Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Ya shilingi elfu kumi kwa kila laki moja ninayompatia. Unataka?Unawakopesha kwa riba ya asilimia ngapi?
Maana wakopeshaji mnasababisha wastaafu kufariki mnapuna pesa zao nyingi kwa riba nyongajiYa shilingi elfu kumi kwa kila laki moja ninayompatia. Unataka?
Unakuta mstaafu kaacha ATM card na namba za siri kwa mkopeshaji mzigo ukitoka jamaa anachana tu ATM card anatoa fedha mstaafu anaambulia kiduchu huu ni utakatishaji.Tueleze jina lako na unapatikana wapi tukushitaki kwa ile kesi isiyo na dhamana
Hili wanalo sana waalimu vijijini aisee hadi huruma.Unakuta mstaafu kaacha ATM card na namba za siri kwa mkopeshaji mzigo ukitoka jamaa anachana tu ATM card anatoa fedha mstaafu anaambulia kiduchu huu ni utakatishaji.
Kipato duni cha walimu fursa kwa wakopeshaji, riba wanagonga mpaka 50%Hivi hao wastaafu mnaowasema wanakopeshwa kwa lazma au wanaenda wenyewe? Kwanza hao ni wasomi mfano walimu kwanini wasitumie akil zao kujua kwamba hizo hela znariba kubwa? Vile vile mabenki mbona yanatoa mikopo ya wastaafu kwa riba ndogo kabisa kwann wasiende huko wahangaike na hela za moto? Hapa kuna tatizo kwenye wasomi wetu pili kuna tatizi kubwa kwenye serikali coz kwa nn mtu aliyetumikia taifa kwa miaka pengne zaidi ya 30 na baada ya kustaafu ashindwe kununua hata ndala
Sent using Jamii Forums mobile app
Naitwa Tila Lila napatikana Idukilo huku Kishapu Shinyanga. Nikishtakiwa wanaIdukilo wataandamana na mtawapiga marungu kwa sababu sijagombana nao na tunasaidiana sanaTueleze jina lako na unapatikana wapi tukushitaki kwa ile kesi isiyo na dhamana
Mbaya sana! Mie nafuu sana. Na wengine wakikwama sana wananirudishia tu bila riba yeyeote.Kina nyangole hapo tabora hadi asilimia 40!mateso kwa watumishi wa umma!!!
Ukimaliza kumlaumu yeye sasa hamia kwa Wanaokopa nao uwalaumu na uwapatie ushauri mbadala nini cha kufanya.Maana wakopeshaji mnasababisha wastaafu kufariki mnapuna pesa zao nyingi kwa riba nyongaji
Eti bhana!Ukimaliza kumlaumu yeye sasa hamia kwa Wanaokopa nao uwalaumu na uwapatie ushauri mbadala nini cha kufanya.
Upo huko nini mkuu - kwa maana unatuletea stori za jikoni kabisa!Ila muwe na subira kwa sababu kuna juhudi zinaonekana tayari zinafanyika, soon kila kitu kitakuwa sawa.
Wale waliotajwa na msiba kumkwamisha Mkuu wameshaanza kushughulikiwa.
Wameshaitwa kwenye kamati ya Mzee Filipu mambo yatanyooka mpaka mtashangaa...sio mikopo ya Wanafunzi, pensheni, ajira zitakuwa nje nje.
Kwa kifupi tunasema yajayo yanafurahisha.