Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Ikiwa hilo litatokea itakuwa ni ushahidi tosha wa kuthibitisha walichokuwa wanapigania sio maslahi ya wananchi bali ni maslahi yao wenyewe na sasa inadhihirika wazi wana njaa kali
Njaa iko wapi?!!!
Yaani mh.Dada mkubwa Hallima Mdee na wengine wote wana njaa?!!

Hivi unajua kuwa mwanajeshi mwenye CHEO KIKUBWA anapostaafu... huwa "hanyongi" zaidi ya 300M na gari moja la kifahari...?!!

Leo mbunge anamaliza miaka 5...kiinua mgongo bila ya kuchelewa kukipata "anafukia mfukoni" si chini ya 300M....
Kumbuka ndani ya hiyo miaka 5 amejikusanyia chini kidogo ya 1.0Billion....

Acha kabisa MASKHARA na kazi ya UBUNGE...hawana NJAA hawana NJAA hawana NJAA...

Kikubwa kwangu waendelee KUPEWA STAHIKI ZAO kwani wanastahili....cha mno tu WAKATUWAKILISHE VYEMA BUNGENI.....

#NINAWAUNGA MKONO AKINA HALIMA JAMES MDEE NA BAWACHA KWENDA BUNGENI KUAPA.
 
Uhalali haudhihirishwi kwa kuwakataza viti maalum kwenda bungeni, kwahiyo hata huyo aliechaguliwa kwa kura nae hakushinda?
Yawezekana akushinda pia, kwani kilichoamuwa mbunge kutangazwa si kupata kura nyingi.
 
Kila chama kinataratibu na sheria zake na kiuhalisia wanachama wanawajibika kuzifuata, ukienda tofauti utawajibishwa na ikiwezekana unafutwa uanachama. Sasa tulishihudia wakati wa uteuzi wa mgombea wa nafasi ya uraisi kwa upande wa ccm kuna walioonyesha nia ya kugombea na kisheria walikuwa sawa lakini wakashughulikiwa mpaka wengine kujitoa na kuhamia vyama vingine; tulitegemea watu kupaza sauti hiki kitu kisifanywe kihuni lakini watu kwa unafiki walikaa kimya.
Sasa turudi kwa hili la chadema haiwezekani na haitokaa kuwezekana mtu kujipeleka bungeni ili kuapishwa bila kupelekwa jina lake na uongozi wa chama kwa kufuata taratibu, na itakuwa halali kabisa kuwafuta uanachama kama watafanya ivyo. KAMA SPIKA ATAWAAPISHA HAO WALIOJIPELEKA KIHUNI, ATATAKIWA KUHOJIWA HAYO MAMLAKA YA KUAPISHA MTU ALIYEJIPELEKA MWENYEWE KAYATOA WAPI?? Na kwa hili chadema wakikaa kimya itakuwa lao moja na ccm.
 
Suala la viti maalum limeshakwisha na majina yamekwenda na wataapishwa

Mm Nampa hongera Sana halima Mdee amefanya kitu kikubwa Sana yy kama Kiongozi wa wanawake

Hizo nafasi ni zao kisheria, Sasa why wasuse?

Kama ni malalamiko ya uchaguzi miaka yote yapo na wao walikuwa wanaenda bungeni Sasa why Leo wasiende?

Hakuna mpasuko wowote ambao utatokea coz viongozi wakubwa wote wanajua na hakuna Kiongozi yoyote wa ccm aliewashawishi
Kukujibu hapo pekundu, ni kwa vile wakubwa akina Mbowe nk hawapo Bungeni. Kungekuwa na viti maalum vya wanaume wasingesusia. Ni UBINAFSI unawasumbua.

Kwa mtu mwenye busara angepeleka hao 19 wakawasumbue wabunge wa CCM kwa kujenga hoja mjarabu
 
Kunywa soda nakuja kulipa hahaha
Umeongea point tupu
 
BAWACHA jiongezeni, nendeni bungeni kwa zile nafasi 19

Mtakuja juta siku nyie mnakataa hizi nafasi halafu viongozi wenu wanakuja kuteuliwa na rais kwa kazi ndogo ndogo wanakubali

Za kuambiwa changanya na zako - Jakaya Kikwete

Msije kusema hatukuwashauri hili 😂😂😂
Kwa kweli kama kuna ushauri feki kutokea hapa Tanzania ni huu ambao umesimama kwa kigezo cha hamsini kwa hamsini isiyokuwa na meno yenye kila dalili la kufikiria posho tu na si kuhudumia wenye nchi bunge la kumpigia makofi ndugai na tulia daima siyo bunge halali bali lipo kwa maslahi ya chama cha mapinduzi pekee na si vinginevyo.
 
Mimi Sina mume labda tumupeleke babako asiyesimamisha viti maalumu maana ni useless and functionless. Mfyuuu
hawala wa mamako alikosea kumwaga upako kwa mamio ndo ukatotolewa kifutu wewe💩💩💩
 
BAWACHA jiongezeni, nendeni bungeni kwa zile nafasi 19

Mtakuja juta siku nyie mnakataa hizi nafasi halafu viongozi wenu wanakuja kuteuliwa na rais kwa kazi ndogo ndogo wanakubali

Za kuambiwa changanya na zako - Jakaya Kikwete

Msije kusema hatukuwashauri hili [emoji23][emoji23][emoji23]
Ulivyomaliza kwa kicheko unaanisha ushauri wako ni kejeli tu. Unawapotosha wenzio.....
 
hawala wa mamako alikosea kumwaga upako kwa mamio ndo ukatotolewa kifutu wewe[emoji90][emoji90][emoji90]
Kubwa jinga wewe na matusi yako nakuweka ignore list,naona umevurugwa mfyuuu, go to hell [emoji48] and byee
Member mzee humu JF hujiheshimu
 
Suala la viti maalum limeshakwisha na majina yamekwenda na wataapishwa

Mm Nampa hongera Sana halima Mdee amefanya kitu kikubwa Sana yy kama Kiongozi wa wanawake

Hizo nafasi ni zao kisheria, Sasa why wasuse?

Kama ni malalamiko ya uchaguzi miaka yote yapo na wao walikuwa wanaenda bungeni Sasa why Leo wasiende?

Hakuna mpasuko wowote ambao utatokea coz viongozi wakubwa wote wanajua na hakuna Kiongozi yoyote wa ccm aliewashawishi
Wanaccm tupo busy kuwashauri watu wasio taka Maendeleo nchi waingie Bungeni duujj BASI WANACCM SISI NI MIJINGA
 
Wataendaje wakati Chama Kimekataa Uchaguzi Haukufanyika na Hivyo Hakuna Kushiriki Mambo yote yausuyo kilichotokana na uchaguzi huo...
Kusema uchaguzi haukufanyika ni jaribio la kutaka kusema kwamba waliokuwa wabunge bunge la 11 waendelee mpaka uchaguzi mpya utakapofanyika ikimaaanisha kuwa Mbowe et al watarudi bungeni- jamani kushindwa kubaya
 
Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini linakula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAVICHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya viti maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa na ambao tulioshuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na kwenda bungeni ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa ua machaguo ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.

Waache tu wawe huru kuamua lifaalo machoni pao.Itatusaidia kujua kwamba wapo kwa ajili ya taifa au maslahi yao binafsi.Hata hivyo ni jambo la hatari kuishi na jini-malaika.
 
Nawaunga mkono hao kina Mama kwani angekuwa Mbowe au Lissu ndiyo kachaguliwa asingekataa kwenda kula kiapo Dodoma, njaa si mchezo jamani. Nyie kina Mama nendeni tu kula kiapo, wengine mna watoto na hata kama hamna mna washikaji wa kuwatunza.
 
Ubunge ni kwa kibali cha chama siyo kibali cha mtu binafsi, huwezi kujipeleka wewe binafsi kula kiapo cha ubunge viti maalum bila jina lako kupitishwa na vikao vya chama!
 
Back
Top Bottom