Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini kula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya Bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya Viti Maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa wizi ambao tulishuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa dhidi ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.

Wizi wa kura kama huu hapa chini, utakubalije uchaguzi wa aina hii?

View attachment 1633707
Wenye tulishauona siku nyingi ibabaishaji na usanii wa wahuni wachache ndani ya Chadema wakiongozwa na TUNDU. Anasingizia kuibiwa kura, huyo hata kwenye ubungebtu asingeshinda safari hii sembuse Urais wa JMT.

MTAUMIA BURE NA ROHO ZENU NA BADO KAZI INAENDELEA
 
Mchezo huu unachezwa na Mbowe. Mbowe hawezi kuacha ruzuku, piga ua garagaza. Akina mnyika wakifanya mchezo mbele ya ruzuku watafukuzwa. Take my words.
 
BAWACHA jiongezeni, nendeni bungeni kwa zile nafasi 19

Mtakuja juta siku nyie mnakataa hizi nafasi halafu viongozi wenu wanakuja kuteuliwa na rais kwa kazi ndogo ndogo wanakubali

Za kuambiwa changanya na zako - Jakaya Kikwete

Msije kusema hatukuwashauri hili [emoji23][emoji23][emoji23]
Wamesikiliza ushauri wako
 
Kuna dalili zote mleta mada kachana kadi yaje ya chadema! Unaweka uso wapi sasa. Mliambiwa Tanzania kwanza vyama baadaye ninyi mkanga'ania vyama! Hata hivyo, nawapongeza viongozi wa Chadema amabao wameona umuhimu wa kuwaruhusu wanachama wao kuwakilisha huko bungeni kwa mujibu wa sheria zilizopo.
 
Mkuu mimi niko upande wa haki, si mwanachama wa Chadema,

Ila swali langu katiba ya Chadema inasema nini katika hili? Tuweke ushabiki pembeni.
Sijui katiba ya CDM ilw wengi wanasema
Mdee hakupaswa kuwemo

Kawemo
 
Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini kula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya Bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya Viti Maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa wizi ambao tulishuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa dhidi ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.

Wizi wa kura kama huu hapa chini, utakubalije uchaguzi wa aina hii?

View attachment 1633707
NJAA HAINA BAUNZA, MJOMDA
 
Walijulikana mapema ,muda si mlefu watafukuzwa chama ,vizuri wapo wengi na wenye misimamo mikali kuliko wao,waende huko kutumwa na kuzomewa na kuendeleza biashala.
 
Back
Top Bottom