Suala la watalii kutokurudi tena Tanzania wanapokuja mara moja, huduma zetu ziboreshwe

Bongo bei kulingana na rangi yako Ili hata serikali inasapoti ubaguzi huu angalia viingilio vya mbuga zetu mweupe upigwa bei mara tatu ya mweusi iwe kuingia au kulala hotel mbugani Hali usingizi ni ule ule.Pia ni ubaguzi na ukaburu kuandika tena bei Bila aibu eti foreigner....usd ... Domestic ...T sh... Halafu tuanze sisi weusi kukomesha ubaguzi
 
Ndio utalii huo sasa🤣
Pia muhimu kuongeza ubunifu wapate vitu vipya Ili wakumbuke kurudi mfano lile supu la pweza uwavutia Sana watalii kuipenda Zanzibar,ni kuongezea tu vitu vitu vipya Kama alkasusu almujarab,vumbi la congo,mundende nk.
 
Ninasikia watalii wanapigwa vizinga huko, kuanzia dereva mpaka mtandika vitanda wote ni mwendo wa “my mother sick” my son school-fees, me rent.

Jamani miliangalie hili swala linatutia aibu.
Tena balaa sana,zamani nilidhani watalii wana pesa sana kumbe wanaumia hatari,
Ndo hvyo kaka,ile mentslity ya kwamba wazungu wana hela inatufanya tufanye mambo ya ajabu sisi watz
 
Buckingham Palace anapoishi Malkia Elizabeth II, wakati wa kiangazi wanaruhusu watalii kuingia. Bei ni moja kwa wote na wanauza pia vitu vidogodogo kama mifuko, vikombe kalamu nk zenye picha za wanafamilia. Unapata kumbu kumbu.
 
Sasa huo ndo utalii,mzungu akale vibandani hasa aone maisha ya hawa watu wa sehemu anayotalii.

Kutalii sio mazingira tuu hata vyakula pia abadilishe pia ni utalii wa vyakula huo.

Utalii wa maeneo pia watembelee maeneo ya waswahili maeneo asilia ya kijogradia huu ndo utalii.

Na gari pia wangekwea daladala wangebanana na kusimama kama sisi hii ni utalii pia anasoma mazingira na kujua tunaishi vipi,sio unampakia kwenye basi yako ya kiyoyozi anaangalia tu mazingira alafu anasema katalii,ndio maana wengi sasa hivi wanajichanganya uswahilini.

MUHIMU VIBANDA VIWE NA USAFI TU AU VILE VIMGAHAWA STANDARD KIDOGO WALI ALFU 5000 MZUNGU HASHINDWI.

Kuna demu mmoja mfilipino ni fariki angu wa kitambo huwa ananiambia kuwa anakuwa anapenda ugali lakini hajui tu kupika ila kuna sehemu huwa anaenda kula ugali,sasa hii ni faida kubwa kwetu wamejua kama kuna ugali na wanakula
 
Hiyo ndio sababu kubwa sana waombaji hawana aibu
Ninasikia watalii wanapigwa vizinga huko, kuanzia dereva mpaka mtandika vitanda wote ni mwendo wa “my mother sick” my son school-fees, me rent.

Jamani miliangalie hili swala linatutia aibu.
 
Sio watalii peke yao ndio wanaibiwa mwarabu muhindi wanaishi tanzania akiingia duka la mwafrika mtanzania huwa bei anampandishia mwarabu na muhindi. Ukimuita fundi atakupa bei kubwa lakini ukimtuma mswahili mwenzao apatane nao bei unapewa ndogo. Trafick akimuona muhindi au mwarabu lazima amsimamishe aanze kumkagua sana
 
muarabu umparamie na bei yako ya kihaya wakati kazaliwa na kukulia nzega,hapo ndio utakuwa umejichanganya[emoji38][emoji38]
 
Unauwaje utalii ambao tayari ulishakufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…