Suala la Wakimbizi wa Ukraine: Ubaguzi wa rangi wa wazungu umekuwa dhahiri

Suala la Wakimbizi wa Ukraine: Ubaguzi wa rangi wa wazungu umekuwa dhahiri

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Tatizo la wakimbizi halijaanza Leo wala halijaanzia kwa wakimbizi wa Ukraine!

Wanavyofanyiwa kwa uungwana wakimbizi wa Ukraine na mataifa ya ulaya ni jambo zuri sana! Swali ni je kwa nini wakimbizi wengine waliokuwa wanakimbilia ulaya toka nchi za mashariki ya kati na afrika ya kaskazini hawakuwa wakipokelewa kwa uungwana hivyo!

Hawa wa ulaya wanakaribishwa kabisa majumbani mwa watu, wanapewa social security na wanaruhusiwa kufanya kazi!

Wale wa kiarabu na kiafrika kwanza walikuwa wakilazimisha tu, na wengi wamefia mipakani au baharini! Hawakuwa wanakaribishwa majumbani hata kidogo!

Hii ni uthibitisho kuwa wazungu wana ubaguzi wa rangi wa kutisha! Hawatuoni sisi kama binadamu sawa na wao!!

Ukiona mzungu anajivuta kwako ujue ni kwa maslahi yake tu!

INAKERA!!
 

 
mzungu ntu mbad sana kwenye races,wonderful enough wakija bara jeusi shobo kibao tunakataana mpaka wenyew .
 
Jirani ni jirani tu mkuu, na poland ni wa-europe wenzao,sasa mkimbizi wa africa kukimbilia ulaya wapi na wapi,mtu wa SUDAN anataka kukimbilia ukimbizi US badala ya Kenya majirani zao mapenzi hayo yanakujaje 🤣 🤣

Ni kweli, akina Lema na Wenje wangepaswa kukimbilia Kenya au Uganda au Rwanda na Burundi kwa majirani zetu wapendwa!
 
mnawaita makafir hlf mkiuana mnataka kukimbiria kwa makafir mnaacha kwenda pepon kwa wavaa vipedo wenzenu
Wewe hata uwe atheist au unachangia damu na yesu au ndugu wa muhamad kama ni mweusi ni mweusi tu.
Mweusi ni mweusi tu kwa mzungu, considering wengi hawajali kuhusu maswala ya dini.

Africa dini ndio deal kubwa na ndio maana tunakuta watu kama wewe.
 
Hilo suala la ubaguzi wa rangi kwa wakimbizi kutoka katika maeneo uliyoyataja bado linahitaji ulitolee ufafanuzi wa kutosha. Hivyo, naweza kusema kuwa sikubaliani na hoja yako kwa 100%.

Kwa sababu hoja au mada yako haina details, mchangiaji yeyote makini atahitaji kwanza kufanya utafiti hasa wa kubaini taratibu zinazotumika kuwapokea wakimbizi katika mataifa hayo. Mataifa mengi yanayopokea wakimbizi yana sera maalumu zinazoweka utaratibu wa utekelezaji wa suala hilo.

Je, hao wakimbizi unaosema wamebaguliwa, ni wakimbizi wa aina gani hasa? Maana kuna wakimbizi wa aina nyingi. Wanaingia katika mataifa husika kwa utaratibu gani? Sheria za mataifa hayo zinasemaje kuhusu wakimbizi wa makundi mbalimbali.

Ni viashiria gani ambavyo vinaweza kuthibitisha kuwa wamefanyiwa ubaguzi wa rangi specifically na sio ubaguzi wa aina nyingine? Maana kuna ubaguzi wa aina nyingi. Ubaguzi huo unafanywa na nani hasa? Raia wa kawaida ama ni ubaguzi wa rangi wa kitaasisi, ama wa kiserikali?

Haya ni mambo machache tu ambayo yangepaswa kutolewa ufafanuzi kwenye hoja yako.
 
Warusi sio wabaguzi! Wanatupenda sana sisi ngozi nyeusi Ndio maana upo busy kuanzisha thread humu kuwaunga mkono
 
Utasikia mbuzi moja toka Namanyele huko inasema "pray for nn sijui"

wapigane tu mpaka akili ziwakae Sawa wote.

mzungu ni mzungu tu .....mbaguzi in nature
 
Jirani ni jirani tu mkuu, na poland ni wa-europe wenzao,sasa mkimbizi wa africa kukimbilia ulaya wapi na wapi,mtu wa SUDAN anataka kukimbilia ukimbizi US badala ya Kenya majirani zao mapenzi hayo yanakujaje 🤣 🤣
Mkimbizi si mjinga sana kiasi cha kutokujua kabisa mahali penye stability na ubora wa maisha. Asijekimbilia mahali ambapo atakutana na matatizo yaleyale aliyoyaacha huko alikopakimbia.

Hata hivyo, nchi kadhaa barani Afrika zimetoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka katika nchi zingine za ndani ya bara hilo. Inategemeana na aina ya wakimbizi. Wapo wale ambao watahitaji kwenda mbali zaidi na mahali walikotoka, kutokana na sababu mbalimbali.
 
Back
Top Bottom