KERO Suala la Watoto katika baadhi ya Shule jijini Mwanza kuendelea na masomo hata wakati wa likizo ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba sauti ya wazazi ifikishwe kwa mamlaka za elimu katika Mkoa wa Mwanza kuhusu suala linalohusu baadhi ya shule kuendelea na masomo hata wakati wa likizo rasmi za wanafunzi.

Kumekuwa na taarifa kwamba baadhi ya shule zinaendelea na ratiba za masomo wakati wa likizo, hali ambayo imeibua maswali na wasiwasi miongoni mwa wazazi. Wazazi wanapofuatilia sababu za utaratibu huo, huambiwa kuwa lengo ni kuandaa matokeo bora kwa wanafunzi.

Hata hivyo, tunajiuliza kwa nini mamlaka za elimu ziliweka utaratibu wa likizo kwa wanafunzi kama likizo hizo hazitekelezwi kwa mujibu wa makusudio yake ya msingi. Likizo zimekusudiwa kuwapa wanafunzi muda wa kupumzika, kujijenga kiakili na kimwili, pamoja na kujifunza stadi nyingine za maisha nje ya darasa.

Tunasisitiza kuwa watoto wanahitaji muda wa kupumzika ili kuondoa msongo wa masomo na pia kupata nafasi ya kujifunza ujuzi wa ziada utakaowasaidia kukabiliana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia duniani. Ni ukweli kwamba elimu ya darasani pekee haitoshi katika kumwandaa mtoto kikamilifu kwa maisha ya baadaye.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba mamlaka husika za elimu katika Mkoa wa Mwanza zifuatilie kwa karibu suala hili ili kuhakikisha kuwa ratiba za likizo zinaheshimiwa na shule zote zinafuata miongozo iliyowekwa kwa usawa na kwa maslahi mapana ya wanafunzi.
 
Bwana wee tutalaumu bure watoto kutokupenda shule ila ukweli ni kwam a hatuwatendei haki watoto wa sasa.....mijitu yenyewe basi ata tungekuwa tunaongoza dunia kwa akili wapi ndio kwanza tunaburuza mkia kutesa watoto tuu
 
Tunaomba sauti ya wazazi ifikishwe kwa mamlaka za elimu katika Mkoa wa Mwanza kuhusu suala linalohusu baadhi ya shule kuendelea na masomo hata wakati wa likizo rasmi za wanafunzi.

Kumekuwa na taarifa kwamba baadhi ya shule zinaendelea na ratiba za masomo wakati wa likizo, hali ambayo imeibua maswali na wasiwasi miongoni mwa wazazi. Wazazi wanapofuatilia sababu za utaratibu huo, huambiwa kuwa lengo ni kuandaa matokeo bora kwa wanafunzi.

Hata hivyo, tunajiuliza kwa nini mamlaka za elimu ziliweka utaratibu wa likizo kwa wanafunzi kama likizo hizo hazitekelezwi kwa mujibu wa makusudio yake ya msingi. Likizo zimekusudiwa kuwapa wanafunzi muda wa kupumzika, kujijenga kiakili na kimwili, pamoja na kujifunza stadi nyingine za maisha nje ya darasa.

Tunasisitiza kuwa watoto wanahitaji muda wa kupumzika ili kuondoa msongo wa masomo na pia kupata nafasi ya kujifunza ujuzi wa ziada utakaowasaidia kukabiliana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia duniani. Ni ukweli kwamba elimu ya darasani pekee haitoshi katika kumwandaa mtoto kikamilifu kwa maisha ya baadaye.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba mamlaka husika za elimu katika Mkoa wa Mwanza zifuatilie kwa karibu suala hili ili kuhakikisha kuwa ratiba za likizo zinaheshimiwa na shule zote zinafuata miongozo iliyowekwa kwa usawa na kwa maslahi mapana ya wanafunzi.
Hata jijini mtwara watoto wanaambiwa waende shule.

Sujui kwanini shule za private zinaamini sana kutengeneza vijana ambao ni too bookish but street aint smart.
 
Back
Top Bottom