Suala la Wamachinga limefika Pabaya

Suala la Wamachinga limefika Pabaya

Comrade Magufuli aliwaambia kuwa wafanye biashara popote pale,wao ndiyo wapiga kura wake,na wao ndiyo wanyonge wa nchi hii
Kwahiyo hakuna mwenye mamlaka ya kufuta agizo la Rais kama sio Rais mwenyewe. SSH alisema 'wapangwe vizuri hapo walipo'!
What an ambiguity!
Wapangwe vizuri barabarani?
Wapangwe vizuri mbele ya maduka?
Wapangwe vizuri miferejini?

Tumefika mahali kazi za serikali zifanywe na Serikali. Tuachane na porojo kwamba Rais anatoa fedha kwa kila kazi ya serikali.

Vinginevyo mambo yakiharibika alaumiwe Rais?
 
watu wenye akili wanapaswa kujiuliza Umachinga ni nini. Is it a thing to be encouraged to grow or demise.
Kwa nini tunataka kuifanya jamii iiamini na kujichagulia umachinnga kama shughuli muimu ya kiuchumi? kila shughuli ya uchumi ni lazima iwe na mahali panapokubalika; sasa ni mahali gani umachinga unafanyika na jel, ni sahihi"
 
wapangwe viizuri mijini kwa kupewa maeneo mengine
 
Kama wanauza vitu halali waachwe.wewe unayesema wanachafua mazingira.nadhani huifaham njaa.wala hujui taabu.kama Mungu amekujaalia Neema hiyo ni bora kukaa kimya kuliko kuchangia kwa mihenko pasi na kuangalia ni madhara gani watakumbana nayo.mana wengi wao ni wanafamilia.na wanasomesha dhen ukija kufanikiwa unasema machinga ni takataka.,ingali mzazi wako alikusomesha kupitia umachinga.,tuwe na akiba ya maneno..Mm sio machinga ila nafarijika nikiwaona wanaposaka Riziki zao kwenye jua Kali pasi na kukata tamaa
 
K
Kama kaawaida kuna ambao wanataka kutumia huu kama mtaji wa kisiasa. Wamachinga walikuwa bad handled before tusiendelee kukosea.

Hakuna Jiji au Mji ambao hauna mipango au utaratibu. Kuwaacha tu wakae au wafanyanye watakavyo si sahihi. Mnaopiga kelele hebu ruhusuni waje waweke nyumbani kwenu hayo mabanda tuone mlivyo na uchungu.

Haiwezekani waweke mabanda hadi kwenye mitaro au barabarani wakiuza kwa kuchuuza bidhaa za watu madukani ambako sasa wanunuaji hawaendi.

Kuna jengo la machinga complex...halina watu....but pia serikali itenge sehemu ambayo mar hing guys watakuwepo. Tukishindwa kujipanga tunajipanga kushindwa.

Wanasiasa wasio na hoja wanataka watumia machinga kama mtaji kwao.mimi hili nakataa....wamachinga waelekezwe au waandaliwe eneo mahsusi ambo watakuwepo. But si kuweka biashara zao popote watakapo.

Kama tunasema wengi ni degree holders bas naamini watakuwa waelewa sana na kuelewa suala la mipango miji lilivyo. Maana hao wana uelewa na wanafahamu au wanaweza kuelekezwa sheria wakazielewa.
Kwanini machinga waone wao wanaonewa tena leo,kwanini hawakuuona uonevu wa waziwazi kwa wenyemawazo mandala na sirikali,aka wapinzani.Leo ndio wanatambua kama walidanganywa wao ni kuni maalumu lisilo gusika?
 
Kama kaawaida kuna ambao wanataka kutumia huu kama mtaji wa kisiasa. Wamachinga walikuwa bad handled before tusiendelee kukosea.

Hakuna Jiji au Mji ambao hauna mipango au utaratibu. Kuwaacha tu wakae au wafanyanye watakavyo si sahihi. Mnaopiga kelele hebu ruhusuni waje waweke nyumbani kwenu hayo mabanda tuone mlivyo na uchungu.

Haiwezekani waweke mabanda hadi kwenye mitaro au barabarani wakiuza kwa kuchuuza bidhaa za watu madukani ambako sasa wanunuaji hawaendi.

Kuna jengo la machinga complex...halina watu....but pia serikali itenge sehemu ambayo mar hing guys watakuwepo. Tukishindwa kujipanga tunajipanga kushindwa.

Wanasiasa wasio na hoja wanataka watumia machinga kama mtaji kwao.mimi hili nakataa....wamachinga waelekezwe au waandaliwe eneo mahsusi ambo watakuwepo. But si kuweka biashara zao popote watakapo.

Kama tunasema wengi ni degree holders bas naamini watakuwa waelewa sana na kuelewa suala la mipango miji lilivyo. Maana hao wana uelewa na wanafahamu au wanaweza kuelekezwa sheria wakazielewa.
Mkuu machinga Hana kosa, wakulaumiwa ni yule aliyewapa uhalali wa kuweka vibanda mpaka kwenye milango ya maduka kwa kigezo cha kwamba wao ndio waliompigia Kura, na ili kuhalalisha aka waletea na vitambulisho kwa malipo 20000, kwahiyo wakati tunatazama kelo zinazo sababishwa na machinga ni muhimu pia tukatazama ninani aliye wapa uhalali Wakuchafuwa majiji namna hii, nionavyo mimi hawa machinga wanatumika kama mtaji kwa wanasia Kisha baada ya hapo wanatoswa kama Ganda LA muwa, ni nafasi nzuri sasa kwa machinga ya kujitathimini upya na kujuwa wao nikina nani na wanapaswa wafanye nini

Baati nzuri msimu wamvuwa Ndokwanza inaanza
 
Machinga wathibitiwe kwanza ni wakwepa kodi na wengi wao wanamitaji mikubwa tu
 
Bila kuwapa alternative ya wapi wafanyie shughuli zao kuwatoa ni kutengeneza crisis ya kijamii.
No alternative no removal, hii nchi yetu sote, hata kama wananchi wataamua kuuza maandazi kwenye geti la Ikulu waache, hii ni nchi yao!
 
Kama wanauza vitu halali waachwe.wewe unayesema wanachafua mazingira.nadhani huifaham njaa.wala hujui taabu.kama Mungu amekujaalia Neema hiyo ni bora kukaa kimya kuliko kuchangia kwa mihenko pasi na kuangalia ni madhara gani watakumbana nayo.mana wengi wao ni wanafamilia.na wanasomesha dhen ukija kufanikiwa unasema machinga ni takataka.,ingali mzazi wako alikusomesha kupitia umachinga.,tuwe na akiba ya maneno..Mm sio machinga ila nafarijika nikiwaona wanaposaka Riziki zao kwenye jua Kali pasi na kukata tamaa
... CHOCHOTE kinaweza kufanyika POPOTE alimradi ni HALALI chief? Au nimekuelewa tofauti?
 
Hakuna ustaarabu Kwa machinga nguvu tu itumike. Hakuna kuchekacheka Na machinga ni nyani hao
 
Kama wanauza vitu halali waachwe.wewe unayesema wanachafua mazingira.nadhani huifaham njaa.wala hujui taabu.kama Mungu amekujaalia Neema hiyo ni bora kukaa kimya kuliko kuchangia kwa mihenko pasi na kuangalia ni madhara gani watakumbana nayo.mana wengi wao ni wanafamilia.na wanasomesha dhen ukija kufanikiwa unasema machinga ni takataka.,ingali mzazi wako alikusomesha kupitia umachinga.,tuwe na akiba ya maneno..Mm sio machinga ila nafarijika nikiwaona wanaposaka Riziki zao kwenye jua Kali pasi na kukata tamaa
nadhani wanaolalamikiwa ni wale wanaokaaa mbele ya biashara za watu
 
Kuna sehemu unachanganya
Umesema machinga wanachukua vitu madukani wanapanga chini, hivyo wsteja hawaendi tena madukani.
Sasa hao wa madukani vitu vyao si vinanunuliww na machinga au?
Hawa machinga hawatoi mizigo yao China, Bali wananunua hapohao kwa wenye maduka. Iweje tena mnasema wenye maduka wanalalamika?
 
Kama wewe ni mtu wa mshahara huwezi kilielewa mapema, Hawa machinga Mahal wanakopanga bidhaa zao, ni kinyime na sheria taratibu za mipango miji.

Wewe binafsi pamoja na wote ni watanzania, huwezi kuruhusu mtu akaja kulima na kuvuna katika shamba lako ambalo unalihudumia wewe, Angalia mbele ya maduka ya watu wanaolipa mamilion ya shilingi kama kodi. Halafu machinga afanyie biashara hapo mbele ya duka lako na halipi hata sumni.

Machinga wataondoka barabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... sio mbele ya biashara za watu tu mkuu; kuna baadhi ya maeneo wameziba kabisa barabara za waenda kwa miguu hivyo kulazimisha waenda wa miguu kutembea kwenye lami hvyo kupelekea barabara za magari badala ya njia mbili kuwa njia moja; do you know what next? Foleni zisizoisha!

Kuna siku nilikatiza maeneo ya Mbezi Luis kuna hii njia mpya kama unatokea Kimara unachepuka kushoto kuelekea Kinyerezi; pale baada ya round about ya kwanza unapoingia kushoto kuacha njia ya kupanda kilima kuelekea stendi ya juu, njia yote hadi round about ya mbele kabisa kule kuelekea Malamba, machinga wamejimegea nusu.

Kuna mmoja just before njia ya kuingia CRDB Bank siku hiyo alikuwa kaweka kabisa kitoroli anauza viazi na mihogo ya kuchoma katikati ya barabara hivyo magari kulazimika kusubiriana simply kuna machinga anauza mihogo barabarani! Trafiki walikuwa wanajitahdi sana kuongoza magari ila kutokana na ufinyu wa njia magari yakawa hayaendi.

You know what, suala la machinga barabarani linatuathiri zaidi sisi akina kapuku kuliko kinyume chake. Imagine watu mmejazana kwenye daladala gari haziendi upumuaji shida, migongo inauma, barabarani waenda kwa miguu wamezibiwa njia, n.k. Suala la machinga ni kero kwa kila mtu labda kwa hao wanaofaidika na umachinga yaani wamachinga wenyewe!
 
Kuna sehemu unachanganya
Umesema machinga wanachukua vitu madukani wanapanga chini, hivyo wsteja hawaendi tena madukani.
Sasa hao wa madukani vitu vyao si vinanunuliww na machinga au?
Hawa machinga hawatoi mizigo yao China, Bali wananunua hapohao kwa wenye maduka. Iweje tena mnasema wenye maduka wanalalamika?
... hawanunui kutoka kila duka bali kwa wenye maduka ma-agent wakubwa wachache ambako hata wenye maduka madogo (ambao ndio wengi) nao hununua ambao, in turn, huzibiwa biashara zao na machinga.
 
Kuna msemo unasema "mipango bila utekelezaji ni uzembe na utekelezaji bila mipango ni vulugu" ni kweli watanzania tunahitaji tupate riziki zetu kupitia shughuli ndogo ndogo kama huu uchuuzi(umachinga) kilimo cha kujikimu n.k lakn kwenye suala hili la umachinga tukiangalia kwa jicho la mbali lazima tulikuwa naenda kugonga ukuta, huwezi kuruhusu kila eneo kuweka biashara, mbele ya ubalozi biashara, mbele ya ikulu biashara,. mbele hospital biashara hata kama ni unyonge hii imezidi, lazima tuelekee kugonga ukuta, hatuwezi kurithisha taifa lisilokuwa na mpangilio wa maeneo ya makazi, kilimo, viwanda, biashara n.k vinginevyo miji yetu itakuwa ya ajabu ajabu tu hapa duniani
 
Kama wewe ni mtu wa mshahara huwezi kilielewa mapema, Hawa machinga Mahal wanakopanga bidhaa zao, ni kinyime na sheria taratibu za mipango miji.

Wewe binafsi pamoja na wote ni watanzania, huwezi kuruhusu mtu akaja kulima na kuvuna katika shamba lako ambalo unalihudumia wewe, Angalia mbele ya maduka ya watu wanaolipa mamilion ya shilingi kama kodi. Halafu machinga afanyie biashara hapo mbele ya duka lako na halipi hata sumni.

Machinga wataondoka barabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
... umenena vyema! Kama vipi sheria zirekebishwe ili kurasimisha umachinga ni mahali popote kwa sababu nao wanajipatia kipato, ni wapiga kura, na wana familia (as if hao wanaozibiwa biashara zao na wanalipa mamilioni ya kodi hawana familia).
 
Back
Top Bottom