Suala la wastaafu kutolipwa kiinua mgongo(Pensheni) kwa wakati

Suala la wastaafu kutolipwa kiinua mgongo(Pensheni) kwa wakati

Upo huko nini mkuu - kwa maana unatuletea stori za jikoni kabisa!
Mimi nina kawaida ya kuwaamini sana Viongozi, huwa nawahesabu wao kama Manabii, hivyo wasemacho ni ukweli.

Kuna kipindi niliona kama serikali imekwama kwenye suala la ajira, mafao, mikopo kwa Wanafunzi, kuzidi kunenepa kwa deni la taifa n.k...lakini msiba (ambaye naamini naye pia ni kiongozi) alipoitisha press akawataja wanaomkwamisha Mkuu nikafarijika sana...maana huku kwetu kuna msemo 'kujua tatizo ni nusu ya kulitatua'

Mimi mwenyewe napumulia mashine ila nina imani muda si muda mambo yanaenda kuwa sawa.
 
Katika biashara yangu ya ujasiriamali nimetokea kuwakopesha sana walimu na hivi karibuni nilikopesha walimu wanaokaribia kustaafu na wamekuwa wanastaafu lkn hawalipi rejesho. Sasa katika hawa niliowakopesha nimewauliza mbona Rais aliwahi kutoa maelekezo penshni zisichelewe inakuwaje?
Majibu yao sasa - Rais ndiyo kasababisha hatulipwi na tena wanadai hali ilivyo waliostaafu kuanzia Mwezi wa Saba Mwaka jana hawatalipwa kwa sababu fedha zinatumika kwenye uchaguzi na Serikali haina fedha.
Sasa hayo sijui ni ya ukweli?

Je ktk biashara yako hiyo,unalipa kodi ya serikali?
 
Katika biashara yangu ya ujasiriamali nimetokea kuwakopesha sana walimu na hivi karibuni nilikopesha walimu wanaokaribia kustaafu na wamekuwa wanastaafu lkn hawalipi rejesho. Sasa katika hawa niliowakopesha nimewauliza mbona Rais aliwahi kutoa maelekezo penshni zisichelewe inakuwaje?
Majibu yao sasa - Rais ndiyo kasababisha hatulipwi na tena wanadai hali ilivyo waliostaafu kuanzia Mwezi wa Saba Mwaka jana hawatalipwa kwa sababu fedha zinatumika kwenye uchaguzi na Serikali haina fedha.
Sasa hayo sijui ni ya ukweli?
Mkuu, hiki ndicho kizazi kinachoaminika kilipiga sana dili kutokana na hisia zake. Kwa hiyo ukisikia kauli kuwa nchi bado inanyooshwa, wapiga dili, wanufaika wa malipo ya wafanyakazi hewa, mafisadi, na mengine kama hayo. Basi utambue bado kizazi hiki hakijaweza kugusa huruma zake.

Labda tusikilizie kwa wale waajiliwa ktk utumishi wa umma kama watakuwa wameshasamehewa dhambi zao za kupiga dili, kukosa maadili na nidhamu kazini hata waanze kukumbukwa kupata stahiki zao za nyongeza za mishahara na kupandishwa madaraja. Tulio katika sekta binafsi usiseme, muda bado kabisa ndio kwanza tunapita katika utakaso na kitubio cha utiriri wa kodi za TRA hata tuweze kugusa hisia na huruma yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakuta mstaafu kaacha ATM card na namba za siri kwa mkopeshaji mzigo ukitoka jamaa anachana tu ATM card anatoa fedha mstaafu anaambulia kiduchu huu ni utakatishaji.
Walipeni mafao yao kwa wakati muone kama watakopa.
 
Je ktk biashara yako hiyo,unalipa kodi ya serikali?
Nalipa Mkuu ingawa ni indirect kupitia biashara zingine ambazo huwa ndiyo mtu akitaka kukopeshwa nachukua huko hela inayozunguka kwa bishara ninayolipa kodi so akirudisha nairuisha kwenye mzunguko huo na kodi inaendelea kulipwa.
 
Hela kwenye mifuko zimekwapuliwa zimepelekwa kwenye miradi ndugu zangu,mifuko imekauka nadhani wanaachiwa za kulipa mishahara ya staffs na OC ndogo ndogo lakini fedha za kuwalipa wastaafu hamna.
 
Magufuli pamoja kwamba nilimpa kura yangu nimekuja kugundua hakufaa kabisa kuwa raisi
 
Mkopaji na mkopwaji wanategemeana kwa mahitaji
Basi usilaumiwe upande mmoja tu, Mkopaji angekuwa na chaguo mbadala sidhani kama angeingia kwenye mkopo 'onevu', na Mkopeshaji akikosa Mkopaji ataacha kukopesha atafute shughuli nyingine.
 
Hivi hao wastaafu mnaowasema wanakopeshwa kwa lazma au wanaenda wenyewe? Kwanza hao ni wasomi mfano walimu kwanini wasitumie akil zao kujua kwamba hizo hela znariba kubwa? Vile vile mabenki mbona yanatoa mikopo ya wastaafu kwa riba ndogo kabisa kwann wasiende huko wahangaike na hela za moto? Hapa kuna tatizo kwenye wasomi wetu pili kuna tatizi kubwa kwenye serikali coz kwa nn mtu aliyetumikia taifa kwa miaka pengne zaidi ya 30 na baada ya kustaafu ashindwe kununua hata ndala

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukistaafu huwezi kulipwa pensheni mpaka ulipwe kiinua mgongo. Sasa hapa tunaongelea wastaafu hawajalipwa, maana yake hawana hata pensheni. Huko benki unakopaje kama huna mapato rasmi? Maana mfanyakazi anakopa kwa kupitisha mshahara wake katika benki hiyo kwanza
 
Hii ishu haina siasa,inabidi serikali ijitathimini haiwezekani miaka yote kuwe na lawama.

Hivi hii mifuku ambayo imewekewa na msimamizi inashindwa nini kutimiza majukumu yake yaliyo kisheria kabisa.

Ikibidi kuwe na penati/riba kwa kuendelea kushikiria mafao ya mstaafu.

Haiwezekani wao wawapige penati waajiri wanapochelewa kupeleka michango tena hata kuwapeleka mahakamani lakini ikifika wao kutimiza wajibu zao wanafanya kama wanaombwa msaada.

Haikubaliki kuendelea kuwa taifa lisilojali haki za wananchi wake.

Mtumishi miezi sita kabla ya kustaafu anawajibika kuanza taratibu za kulipwa mafao,ikiwa ni pamoja na kupeleka taarifa zote.

Muda unafika,hapewi mafao wala hizo monthly pension. Huu ni upuuzi kuwakopa wastaafu.

Tuheshimu na kuwaenzi wazee wetu kwa michango yao kwa taifa kwa hii mifuko kuwalipa kwa wakati stahili zao.

Ili sisi vijana pia tuone umuhimu na thamani ya hii mifuko,vinginevyo ni sawa na magenge tu ya ya kuwatapeli watumishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom