Suala la watalii kutokurudi tena Tanzania wanapokuja mara moja, huduma zetu ziboreshwe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nchi nyingi zinazotegemea utalii katika uchumi wa Taifa, zimelenga kupata watalii wengi kwa gharama nafuu. Nchi nyingi zinafanya package holiday, ambayo watalii wa kipato cha kawaida wanaimudu.

Si wazungu wote kuwa ni matajiri. Wazungu wanaotalii wengi wanategemea credit cards. Kwa gharama za kuja Tanzania, akirudi kwao inambidi afanye kazi miaka miwili ili kurudisha pesa aliyokopa. Sasa kama huduma ilikua mbovu utalipa pesa huku una kiss meno mpaka unamaliza na ukimaliza unafuta kumbukumbu yote.

Chukulia mtalii anaekwenda Mikumi, kutoka Airport ya JKN mpaka Mikumi kungekua na sehemu ya kuchimba dawa inawezekana Chalinze. Sehemu yenye vyoo, maji, vinywaji na wahudumu wa kueleweka wanaojua lugha za kimataifa.

Mnafahamu wazungu wanavyopenda beer, na hapo ndiyo wako likizo. Wape chaguo la vinywaji, kutokana na package zao. Wale wenye package kubwa wapewe beer bure. Give aways pia. Ni shilingi ngapi inagharimu kushona magauni ya khanga one size kwa wanawake na mashati mfano wa kimono kwa wanaume.

Vyombo vya usafiri, mabasi ya kueleweka yenye viyoyozi. Ukitaka kufanya biashara ni lazima uwekeze kwanza.
 
Azam ferry mimi nalipa 25000 mtalii analipa sio chini ya laki economy kama sijakosea kumbukumbu.

Kuna mrusi mmoja nilikutana nae akawa analalamika sana kuhusu nauli kama hii,nikamuambia wewe ni mtalii ndio maana bei yako tofauti na sisi wazawa.
 
Azam ferry mimi nalipa 25000 mtalii analipa sio chini ya laki economy kama sjakosea kumbukumbu.

Kuna mrusi mmoja nilikutana nae akawa analalamika sana kuhusu nauli kama hii,nikamuambia wewe ni mtalii ndio maana bei yako tofauti na sisi wazawa.
Wakati Mzungu akitoka Ujerumani au Uingereza kwenda Spain anapata package ya ndege na hoteli ya nyota nne karibu na bahari kwa siku 5 kwa €550. Hiyo ni pamoja na breakfast. Mchana kula kwenye cafe €7 unapata lunch na glass ya wine.
 
Akitaka kuja bongo atalipia dola 2000 per night!!

Niliwahi panga kufanya uwindaji wa kitalii hapo nyumbani na wenzangu lakini gharama niliyotajiwa ni mara tatu ya ile ya South Africa. Nika opt kwenda south Africa.
 
Napenda kukiri kwamba kwenye swala la huduma tuko nyuma sana.

Maeneo mengi hakuna lugha nzuri za kibiashara wala huduma za kukufanya utake kurudi eneo lolote la biashara.

Unakuta mtu huna option ndio maana unakwenda mahali,

Ila swala la huduma kuna kazi kubwa Sana ya kufanya,

Mfano mdogo tu ni hayo maeneo ya starehe huko mtaani, unakuta sehemu inavuma ikiwa mpya kwani huduma zinakuwa nzuri ila wakishazoea watu uswahili unarejea biashara inafungwa.

Tubadilike jamani.
 
Kuna kipindi hotel moshi zilikuwa zinalalamika watalii wanakwenda kula mtaani, mtaani chakula rahisi na kina ladha nzuri bei zetu sio rafiki kabisa
Grilled fish anazungushiwa pili-pili hoho pembeni na nyanya, ki pande cha limao unaambiwa 35,000. Hawa watu wanataka kufurahia vyakula vyetu pia.
 
Akitaka kuja bongo atalipia dola 2000 per night!!

Niliwahi panga kufanya uwindaji wa kitalii hapo nyumbani na wenzangu lakini gharama niliyotajiwa ni mara tatu ya ile ya South Africa. Nika opt kwenda south Africa.
Nimeangalia brochure ya Botswana hii Januari wana promotion, siku 9 Kalahari dessert kulala kwenye camps kwa £750 ilikua £900. Hii ni pamoja na flight.
 
Ninaye rafiki mmoja huko nchi za skandnavia huweza kuja hapa nyumbani baada ya kusave kwa miaka isiyopungua mitatu
 
Ninasikia watalii wanapigwa vizinga huko, kuanzia dereva mpaka mtandika vitanda wote ni mwendo wa “my mother sick” my son school-fees, me rent.

Jamani miliangalie hili swala linatutia aibu.
Hii inatokana pia na tabia ya baadhi ya travel agency wa aina fulani kutuponda wabongo wanapokuwa wanatafuta watalii nje ya nchi! Nilishuhudia mtu anaishi London ndio anaiuza Tanzania, hajui watu wake, hajui traditional za wabongo , hajui hata geographical ya nchi ila anashindilia msumari wa ” Dont give tip more that $5 because they are going to drink alcohol and always hide your valuable things because Tanzanian are thieves” sasa huyu mdada mtandika vitanda unaanza kumbania tip yake kuanzia ughaibuni na kamshahara kenyewe ndio hako laki na nusu pamoja na kusafisha vyoo, vitanda vyenye mipira ya kiume iliyotumika, mataulo yaliyofutiwa kila aina ya uchafu unadhani hataomba hela kwa mgeni kweli!!? Tip zenyewe zikiwekwa kwenye tip box management wanaanza na noti kubwa kubwa mnaachiwa zile moja moja mgawane mwisho wa mwezi unaambuli $10 per person tip per month!

Watu wanalishwa ugali dagaa wenye mchanga huko maporini from lunch to dinner breakfast chai ya rangi na andazi!

Wizara fuatilieni huduma kwa hawa wafanyakazi wa mahoteli vile vile muwawekee standard wenye mahoteli & lodges ni aina gani ya watu wawaajiri , pitieni pia vyuooni huko maana ujinga woote unaanzia huko vidada vonapata ajira with no ideas wanaenda kufanya nini but ngono iliwapitisha!

Receptionist ni mchepuko wa meneja , waitress ni mchepuko wa chef nakwambia hayo majibu utapata utajuta kuzaliwa! Suala la discipline kazini nalo changamoto maana hamna vyombo vyakuwashughulikia hawa wahuni kazini kama mwenye property hutakuwa mkali ni hasara kila siku!

Menu zetu nazo za hovyooo yaani hoteli nyingi ni ” deep-fried fish/chicken and chips, rice and beef/ chicken!! Vilivyo orodheshwa kwenye menu vingi havipo zaidi zaidi mhudumu akwambie ngoja nikamuulize chef nae chef anaropoka huko huko jikoni. Vineishaaa!!

Breafing kuhusu tip ziwe resonable! Serikali isitegemee watu wachache kuutangaza utalii kwamfano ikichukua guides wazuri ( siongelei wale wanaojipa tuzo wenyewe kila mwaka) kuna vijamaa vinajua lugha hadi tano za kigeni mpaka kijapani, vinajua tamaduni zetu , vinajua inchi yao ,vinajua kufurahisha wageni, yaani muonekano wao tu unacheka unataka umsikilize, na vinapendwa na wageni sio unapeleka mtu mgeni akimuangalia tu ile body morphology anamkwepa! Wizara iunde tume ya hawa chipukizi wakatangaze utalii huko mtaona majibu!

WIZI RECEPTION - Mgeni analipa cash au kwa card anakuja kupigwa bili nyingine hiyo hiyo siku anacheckout !

VIINGILIO VINAKWAMISHA - Punguzeni viingilio
 
Kigwangala ndiyo aliyakoroga maji kabisa
Unamteua waziri wa utalii kutolea Geita au nzega, anajua utalii au aliuona wapi utalii? Utalii ni professional sio siasa. Hotel za utalii ziko ngapi Geita au nzega? Vyuo vya utalii viko vingapi nzega au Geita? Utalii pia ni nature, exposure, ni ethics, sio kukurupuka. Utalii ni despline ya eneo . Utalii ni nipe nikupe, sio wewe upewe tu. Utalii sio kuangalia nyati na tembo. Porini na kuondoka kurudi ulaya, pia mtalii anapanda babies na totoes wazuri akirudi kwao akasimulie. Jipangeni upya kuhusu utalii nchini
 
Kuna Mzungu nilikutana nae, kumbukumbu yake kubwa ya Tanzania ni chips zege na mishikaki alikula Posta, anasema kile chakula ni kitamu sana. Ni kweli sehemu ya utalii wanapenda utamaduni.
 
Wakati Mzungu akitoka Ujerumani au Uingereza kwenda Spain anapata package ya ndege na hoteli ya nyota nne karibu na bahari kwa siku 5 kwa €550. Hiyo ni pamoja na breakfast. Mchana kula kwenye cafe €7 unapata lunch na glass ya wine.
Kuna watu wanafaidi sana duniani hapa aisee
 
Hii inatokana pia na tabia ya baadhi ya travel agency wa aina fulani kutuponda wabongo wanapokuwa wanatafuta watalii nje ya nchi! Nilishuhudia mtu anaishi London ndio anaiuza Tanzania, hajui watu wake, hajui traditional za wabongo , hajui hata geographical ya nchi ila anashindilia msumari wa ” Dont give tip more that $5 because they are going to drink alcohol and always hide your valuable things because Tanzanian are thieves” sasa huyu mdada mtandika vitanda unaanza kumbania tip yake kuanzia ughaibuni na kamshahara kenyewe ndio hako laki na nusu pamoja na kusafisha vyoo, vitanda vyenye mipira ya kiume iliyotumika, mataulo yaliyofutiwa kila aina ya uchafu unadhani hataomba hela kwa mgeni kweli!!? Tip zenyewe zikiwekwa kwenye tip box management wanaanza na noti kubwa kubwa mnaachiwa zile moja moja mgawane mwisho wa mwezi unaambuli $10 per person tip per month!
Watu wanalishwa ugali dagaa wenye mchanga huko maporini from lunch to dinner breakfast chai ya rangi na andazi!
Wizara fuatilieni huduma kwa hawa wafanyakazi wa mahoteli vile vile muwawekee standard wenye mahoteli & lodges ni aina gani ya watu wawaajiri , pitieni pia vyuooni huko maana ujinga woote unaanzia huko vidada vonapata ajira with no ideas wanaenda kufanya nini but ngono iliwapitisha! Receptionist ni mchepuko wa meneja , waitress ni mchepuko wa chef nakwambia hayo majibu utapata utajuta kuzaliwa! Suala la discipline kazini nalo changamoto maana hamna vyombo vyakuwashughulikia hawa wahuni kazini kama mwenye property hutakuwa mkali ni hasara kila siku! Menu zetu nazo za hovyooo yaani hoteli nyingi ni ” deep-fried fish/chicken and chips, rice and beef/ chicken!! Vilivyo orodheshwa kwenye menu vingi havipo zaidi zaidi mhudumu akwambie ngoja nikamuulize chef nae chef anaropoka huko huko jikoni. Vineishaaa!!
Breafing kuhusu tip ziwe resonable! Serikali isitegemee watu wachache kuutangaza utalii kwamfano ikichukua guides wazuri ( siongelei wale wanaojipa tuzo wenyewe kila mwaka) kuna vijamaa vinajua lugha hadi tano za kigeni mpaka kijapani, vinajua tamaduni zetu , vinajua inchi yao ,vinajua kufurahisha wageni, yaani muonekano wao tu unacheka unataka umsikilize, na vinapendwa na wageni sio unapeleka mtu mgeni akimuangalia tu ile body morphology anamkwepa! Wizara iunde tume ya hawa chipukizi wakatangaze utalii huko mtaona majibu!
WIZI RECEPTION - Mgeni analipa cash au kwa card anakuja kupigwa bili nyingine hiyo hiyo siku anacheckout !

VIINGILIO VINAKWAMISHA - Punguzeni viingilio
Umeeleza vizri ila hilo tatizo sio la wafanya biashara ila ni la serikali, na ni kwaajiri ya shida kubwa nne kwa watanzania wote:

1.Ukosefu wa elimu muhimu ya huduma ya utalii.

2.Lack of exposure (limbukeni) kwa watanzania tulio wengi.

3.Umasikini ulio kithiri na ujinga

4.Sera mbovu za serikali kuhusu biashara katika private sector.

Na hili liko sehemu zote za Tanzani ndo maana wtnia tunadharauliwa na mataifa mengine tukitok nje ya nchi hata hatujamini kama tunaweza.
 
Kama vile imepitiapitia katika hotel industry kamanda yaani nimewahi kuwa sehemu flani hivi napiga kazi enzi za TAHI haya unayoyasema ni kweli kabisa nakumbuka tour guide mmoja alimwambia mtalii usiwape tips hotel inawakata pesa kwa ajili ya huduma mnayopewa/ service charges/

Back
Top Bottom