Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Ila wakikaa tu home hakuna forum yoyote ya kuongelea kwa miaka mitano ndio wananchi watakuwa wamewaelewa?
 
Na maslahi ya chama pia
 
"Makamanda maandazi" wa CHADEMA mnanikumbusha wakati wa tetesi za Lowassa kujiunga CHADEMA!

"Makamanda maandazi" mlikuwa mnajiapiza kama atajiunga CHADEMA mtahakikisha Mbowe anang'oka!

Baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA, kelele zote zilipotea na Mbowe mpaka leo ni mwenyekiti

Kelele nyingi, matendo zero.

Mbowe alishawajua ninyi ni debe tupu...

Wabunge CHADEMA viti maalum wataenda bungeni na hakuna lolote mtakalofanya zaidi ya kuanza kupongeza na kusema "hatuwezi kumwachia bla bla shamba peke yake". Tunaenda kubanana huko huko!

''Makamanda maandazi'' mna vituko!
 
CHADEMA ni Wabinafsi saana, ndiyo maana wanasema Chadema ni kusanyiko la Wapigaji na wanajiona wao tu wengine no that is ur stupidity
 
Wanawake wanapiginia usawa kitambo sana, kwenye hili wapewe haki ya kuamua na so kulazimishwa na watu ambao wao wamekosa kula yao.
 
Nikwambie utake usitake nyie manyumbu hamuwezi kuiangusha chadema kwa ujinga wenu, mmembana mwenyekiti kwa tundu lisu mpaka akaamua kumpistiha kisha amepata hasara.

Mnadhani tena atatumia ujinga wenu kususa vit maarumu?

Anawavutia muda tu na ndo.maana mpaka sasa hajaongea kuchunga mdomo usije mponza. Siku akiamka atamfuta Tundu umakamu na kuchagua mwingine na kuwapeleka bungeni wanawake viti maalumu kisha mta kaa chini kama bata kwa aibu nyie vibaraka wa beberu, eidha mmfuate Lisu huko na muiache Chadema iendelee.
 
Jibu ni kwamba unaelekea kuachwa kwenye mataa, alaf hakuna mamilion ya wafuas wa Chadema Kwa wanawake
 
Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowot
Hapa uhuni wa Ndugai unatoka wapi?

Kuugua muugue nyie, halafu afe mwingine??

Chadema ni Chama cha hovyo kinachokandamiza haki ya watu!

Hakuna hata vikao vilivyoamuru na kuweka msimamo wa Chama kuhusu kususia bunge hata kile cha tathimini nacho hakuna!! zaidi Sana ni watu tu wanaibukia mitandaoni kujisemea tu eti tumesusia Bunge

Tangu MM/kiti agalagazwe, hamjawahi hata kuitisha kikao, badala yake baada tu matokeo kutangazwa alikimbilia Ubalozini na hakuitisha kikao

Watu wanasubiri kikao maalumu ili waseme dukuduku Lao na misimamo Yao juu ya Hilo,Ninyi hamitishi kikao, vikao vyenu ni Mitandaoni tu na kila mtu ni msemaji

Hovyo!!!
 
Kigogo anatengeneza tsharuki hakuna kitu kama hicho.
Jamaa style yake ya kutuhumu haijakaa poa.List ya mwanzo alituma akasema wafukuzwe,jana katuma majina baadhi ya mwanzo na mengine mapya;manake hawa ambao wametolewa wangeshakuwa wamefukuzwa kama alivyokuwa anataka si ingekuwa si haki? Mimi nadhani chama makini kisideal na uzushi au fununu
 
Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Nyie watanzania hata hamfiki milioni mbili mnaweza kumtoa mtu heshima kwa watu milioni 60?
We mwenyewe hata wakikupa mchngo wa chama elfu kuminkwa mwezi.huwezi.kulipa iezi mitatu, sasa unataka chama kiendeshwe vipi?
 
Kwanza bora tuelimishane - pengine tunakosea pahala. Hivi viti maalum vinatokana na vigezo gani kwa chama husika - kutokana na idadi ya wabunge chama kilichopata ktk uchaguzi, au kutokana na idadi ya kura za mgombea urais alizopata mgombea wa chama husika?
Nadhani sheria lazima itakuwa wazi ktk hili na mwenye kufahamu twaomba atuwekee hapa kipengele/vipengele husika.
 
Mpango wowote wa kupeleka wabunge viti maalum bungeni,utaiathiri pakubwa chama kikuu CHADEMA kwa kuwa watakua wamekubali kuwa Uchaguzi ulikua huru, Chama kikuu kineyakataa matokeo ya uchaguzi wote kitendo cha kukubali kupeleka wabunge viti maalum Bungeni ni kukubaliana na dhulma zilizofanyika katika uchaguzi.
 
Kuna watu kawataja kwenye ile orodha wamekanusha, na mimi nimeongea na mojawapo pia kakanusha juu ya hilo.
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…