Nadhani sheria lazima itakuwa wazi ktk hili na mwenye kufahamu twaomba atuwekee hapa kipengele/vipengele husika.
 
Mpango wowote wa kupeleka wabunge viti maalum bungeni,utaiathiri pakubwa chama kikuu CHADEMA kwa kuwa watakua wamekubali kuwa Uchaguzi ulikua huru, Chama kikuu kineyakataa matokeo ya uchaguzi wote kitendo cha kukubali kupeleka wabunge viti maalum Bungeni ni kukubaliana na dhulma zilizofanyika katika uchaguzi.
 
Kuna watu kawataja kwenye ile orodha wamekanusha, na mimi nimeongea na mojawapo pia kakanusha juu ya hilo.
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
 
Back
Top Bottom