Hii inatokana pia na tabia ya baadhi ya travel agency wa aina fulani kutuponda wabongo wanapokuwa wanatafuta watalii nje ya nchi! Nilishuhudia mtu anaishi London ndio anaiuza Tanzania, hajui watu wake, hajui traditional za wabongo , hajui hata geographical ya nchi ila anashindilia msumari wa ” Dont give tip more that $5 because they are going to drink alcohol and always hide your valuable things because Tanzanian are thieves” sasa huyu mdada mtandika vitanda unaanza kumbania tip yake kuanzia ughaibuni na kamshahara kenyewe ndio hako laki na nusu pamoja na kusafisha vyoo, vitanda vyenye mipira ya kiume iliyotumika, mataulo yaliyofutiwa kila aina ya uchafu unadhani hataomba hela kwa mgeni kweli!!? Tip zenyewe zikiwekwa kwenye tip box management wanaanza na noti kubwa kubwa mnaachiwa zile moja moja mgawane mwisho wa mwezi unaambuli $10 per person tip per month!
Watu wanalishwa ugali dagaa wenye mchanga huko maporini from lunch to dinner breakfast chai ya rangi na andazi!
Wizara fuatilieni huduma kwa hawa wafanyakazi wa mahoteli vile vile muwawekee standard wenye mahoteli & lodges ni aina gani ya watu wawaajiri , pitieni pia vyuooni huko maana ujinga woote unaanzia huko vidada vonapata ajira with no ideas wanaenda kufanya nini but ngono iliwapitisha!
Receptionist ni mchepuko wa meneja , waitress ni mchepuko wa chef nakwambia hayo majibu utapata utajuta kuzaliwa! Suala la discipline kazini nalo changamoto maana hamna vyombo vyakuwashughulikia hawa wahuni kazini kama mwenye property hutakuwa mkali ni hasara kila siku!
Menu zetu nazo za hovyooo yaani hoteli nyingi ni ” deep-fried fish/chicken and chips, rice and beef/ chicken!! Vilivyo orodheshwa kwenye menu vingi havipo zaidi zaidi mhudumu akwambie ngoja nikamuulize chef nae chef anaropoka huko huko jikoni. Vineishaaa!!
Breafing kuhusu tip ziwe resonable! Serikali isitegemee watu wachache kuutangaza utalii kwamfano ikichukua guides wazuri ( siongelei wale wanaojipa tuzo wenyewe kila mwaka) kuna vijamaa vinajua lugha hadi tano za kigeni mpaka kijapani, vinajua tamaduni zetu , vinajua inchi yao ,vinajua kufurahisha wageni, yaani muonekano wao tu unacheka unataka umsikilize, na vinapendwa na wageni sio unapeleka mtu mgeni akimuangalia tu ile body morphology anamkwepa! Wizara iunde tume ya hawa chipukizi wakatangaze utalii huko mtaona majibu!
WIZI RECEPTION - Mgeni analipa cash au kwa card anakuja kupigwa bili nyingine hiyo hiyo siku anacheckout !
VIINGILIO VINAKWAMISHA - Punguzeni viingilio